Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
Mtaliki wa Chifupa azungumza
*Asema hakushawishiwa kumwacha mkewe
*Asema anamwachia Mungu kila kitu
Na Waandishi Wetu
MTALIKI wa Mbunge wa Viti Maalum, Amina Chifupa, Mohamed Mpakanjia, amejitokeza hadharani na kusema hakushawishiwa na mtu yoyote kumtaliki mkewe wa zamani.
Mpakanjia aliliambia gazeti hili jana kuwa uamuzi wa kumtaliki mkewe aliuchukua baada ya tafakuri binafsi na kwamba hakuna mtu yeyote aliyemshawishi kuchukua hatua hiyo.
"Ni kweli nilimuona Nchimbi (Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa UVCCM) na nilitaka tu kumueleza kuhusu uamuzi wangu na si vinginevyo. Alinishauri tu na maamuzi ya kumuacha mke wangu yalibakia mikononi kwangu," alisema na kuongeza;
"... Alionyesha kiburi na ndio maana niliamua kuandika barua ile kwa Spika wa Bunge. Naamini kuwa siku si nyingi yote yataonekana na kwa sasa namuachia Mwenyezi Mungu."
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, aamekataa kuzungumzia jambo hilo akisema halihusiani na chama chake.
Makamba aliliambia gazeti hili kuwa, "usiniulize masuala ya watu, hilo ni suala la watu na kama unataka kuniuliza uliza kuhusu uchaguzi."
Katibu huyo alifafanua pia kuwa, yeye hawezi sasa kulijadili suala hilo, badala yake yuko radhi kujadili masuala ya uchaguzi.
Alipotakiwa kuelezea kuhusu utata wa azma ya Amina Chifupa kugombea nafasi ya Mwenyekiti UVCCM mwakani na kisha kupewa kauli ya kukataliwa, kauli iliyotoka kwa kiongozi mmoja wa juu wa UVCCM, Makamba pia hakutaka kuzungumza na akalitaka gazeti hili kumuuliza siku nyingine.
Katika hatua nyingine, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Amos Makalla, amewashangaa na kuwabeza wanachama wa umoja huo wanaofikiria kuwania uenyekiti wa umoja huo kwa sasa.
Akizungumza na Mwananchi jana, alisema yeyote anayefikiria kuwania nafasi hiyo kwa sasa si makini katika siasa.
Alisema umoja huo hauna taarifa za Chifupa kutaka kuwania uongozi katika umoja huo, lakini akasema hadhani kama mtu makini anaweza kujitokeza hivi sasa kuwania uongozi huo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.
"Mimi sijui kama Amina Chifupa anataka kugombea UVCCM. Lakini sidhani kama mtu makini anaweza kujitokeza hivi sasa," alisema Makala.
Chifupa alikaririwa na gazeti moja juzi akisema kwamba kuvunjika kwa ndoa yake kulitokana na nia yake ya kutaka kuwania uenyekiti wa umoja huo.
Mbunge huyo juzi alishindwa kutimiza ahadi yake ya kuzungumza na waandishi wa habari kumtaja Naibu Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne anayedaiwa kuvuruga ndoa yake.
Tovuti inaendelea kujengwa...