Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Huyo Mungu wako wewe.. Mungu wangu mimi hana ubovu..
Ndiyo yule waliompelekea maombi na mwanakjj? ili JK apate mabalaa. walisema ugonjwa wa homa ya ndege usiondoke ili wananchi waone CCM si lolote na iwe bakora kwa JK. migomo izidi. kweli ilikuwa misa ya kijinga sana. hakukuwa na comments.
tuko nao mzee masatu.
 
Mswahili,
Mwanzoni nilikuwa nashangaa na pengine kutokuelewa maudhui ya michango yako ktk JF. Lakini sasa ndio nimekuelewa ni mtu wa aina gani kutokana na kile unachokiandika.
Unahalalisha kabisa tuhuma za upande mmoja na kuchanganya mambo yasiyohusiana nayo kwa maslahi yako binafsi.
Acha hizo.

Kwako Chakaza na Wana JF wote,

Nadhani wakati umefika wa kutumia busara na hikma za Mheshimiwa Spika Samuel Sitta kuhusiana na hoja kengeufu za Ndugu yetu Mswahili.

"MPUUZI MPUUZE|"
 
Wanabodi,
Tukumbukeni kuwa huyu jamaa Dr.Nchimbi sii mchezo mdogo?.. Mzee Es unakumbuka ya Ippy, yalianza hivi hivi watu wakicheka na kusema ovyo...
Mwanakijiji has a point, jamani tusichanganye vitu hapa kuepuka ku-face ukweli.
 
Mswahili,
Sikujua Mkandara ameshajiunga na Chadema. Kadi ulimpa lini?
 
kama wanaweza kufanya hivi kwa MP mjue yanayewe kumkuta yeyote. Mkakati wao uko hivi:

a. Hali ya Amina itaendelea kuwa mbaya na hivyo kumfanya ashindwe kutimiza mambo fulani ya kibunge. Hata hivyo mtakuwa mnasikia after the fact, Amina amefanya hivi au amefanya vile.

b. Habari za uhakika zinazopenyezwa kwa wenu mtiifu ni kuwa Amina bado hajabadili msimamo wake wa kutaka kuzungumza kwani anadai kitendo alichofanyiwa "kinamuuma" na ameapa kuwa "atakula nao sahani moja" wale wote waliohusika na kuvunja nyumba yake. Habari hizo za uhakika zinasema Mhe. Amina alikuwa anapanga kutumia Bunge la bajeti kama jukwaa la "kumpaka" kiongozi mmoja wa ngazi za juu.

c. Licha ya ushawishi wa wazazi na baadhi ya "wazee" wa chama waliokwenda kukutana na mheshimiwa huyo, licha ya kuahidi kuwa hatamwaga mtama hadharani, wazee waliondoka wakiwa na hisia kuwa AC alikuwa anawaambia tu.. lakini ameshaamua cha kufanya.

d. Hapa ndipo penye tatizo kwani hawawezi kumwacha awe peke yake au akutanane na waandishi wa habari hata wa jambo lolote lile. Mmoja wa wakubwa hao amesikika akisema AC ni "loose canon".

Njia moja kubwa wanayotaka kutumia ni kumpa kawadhifa kaina fulani ka kumtuliza, kuhakikisha anarudiana na Medi, na mhusika wa njama za kuvunja ndoa kupewa karipio kale la kuacha kuleta mambo ya ndoa za watu serikalini. Mhusika huyo EN hii sasa anatembea kwa kuinamisha kichwa na baadhi ya wabunge wenzake wanamkwepa. Hata alipoingia Bungeni "hakushangiliwa" kwa kitendo chake hicho..

la mwisho ni uwezekano wa Mhe. Amina kujiuzulu au kudaiwa kula njama na wapinzani na hivyo chama kitamtosa!. Ukweli ni kuwa AC amekuwa kwa CCM an Enigma!
 
Shusha data "Shigongo"! Shusha! Ila sasa rekebisha ka-discrepancy kadogo hapo: umekuwa ukisema Amina amekuwa "mental" na hali yake ni mbaya sana, halafu sasa unasema she held negotiations na CCM bigwigs over her terms of "release"!

