Mikuki na wengine wana JF wapendwa:
Nikutoeni wasiwasi kuwa madamu thread hii ni ya siasa haiepukiki kwamba kuna watu wataegemea upande fulani wa kiitikadi. Lazima kutakuwa na angalau makundi matatu: upinzani, CCM na wale wasio na upande.
Ukiangalia mtiririko wa hoja hapa, utagunda mambo yafuatayo:
Kwanza kuhusu CHADEMA, mambo mawili ni bayana:
i) wanachama wa chadema hawajawahi kujificha, wapo wazi kwa uanachama wao na mawazo yao pia
ii) Ni kweli kabisa kuwa kama alivyosema Mugongomugongo sisi chadema tumekuwa tukiongoza katika kuikosoa na kuizodoa serikali ya CCM. Kwa hili hatuna cha kuomba msamaha maana ni sehemu ya kazi yetu kama chama cha upinzani. Kama alivyosema Ngurumo katika makala yake ya Jumatano ya juzi, wanaosifu CCM na serikali yake wapo wengi, waacheni watu wachache wenye ujasiri waikosoe.
Kuhusu wenzetu wa CCM-mambo mawili ni bayana pia:
i) wale ambao kwa njia moja au nyingine wapo CCM wamekuwa wakijificha. Hawataki kuweka identity zao wazi. Isipokuwa kwa matendo yao na hoja zao utawajua kuwa hawa ni ama ni CCM au ni serikali moja kwa moja. Hawa ni the likes wa akina Mugongomugongo . Mtu pekee aliyeweka bayana kuwa yeye ni CCM hapa ni Mzee ES. Watu wengi waliopo CCM hawapendi kujulikana kuwa wao ni CCM, na hii ni aibu! Kama wewe ni mpenzi na mwanachama wa chama fulani, sioni sababu ya kujificha unless upo katika taasisi ambazo ni kinyume cha sheria kuji-identify na chama fulani
ii) wenzetu wa CCM wamekuwa wepesi na wajuzi wa kututoa katika mada inayojadiliwa ili kupunguza makali ya mashambulio na uumbuliwaji kwa serikali. Kwa hiyo wenzetu wa CCM kwa kweli hawana kabisa uwezo wa kujibu mashambulizi yanayoelekezwa kwa chama chao, zaidi ya kutafuta njia ya kuyeyusha mada inayokuwa imeelekezwa kwao. Kwa kifupi, CCM wamezoea ujanjaujanja, hawana uwezo wa kukabili hoja. Sasa hivi tunashambulia budget kule kwenye mada husika wao wapo kimya kabisa, hawana hoja za kujibu, wamebaki na Zitto wakiongozwa na rafiki yangu Mzee ES.
Kuhusu itikadi za wachangiaji hapa, ni kwamba haiwezekani kuwazuia wana JF wote kutokuwa na upande. Wengine hatuamini katika kuwa neutral, na popote tuendapo huwa hatuwezi kuficha uanachama na upenzi wa vyama vyetu. Kwa hiyo adm hana kabisa uwezo wa kutuzuia sisi kuonesha itikadi zetu. Kama hatutatofautiana kivyama, kiitikadi, kifalsafa na kisera hivi msingi wetu wa debate utakuwa ni upi hasa?
Ndugu Mikuki na wengine, naomba muelewe kuwa tukishashindwa kujitofautisha kiitikadi, kifalsafa na kisera, matokeo yake itabidi tujadili pua na masikio ya watu. Ndio maana katika forum hii utaona kwamba zile mada zinazohusu watu zinajaa haraka na kudumu muda mrefu kuliko mada zinahusu maswala na falsafa za siasa na uongozi. Njia moja ya kuepuka kujadili watu ni kuangalia mambo kwa upeo wa kiitikadi, kifalsafa na kisera. Hapo ukitaka kujadili jambo hutaangalia nani kasema bali nini mantiki ya jambo lenyewe.
Kwa hiyo ndigu yangu Mikuki usihofu, kujitambulisha kiitikadi na kivyama sio tu kuwa ni ruksa bali ni muhimu sana pai!