DOKEZO Kashfa kubwa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kanisa latumika kuwauzia mashamba hewa waumini wake. Ekari feki 15,000 ziliuzwa

DOKEZO Kashfa kubwa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kanisa latumika kuwauzia mashamba hewa waumini wake. Ekari feki 15,000 ziliuzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani limeingia kwenye kashfa kubwa ya utapeli baada ya makanisa yake ya Kijitonyama, Salasala, Mwenge, Ubungo na Mbezi Beach kuwauzià waumini wake mashamba feki yaliyopo Bagamoyo.

Mashamba hayo yenye zaidi ya heka 15,000 yalikuwa yakiuzwa kwa shilingi laki tano na sitini elfu kwa heka ambapo heka zote zilizopangwa kuuzwa ziliuzwa na baadhi ya waumini wengine hadi leo hawajawahi kupewa wala kuonyeshwa mashamba yao.

Malipo ya mauzo ya mashamba hayo yalifanyika kupitia account za kanisa hilo, kumbe ardhi inayouzwa ni mali ya Ranch za Taifa huku kanisa hilo likijua fika uhuni huo.

Katika kijiji cha Fukayose, Ranch imesema itaachia heka mia tu kwa kijiji. Kwenye kijiji cha Fukayose Ranch ina heka 3000.

Heka nyingine zimesambaa kwenye vijiji mbalimbali wilayani Bagamoyo.


View attachment 2639510
Viongozi makanisa wanapend hela kuliko chochote na hiyo ndio tabia ya wakirito wote waliomo serikalini kazi ufisadi tu
 
Nimeziona na namm nimezungumza kile ninachokijua na kukishuhudia, siwezi kuthibitisha hayo ya wengine
Niliwahi kuipenda sana KKKT sana tuu. Ila malasusa na Genge lake kwanza walianzisha sadaka zisizo na mpangilio then wakaja kupora kiti cha mtu huku konde nimejiunga na warutheli wa africa mashariki na naendelea kumuabudu Mungu kwa furaha na uhuru
 
Si muumini wa kanisa hilo lakini naamini huwezi tapeliwa mpaka hapo. Umelipa 500,000 kwenye akaunti inayofahamika ya taasisi, jina la akaunti uliandika la taasisi, una bank slip ya malipo yenye mhubiri wa kupokea pesa kwa tarehe husika. Unatapeliwaje?

Kuna upande haujafanya kazi yake vizuri au kanisa ndio limetapeliwa na kwa vyovyote litawajibika kuwarejeshea pesa endapo mambo hayataenda sawa. Unaweza kuta taasisi ndio imepigwa na wahuni ingawa yawezekana walikuwa na nia nzuri tu kuelekea waumini wake

Ila ikiwa pamoja na ushahidi mlio nao kanisa limekataa kuhusika na mpango huo, hapo mtakuwa na haki ya kuilaumu taasisi ya dini kwa utapeli.
usitetee upuuzi, KKKT miaka ya hivi karibuni limekua kanisa la ovyo sana. Mbey washaivuruga vipande vipande
 
Kwa kawaida taasisi kama KKKT huwa inafanya mambo yake kwa usahihi kulinda heshima yake. Yawezekana mpango wa kanisa ni mzuri ila watekelezaji wameenda kinyume na maadili.
Hakuna cha usahii walijua kuwa haya maeneo sio yao tu wachungaji kwa hela ni zaidi ya hatari
 
Hakuna Kanisa linafanya haya, atakuwa ni muhuni Mmoja wa Kanisan, muwage mnaheshimu watu na kutosema vitu ambavyo hamna ushahidi navyo
Mchungaji gani asie penda hela tena za Magumashi mpaka wamepandikiza watu wao serikalini hili wapige hela
 
Nidhani nimepigwa peke yangu mkazi wa hapa JF. Jamaa walinikomba 10,200,000/-
Kufanya biashara na kanisa ni kujitafutia kutapeliwa
 
Kinachofanyika sasa hivi ni wajanja wachache wanaenda ardhi wanaangalia maeneo yote yaliyotelekezwa na mashirika na taasisi mbalimbali za serikali hata kama ni miaka 40 lakini hati zao hazijafutwa kamailivyotokea Mabwepande kwenye eneo la DDC. Basi zinaundwa "syndicate" kwa kupitia viongozi wachache wa chama na serikali wasiokuwa waaminifu basi kazi inaanza. Kitachofuata hapo utaandaliwa muhtsari feki kuwa wanachi wamekubali kulipa sqm 1 TZS 4,000 jamaa watakusanya pesa watagawana. Haiingii akilini kabisa eti leo Bagamoyo na hususani Fukayosi ilivyojengeka eti leo wakafufue ranchi wakati ranchi kibao serikali imeshindwa kuziendesha.
 
usitetee upuuzi, KKKT miaka ya hivi karibuni limekua kanisa la ovyo sana. Mbey washaivuruga vipande vipande
Mkuu una hasira sana na KKKT. Mimi si mmoja wao ila huoni wapuuzi ni wale wanaovumilia uhovyo wake? Angalia vizuri nilichoandika
 
Wewe unaonekana una CHUKI KUBWA na KKKT

KKKT kwa ninavyowajua hawawezi kufanya uzembe kama huo, labda waliouziwa kuna terms hawakuzifuata vizuri
 
Mbona mi nshapewa mpaka hati yangu ya eka 5 sa itakuwaje ?
 
Back
Top Bottom