Halafu umesema:
Mhusika huyo EN hii sasa anatembea kwa kuinamisha kichwa na baadhi ya wabunge wenzake wanamkwepa

Hapa mkubwa unatupiga fix kwasababu juzi tuliona kwenye magazeti matatu picha ya Nchimbi akiwa ameshikana mikono na Mbunge John Komba wakicheka wakielekea mahali. Ikumbukwe kwamba Komba, na sio EN, ndiye rafiki mkubwa wa Mpakanjia. (Nadhani ndiye aliyekuwa mshenga wake kwa Amina).

Sasa hii kauli ya kusema Nchimbi anakimbiwa na Wabunge wenzake ni ya kutuongopea na kutufanya watoto wadogo. Bahati nzuri tumeona hiyo picha. Mkubwa upo Michigan, saa nyingine wanaokupa huu udaku wanatia chumvi kidogo, kwahiyo na wewe kuwa makini kidogo.
 
Admin, Mimi nilijiunga kwenye hii forum bila kukaribishwa wala kushurutishwa, bali umahiri wa hoja na utashi wangu ndo vilinisukuma kuingia humu. Kweli lazima nikiri nimejifunza mengi sana sana humu na nina imani wenzangu na mie tumejifunza na tutazidi kujifunza! Bila unafiki I have learnt alot from Mwanakijiji, Mkandara, ES, Mswahili, Kichuguu, TZ njema, Masatu... na wengi chungu nzima. I salute all members of this forum! Wakati huo huo, wengine tumejifunza kutoa hoja, hata tunapoteleza tumevumiliwa!..kweli I RESPECT THIS FORUM na sijui kama hata kama ingeanza nyingine itakuwa na mvuto kama hii!

Lakini shida kubwa sana ambayo nimei-experience siku nyingi ni hii..kwa nini humu watu mkitofautiana kwa hoja...directly unakuwa branded kwamba wewe ni either Chadema au CCM? Nauliza kwa sababu mimi ni muumini wa Tanzania na wala sina chama, bali naamini katika chochote/yeyote anayeweza kutuletea ukombozi katika maisha yetu sisi walala hoi..whether its JK, FM, J Mbatia etc..ilmradi..mwenye vision! I will give him my thumb....

Naomba kuchukua nafasi hii, kukuuliza wewe admin, hii forum ina uhusiano gani na Chadema/CCM au vyama vya siasa? Kwani kila mara inaonekana whenever mtu ukitoa hoja inayopingana na mtu..unaambiwa wewe ni chadema/CCM...To me, lazima nikiri, Iam not happy kwa sababu..nilikuwa najua from day one naingia kwamba hii Forum ni Independent na haina ideology yoyote! Na wewe kama mkubwa wa hii forum umechukua hatua gani kuwaonya wanachama na wachangiaji kujifunza kuvamia hoja na si watu binafsi? Na kama hii forum ni ya Chadema/CCM au mna working relationship..let me know so that I can fully adjust to the new revelations of the status.

Tafadhali niondolee wasi wasi

NI MIMI MSOMAJI NA MCHANGIAJI WA JF
Mikuki
 
Mkuu Mwanakijiji,

Mimi nimeshindwa kuelewa kwenye hii thread unataka kuongelea nini? Mbona kama haya ni mambo binafsi ya Amina na familia yake?

Kuumwa pia ni mambo binafsi. Sioni tofauti ya hii thread na ile ya kule kwa Zitto.

Labda nifafanulie kwanini unaona hapa kuongelea mambo ya Amina ni ruksa lakini kule kuongelea ya Zitto ni mambo binafsi?
 
Mikuki,

Of course swali umelielekeza kwa Admin, lakini niwie radhi nitoe maoni yangu kwenye hili:

Toka nianze kuingia humu muda mrefu kidogo, somehow, the dominant views were those of CHADEMA. Mnyika was popular in here. Zitto, using a different name, as well. Trend ilikuwa ni kulaani everything kuhusu Serikali na CCM. Then, zikatokea few voices hapa na pale. Those few voices ndio zikaanza kuwa branded CCM - or mamluki or whatever. Mie ni mmojawapo. Nilivyompinga Mbowe nilifurumushiwa matusi na kwamba ni mamluki and so on and so on. Baadaye busara ikaanza kuingia kwenye Forum, waungwana wakaanza kusema "wait a minute, mbona kuna unafiki hapa". Sasa hapa ndipo tulipofikia.

Hii habari ya kuita watu mamluki ni tabia iliyojikita ndani ya CHADEMA (mfano, Ngurumo waandishi wote wanaoandika mema kuhusu Serikali, hata kina Bagenda, anawaita mamluki!). Hapa ndipo tulipofikia.
 
Mkuu Mwanakijiji,

Mimi nimeshindwa kuelewa kwenye hii thread unataka kuongelea nini? Mbona kama haya ni mambo binafsi ya Amina na familia yake?

Kuumwa pia ni mambo binafsi. Sioni tofauti ya hii thread na ile ya kule kwa Zitto.

Labda nifafanulie kwanini unaona hapa kuongelea mambo ya Amina ni ruksa lakini kule kuongelea ya Zitto ni mambo binafsi?

Haya ni maswali ya msingi na natumai huyu Bwana atayajibu kwa ufasaha!
 
Mwakjj

Tukisema una double standards tunaambiwa tunatukana. Kama mambo binafsi hayafai kujadiliwa humu iweje sasa unatuletea hizo habari za ugonjwa wa akili wa Amina hapa? Hujui kuwa masuala ya ugonjwa wa mtu ni siri baina yake (familia) na daktari wake?

Wewe endelea kutuburuza tu.....
 
Shusha data "Shigongo"! Shusha! Ila sasa rekebisha ka-discrepancy kadogo hapo: umekuwa ukisema Amina amekuwa "mental" na hali yake ni mbaya sana, halafu sasa unasema she held negotiations na CCM bigwigs over her terms of "release"!

Mkuu, nawe umeingia kwenye mtego wa kupachika watu majina?! Waachie wenyewe hii, achana nayo si tabia nzuri, ushauri tu!
 
Mikuki na wengine wana JF wapendwa:

Nikutoeni wasiwasi kuwa madamu thread hii ni ya siasa haiepukiki kwamba kuna watu wataegemea upande fulani wa kiitikadi. Lazima kutakuwa na angalau makundi matatu: upinzani, CCM na wale wasio na upande.

Ukiangalia mtiririko wa hoja hapa, utagunda mambo yafuatayo:

Kwanza kuhusu CHADEMA, mambo mawili ni bayana:

i) wanachama wa chadema hawajawahi kujificha, wapo wazi kwa uanachama wao na mawazo yao pia

ii) Ni kweli kabisa kuwa kama alivyosema Mugongomugongo sisi chadema tumekuwa tukiongoza katika kuikosoa na kuizodoa serikali ya CCM. Kwa hili hatuna cha kuomba msamaha maana ni sehemu ya kazi yetu kama chama cha upinzani. Kama alivyosema Ngurumo katika makala yake ya Jumatano ya juzi, wanaosifu CCM na serikali yake wapo wengi, waacheni watu wachache wenye ujasiri waikosoe.

Kuhusu wenzetu wa CCM-mambo mawili ni bayana pia:

i) wale ambao kwa njia moja au nyingine wapo CCM wamekuwa wakijificha. Hawataki kuweka identity zao wazi. Isipokuwa kwa matendo yao na hoja zao utawajua kuwa hawa ni ama ni CCM au ni serikali moja kwa moja. Hawa ni the likes wa akina Mugongomugongo . Mtu pekee aliyeweka bayana kuwa yeye ni CCM hapa ni Mzee ES. Watu wengi waliopo CCM hawapendi kujulikana kuwa wao ni CCM, na hii ni aibu! Kama wewe ni mpenzi na mwanachama wa chama fulani, sioni sababu ya kujificha unless upo katika taasisi ambazo ni kinyume cha sheria kuji-identify na chama fulani

ii) wenzetu wa CCM wamekuwa wepesi na wajuzi wa kututoa katika mada inayojadiliwa ili kupunguza makali ya mashambulio na uumbuliwaji kwa serikali. Kwa hiyo wenzetu wa CCM kwa kweli hawana kabisa uwezo wa kujibu mashambulizi yanayoelekezwa kwa chama chao, zaidi ya kutafuta njia ya kuyeyusha mada inayokuwa imeelekezwa kwao. Kwa kifupi, CCM wamezoea ujanjaujanja, hawana uwezo wa kukabili hoja. Sasa hivi tunashambulia budget kule kwenye mada husika wao wapo kimya kabisa, hawana hoja za kujibu, wamebaki na Zitto wakiongozwa na rafiki yangu Mzee ES.

Kuhusu itikadi za wachangiaji hapa, ni kwamba haiwezekani kuwazuia wana JF wote kutokuwa na upande. Wengine hatuamini katika kuwa neutral, na popote tuendapo huwa hatuwezi kuficha uanachama na upenzi wa vyama vyetu. Kwa hiyo adm hana kabisa uwezo wa kutuzuia sisi kuonesha itikadi zetu. Kama hatutatofautiana kivyama, kiitikadi, kifalsafa na kisera hivi msingi wetu wa debate utakuwa ni upi hasa?

Ndugu Mikuki na wengine, naomba muelewe kuwa tukishashindwa kujitofautisha kiitikadi, kifalsafa na kisera, matokeo yake itabidi tujadili pua na masikio ya watu. Ndio maana katika forum hii utaona kwamba zile mada zinazohusu watu zinajaa haraka na kudumu muda mrefu kuliko mada zinahusu maswala na falsafa za siasa na uongozi. Njia moja ya kuepuka kujadili watu ni kuangalia mambo kwa upeo wa kiitikadi, kifalsafa na kisera. Hapo ukitaka kujadili jambo hutaangalia nani kasema bali nini mantiki ya jambo lenyewe.

Kwa hiyo ndigu yangu Mikuki usihofu, kujitambulisha kiitikadi na kivyama sio tu kuwa ni ruksa bali ni muhimu sana pai!
 
silencing of an mp - inaweza kumaanisha kanyamazishwa na vile vile kasailensisha mwenyewe !! sasa sijui ipi hapa unasemea wewe !!
halafu hiyo sidhani kabisa kama ndio ishu yenyewe, yaani kumnyamazisha, kama kweli wangetaka kumnyamazisha sidhani hata kama huo ubunge angeukwaa, mie nadhani anasubiri moto uliowaka upoe na atoke upya lakini hilo la kusema amenyamazishwa nalipinga, umeenda mbali mno kufananisha na anna nicole smith ( kama alivyosema glenn beck mwenyewe ) kama ni hivyo, basi kila kitu tunaweza kufananisha na marehemu anna nicole smith, both kwa wanawake na wanaume !
chifupa atatoka tu upya nani aliyekwambia kanyamazishwa na kama ikitokea hiyo uliyosema yote ni kazi ya mola kwani mimi na wewe pia vile vile wakati wetu ukiwadia tutarudisha namba !!
 
Kadampinzani... haya mimi nimeshanyanyua bendera ya tahadhari. Anachofanyiwa Amina kimuudhi Mtanzania yeyote yule na kutaka kama ni mgonjwa aruhusiwe kumuona daktari, kama anataka kukutana na mtu yeyote au kuzungumza na mtu yeyote awe huru kufanya hivyo. Na kama hataki kuzungumza basi aachwe aendelee na mambo yake, mimi siko kwenye watu watakao'mlazimisha azungumzie kilichojiri" kwani kashema hadharani kwamba hakukuwa na kitu hicho na ninaamini. Hilo jingine la njama za kiongozi wa CCM hilo akitaka kulizungumzia basi aachwe asipotaka basi aachwe aseme kabadili mawazo. Lakini kitendo cha kumuwekea minders, kuingilia mawasiliano yake binafsi ni kitendo kisichokubalika kabisa.
 
Huyo Mungu wako wewe.. Mungu wangu mimi hana ubovu..

I know you, na wala sikusema Mungu ana ubovu.

Najua kuwa una tatizo na mimi personally, na of course siwezi kukuzuia. Ukipost vitu vya maana vinavyoelemisha kwa namna yoyote ile nitavisoma na kujifunza, na ukitoa matusi dhidi yangu nitayadharau.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom