Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Na: Athumani Hamisi

HabariLeo

ALIYEKUWA mume wa Mbunge wa Viti Maalumu, Amina Chifupa (CCM), Mohammed Mpakanjia amesema kupeana kwao talaka isiwe sababu ya kumfanya mbunge huyo ajifiche na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya siasa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na HabariLeo Dar es Salaam jana, Mpakanjia alisema kupeana talaka ni jambo la kawaida katika maisha hivyo Amina awe huru kufanya shughuli zake za siasa.

Mpakanjia na Amina ambao wamedumu katika ndoa kwa miaka mitano na wana mtoto mmoja wa kiume wa miaka minne, walitalakiana Alhamisi iliyopita kwa sababu ambazo hazijabainishwa rasmi ingawa kuna madai yasiyothibitishwa kwamba ni saa chache baada ya Mpakanjia kudokezwa na Naibu Waziri mmoja madai juu ya mwenendo usiofaa wa mkewe.

"Anaweza kushindwa kufanya kazi zake nyingine na kujikuta anapoteza muda wake mwingi kujificha ama kutopatikana katika simu zake na sehemu muhimu anakotakiwa bila sababu za msingi," alisema Mpakanjia ambaye kwa sasa anauguza majeraha aliyoyapata katika ajali ya gari iliyotokea wiki iliyopita mkoani Morogoro. Alisema anajisikia vibaya kusoma katika magazeti kuwa Amina anajificha ama haonekani mitaani, kutokana na tukio hilo, jambo ambalo anadai limekuzwa kupita kiasi.

Alisema kuwa suala la mtalaka wake ni la kijamii na kuwataka watu waliolirukia, kuliacha na kumuacha Amina, awe huru katika kufanya kazi zake. "Nisingependa kuendelea kuzungumzia suala hili, napenda kulifunga rasmi na Amina awe huru kufanya mambo yake ya kisiasa.

Mpakanjia ambaye alifanya mahojiano na HabariLeo katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo, Dar es Salaam, alisema licha ya talaka bado ana ushirikiano mzuri na familia ya akina Chifupa akiwamo baba na babu yake.

"Niko hapa kumpokea babu yake Amina. Nimelazimika kuja licha ya kuwa naumwa kwa heshima na mapenzi makubwa ya familia. Ningekuwa na kinyongo nisingekuja," alisema. Wiki mbili zilizopita, Mpakanjia alijeruhiwa kwa kuungua sehemu kadhaa za mwili, baada ya gari lake kuwaka moto ghafla. Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser , liliteketea katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Mpakanjia, hakupenda kuzungumzia suala la kuwapo kwa barua aliyoiandika kwenda kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na kama alitaka lizungumziwe katika chama.

"Kama kutakuwa na suala la nidhamu kichama, litashughulikiwa kichama na vikao vyake. Tatizo ni dogo sana lisikuzwe na kuharibu ‘CV' ya Amina. Nataka awe huru na shughuli zake za kila siku," alisema. Pia hakupenda kuzungumzia zaidi suala la talaka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za ndoa ya Kiislamu ana nafasi ya kumrudia Amina endapo ametoa talaka moja.

Sheria ya ndoa ya Kiislamu, kuachwa kwa mke kwa talaka tatu ni ngumu kurudiana. Lakini mke huyo akiolewa na mume mwingine, kisha akaachika tena, mume wa kwanza anaweza kupeleka maombi yake tena na kumuoa upya. Lakini, endapo talaka moja itatolewa kwa mke na kuishi zaidi ya miezi, mwaka ama miaka bila kuolewa ama bila kupewa talaka nyingine mbili zilizosalia, inahesabika kuwa mwanamke huyo ameachika rasmi kisheria.

Kwa suala la matunzo ya watoto, sheria hiyo inamlazimisha mwanaume kumtunza mtoto/watoto. Ikiwezekana mke naye anastahili kutunzwa kama ana talaka moja ndani ya miezi kadhaa.

Katika moja ya vipengele vya kisheria, mume ataruhusiwa kuwachukua mtoto/watoto, endapo watatimiza miaka minane. Pia, haimzuii kuchukua mtoto/watoto kutoka kwa mwanamke, endapo itabainika kuwa hali ya mwanamke huyo kwa fedha ama maisha siyo nzuri.
 
Sasa haya ni makubwa tena. Kwa nini hasa wanamshikilia?

CCM waache siasa za kimafia. Zimepitwa na wakati.
 
interesting...
Naona huu mjadala umekuwa udaku, labda na thread ipelekwe huko.

Huu ni mwendelezo wa vituko vya 'mastaa' wa Bongo, hii inafanana na kisa cha msanii wa michezo ya Luninga aitwaye Sinta ambaye mwaka juzi alidanganya amekunywa sumu na kulazwa Muhimbili ili aandikwe/atangazwe na vyombo vya habari.
 
Kakalende, wakati Mbunge wa Bunge la Muungano anashikiliwa na watu pasipo ridhaa yake na kunyimwa uhuru wake wa kikatiba, hilo linapita Udaku! Wakati raia wa Tanzania anataka kutoa mawazo au maoni yake ambayo yanatishia maslahi ya watu wachache, na watu hao wachache wanatumia nafasi zao katika maisha ya mtu huyo ili kumnyamazisha, hilo linapita Udaku! Inapotokea kuwa serikali inakalia kimya kiongozi wa juu katika siasa kushikiliwa bila ridhaa yake na hadi mumewe (licha ya matatizo yao ya chumbani) anatokea na kuomba mtalikiwa wake ajitokeze hadharani hilo linapita udaku! Kama wanaweza kufanya hili (la kumnyamazisha Amina kulinda maslahi yao) kwa Mbunge wa Bunge la Muungano ambaye pia Mbunge wa Chama tawala, hivi unafikiri wanaweza kufanya nini kwa mtu wa kawaida ambaye anatishia maslahi yao? kama yanavyosema Maandiko "Kama wameweza kufanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu?".

Binafsi nimeshaachana na suala la chumbani la Amina na Zitto siku mbili zilizopita. Ninachopigia kelele ni hii tabia ya kuvumilia ukandamizaji kwa vile anayekandamizwa tunafikiri "anastahili" kwa vile tu "amekiuka maadili n.k". Hilo nalikataa na nitaendelea kulikataa!!

Free Amina Now!!! Free Amina Now!
 
Kwenye mjadala kuhusu wanaostahili kuitwa vigogo ndani ya CCM wapo wajuzi waliofikia hitimisho kuwa John Malecela ndio mtu mwenye sauti ya juu kabisa kwa sasa.Kwanza I doubt about that assertion,kwa vile yeye mwenyewe ni majeruhi wa mchezo mchafu wa wanamtandao.Uteuzi wa mgombea wa CCM katika awamu zote baada ya Mwalimu umethibitisha kuwa Malecela ni mtu wa kawaida tu.Anyway,hili sio mahala pake hapa.
Let's assume kuwa Malecela ndio the most powerful man in CCM.Yuko wapi wakati chama chake kinafanya mambo ya ajabu namna hii?Mtandao ni sawa na kundi la majambazi.Mgawanyiko wa mtandao unathibitisha hekima za wahenga kuwa "ushirika wa wachawi haudumu."Japo wapo wanao-doubt kuhusu taarifa zako Mzee Mwanakijiji kuwa AC amezuiliwa pasipo hiari yake,mie binafsi naamini kuwa hili linawezekana kabisa kwa kuzingatia historia za michezo michafu ndani ya chama hicho.Hata kabla ya mtandao sote tunafahamu yalowakumba marehemu Sokoine,Kolimba na hata wasio wana-CCM kama shujaa Katabalo.Hili dude linaloitwa CCM limejaa watu ambao wako radhi kutoa uhai wa mtu pale wanapoona maslahi yao yanahatarishwa.Na haiishii ndani ya CCM yenyewe bali hata kwenye organs zake (refer kilichomkumba Ipyana Malecela).

Pamoja na kuwa contradictory figure,sio siri kuwa AC alijijengea jina kubwa alipotangaza vita dhid ya wauza unga.Whether vita hiyo ilikuwa ya dhati (yafahamika kuwa Medi ni muuza unga sugu) au ilikuwa kujitafutia jina,ukweli unabaki kuwa she did what mtu kama Lowassa hajawahi kufanya hadharani.Wanasema ukiwa mchawi basi hata sauti ya adhana msikitini au kengele za kanisani zinaupeleka moyo mbio.Na ndivyo ilivyokuwa kwa mazungu ya unga yaliyoko ndani ya CCM au kwenye mtandao (taasisi isiyo rasmi ambayo imefanikiwa kutoa hifadhi salama kwa majambazi wa kisiasa na kiuchumi).Yalipomsikia AC anatangaza vita dhidi yao yakarejea kwenye vitabu vyao vya mbinu chafu dhidi ya wale wote wanaohatarisha ulaji wao.

Leo Mangula amemtaka Muungwana kukemea wanamtandao kwa vile wanahatarisha uhai wa chama hicho.Achana na porojo kuwa Malecela ndiye mwenye nguvu ndani ya CCM bcoz wenye nguvu ya kweli ni hao wenye fedha zao ndani ya mtandao,nguvu ambayo Malecela mwenyewe ni majeruhi wake.Muungwana hana jeuri ya kuwakemea wanamtandao kwa vile anafahamu fika kuwa pindi wakimgeuka atakuwa kwenye wakati mgumu sana kuendeleza utawala wake dhaifu.

AC ni kama Allan Johnstone wa BBC anayeshikiliwa huko Gaza,na kama ambavyo jumuiya ya wanahabari ulimwenguni inavyopiga kelele kutaka mwandishi huyo aachiwe,nami natamka kwa sauti kubwa "FREE AMINA NOW"
 
Hii Habari nzito
Kwa nyepesi nyepesi za haraka kuna watu wanadai bibie hakuwa na hiana tangu akiwa shule.
Maswali ya kujiuliza Mpakanjia alijua lini na why now?

labda alimpata kwa staili hiyo hiyo......hii inanikumbusha...easy come,easy go!
 
Kama kweli mh. Zitto kale uroda wa huyu bibie, it is a big shame to himself and to my party. Nampa pole na kumtakia uponyaji wa haraka ili asimame tuendelee kukijenga chama chetu. Sio kwamba kula uroda ni kitu kibaya; kibaya hapa ni kula uroda wa mke wa mtu. Mbaya zaidi mke mwenyewe ni Amina Chifupa ambaye maadili yake ni questionable for ages.

Ukishakuwa mwanasiasa unayeng'ara lazima uwe makini sana. Ujue kuna watu watafurahia mafanikio yako na kuna wengine hawatafurahia tu bali pia watakuchukia na kufanya kila hila ili kukumaliza kisiasa. Hii ni hasa katika nchi kama za kwetu ambazo bado zimekaa kikomunisti komunisti. Sasa Zitto hata kama kweli hajamla uroda huyu binti alipaswa kujua kuwa kuwa naye karibu kiurafiki ingempeleka pabaya. Ni rahisi wote wawili kukanusha, lakini the damage has been done and it should have been possible to prevent it.

Sasa kinachotakiwa hapa kama kweli kosa hili limetokea ni Zitto kukiri na kuomba msamaha kwa Bwana Mpakanjia, kwa mke wake na kwa CHADEMA. Then asimame tuendelee na mapambano. Hakuna njia nyingine ya uponyaji hapa zaidi ya yeye kukiri na kuomba msamaha hadharani!

Zitto amekuwa mtu wa madili kwa muda mrefu sana. Nitasikitika kama kweli atakuwa amefikia hatua ya kuporomoka kimaadili kwa muda mfupi namna hii tangu awe mbunge.

Nasubiri kusikia kwake.

mzee wa politic,....siasa zisiwe nyingi...aombe chama msamaha...kwani huyo ni mke wa chama[nimekuelewa maana yako,anyways!]

halafu ushasahau aliyowahi kuyasema ustaadh,maalim,alhaji,rais mstaafu,mzee wetu,ali hassan mwinyi....kuhusu ukimwi[ila alimaanisha ngono!]....huo mtego haubagui,cadre wangu!...unanasa wote...wenye akili,maadili,busara,uwezo,viongozi wa dini,wauza mkaa,na wengine wote unaoweza kuwataja!

issue ni je?hili suala ni lenye nia njema[kumnusuru mpakanjia aibu na kulinda hishima yake]au ni political plot for some backstage show...open minded i remain!
 
Hii Sasa Itawafanya Wenye Wake Wabunge Wawe Na Khofu, Pia Wale Ambao Wake Zao Watataka Wagombee Watakuwa Na Hali Ngumu Kulikubali hilo


sama alekhu!

leo hii yakhe!.....mbona hilo watu wana hofu nalo toka zamani....hasa jamaa zangu ambao hata kuwaacha wake zao kwenda sokoni...huwa...kaaazi kweli kweli!

we hata akenda afisini tu...waliwa!...labda asitoke nyumbani...nawe usitoke pia!...kaaazi kweli kweli!

kiufupi yakhe!kama chakula rizki...chalika...hata ukakilinda kwa jambiya!wasipokula watu watakula nzi,nyenyele,hata kunguru!

chakula kikiwa rizki yakhe......!
 
jamboonormal_amina6.jpg

sasa hiyo TV watagawana vipi?

hiyo picha alopiga nani?.....utafikiri[usipojua kama mwenye mke ni mpaka road]michuzi ndo mwenyewe....au ilikuwa ni mambo ya ku-balance vimo vya wahusika[bila kusahau miili!]
 
NA JINA LA UNGUJA LINATOKANA NA UNGO JAAA, INAMAANISHA NI KISIWA CHENYE NEEEMA.

unajua usukumani[wasukuma si unawajua weye!]kuna kijiji kinaitwa LUNGUYA....naambiwa maana yake ni unguja!

hivi watu wa unguja...si wenye asili ya bara hasa....wakina makungu and co. sasa,nikisema hawa ndio walokuja na jina la unguja ntakuwa nimezusha au nimeibua mada?

uta'nsamehe ustaadh!...kina neema kweli....kama usukumani![ng'ombe,dhahabu,mchele,mabinti,na kila utakachoweza kukitaja!]ila wanachuma wengine!....wana'haramu!
 
Kwako Zitto, sijui ni lini ulikuja Dar, kama ulikuja kimasomo (hukuwa mkazi) basi una mengi ya kujifunza mdogo wangu. Kama kweli umelala naye siwezi kushangaa sana. Ila .... kwa kumchukua mke wa mtu hapo ulikosea. Ma miss wooote wale mzee?!? njoo jijini tukupe vimwana. Ningekushauri ukae kimya wala usijibu hizi tuhuma si kwenye magazeti wala sio humu!FD


mzee fd,

na asiyefanya mambo haya awe wa kwanza kurusha jiwe!...

alofanya mhishimiwa si la ajabu wala la kuongewa hivi[ukizingatia jamii hii ni ya kiafrika halafu mbaya zaidi ya kiswahili]....tatizo ni kuwa limetoka hadharani....wangapi wametembea na wake za watu[sisemi yeye kafanya hivyo,sijabaini bado]na wakafikia kuhalalisha kwa kuoana?.....this is a common sin!..commited everyday with people of all walks of life!
 
Kwa kweli nimegundua tunapenda sana udaku, pamoja na kuchokoza kwa kuonyesha jinsi mapesa yetu yanavyoliwa na wajanja serikalini,mzalendo mmoja anasisitiza tuendelee na Mjadala wa vijana wetu, hoja akiicement kwa kusema kwamba , naomba kunukuu"maana ni lazima tujue kesho na kesho kutwa, tutawapaje hawa wabunge wa wawili madaraka ya kuamua mambo muhimu ya taifa letu, wakati tayari tunajua kuwa ni wadhaifu, kwa mfano Tanzania tumeamua kumpa ac au Zeeee madaraka ya kutuamulia kama taifa kama tujiunge na EAC au tusijiunge nayo, sasa ni wazi kabisaa kuwa kama Kenya wanaitaka zaidi EAC, watampa ac mwanaume ili aamue kwa kuwapendelea, au kama ni Zeee watampa kimwana aaamue kwa upendeleo wa nchi hiyo, huku sisi tukiumia" mwisho wa kunukuu ! Sijui ni maadili yepi ndugu yangu anayoyazungumzia! usipime ndugu yangu si tumeyaona! Mbona watu wana hayo madaraka unayoyazungumzia wewe na wanafanya mambo ya ajabu, kuzidi hata hayo yaliyofanywa na vijana(kama ni kweli).Sana sana nchi hii ukionekana mwingi ndio hata wapiga kura wanakufagilia. Ingekwa uadilifu unaouzungumzia wewe ni kigezo cha kutokupata uongozi kwa jinsi bwana shigongo na magazeti yake ya udaku alivyomshambulia mheshimiwa fulani akiwa katika mbio wa kuwania ubunge,hakika asingeupata ubunge ! Tusingekuwa hata na .....Sababu wengi hata wewe unajua maadili unayoyazungumzia wewe pale hakuna hata kidogo. Sio kwamba natetea uovu,kama mzalendo toka unyaluni natamani sana Tanzania ingekuja kuwa na viongozi wa aina unayoisema wewe, sana tu, ila kwa sasa ni alinacha, si tuko nao, tunaishi nao, tunawaona!

Maadili yaliyo muhimu kwa mtanzania mlala hoi kwa sasa ni kuwa na viongozi safi , ambao kuomba ama kupokea kwa rushwa ni mwiko, ambao kuingia mikataba mibovu ya madini kwa kupewa $ 200,000 ni mwiko, ambao wanaacha taratibu za procurement kuchukua mkondo wake na sio kutumia mabavu ili mtoto wa mjomba apate, mtoto wa mjomba mwenyewe haa uzoefu wa kazi, pesa zinaingia shimoni, ambao badala ya kuongeza magari ya kifahari angetumia pesa husika kujenga madarasa na sio kuwalazimisha kila kukicha wananchi masikini kuchangia mashule , zahanati ets...tunatakiwa kuwaonyesha watawala wetu kwamba wenye nchi ndio wenye nguvu na kwamba wanaweza kuhojiwa na kuwajibishwa kwa kila senti inayotokana ama na kodi,rasilimali zetu na mikopo ya nje(zalio la umasikini).

Tujadili issues, kama wazee wetu mnavyoyakamua manyuzi kila siku, maadili unayoyazungumza tuanze kuyatengeneza kwa wanetu,Mnyalu junior (The President to be)nimeshaanza nae, sisi tumeshachemsha!Hata wewe unajua!

Mambo ya akina AC na Nchimbi ni siasa za CCM , yote hayo ni mapambano katika kuelekea uchaguzi wa viongozi wa UVCCM...Jamani, tushapotea. Wanamalizana kwa kalamu, kama kawaida yao!Wasituingize mkenge na sisi!


.....................................................................................................


Mandugu na huyu Padri kulikoni? ndio yale yale ninayoyazungumza, kama huyu mchungaji anakananga mpaka kukaua kamwanakondoo sembuse hao unaowazungumzia! Hawa ndio watanzania,si unaona kanisa limemkingia kufua? Mambo hayo!


Haya Mandugu, Mnyalu nawapa 5 , tukaze buti tutafika!
 
FIKIRADUNI WROTE:


jamboonormal_amina5.jpg


Huyo mumewe hana wivu angekuwa na wivu angemuachia TAJIRI MTOTO amchekelee mkewe namna hiyo? Hivi huyu Mumewe ni wawapi? maana sidhani kama ni wa Pwani huyu.

kaka...huyo ni wa pwani....ila pwani ya kimjini mjini....pwani ya kwetu lamu...hicho kitendo cha,tajiri nani vile? kingemfanya bibie kukaa ndani bila kutoka na kuonana na wageni wa kiume....tamaa unaizuia mbaali kabisa...usiilete karibu!
 
mswahili
JF Senior Expert Member Join Date: Wed Sep 2006
Posts: 427
Rep Power: 21




--------------------------------------------------------------------------------

Heshima zetu wakuu.

Suala la Amina na Zitto halikuwa na kificho ndani ya bunge. kwa mshangao mkubwa Phillimon mikael ambaye ni mtu tuliyekuwa tunamtegea ameamua kumtetea ZITTO kwa vile ni mfuasi wake.

phillimon mikael huoni aibu kumtetea mtu anayekula mke wa mtu mchana wazi?
ina maana mkiingia madarakani wake zetu itakuwa chakula chenu? kama Zitto kaweza kuchukua mke wa mtu atashindwa vipi kuchukua rushwa na kutuingiza kwenye kashfa za Rada? sifa za kiongozi ni kuaminika kwa watu wake na kuwa na sifa njema kwa wananchi, kwa hali hii mtu ukiwa na mkeo wakati wa kampeni usimruhusu aende kwenye kampeni za Chadema.

Mwanakijiji.

Unazidi kujishusha hadhi yako kwa kutetea ujinga yaani unapinga Zitto hajafanya kosa anasingiziwa tu. Phillimon Mikael hajakanusha na anashabikia jambo hilo. Zitto mwenyewe anakubali kuwa yuko karibu na Chifupa kwa vile mtu makini na anafaa kufanya nae kazi. wewe unabisha tu kwa vile aliyefanya ni Chadema. wewe na Phillimon nani chadema zaidi? wewe na Mwanasiasa nani anaijua chadema zaidi? Mwanakijiji kuwa Neutral mke wa mtu anachukuliwa wewe unasema sio issue? jee issue ni kuandika barua kwa Rais JK kisa Tanzania Daima limepewa onyo.

WANABODI.

Huyu ZITTO KABWE ajiuzulu na hafai uongozi labda aongoze wanaume tu.
last week CEO wa BP Lord Browne amejiuzulu kutokana na kashfa hizo hizo za KI ZITTO.

Waziri wa Mambo ya ndani wa U.K David BLUNKETT alilazimika kujiuzulu kwa kujaribu kumsaidia kupata visa mtumishi wa kimada wake ambaye hakuwa mke wa mtu. leo ZITTO kavunja ndoa ya Mpakanjia lakini Phillimon na Mwanakijiji wanafagilia tu.

kama mnafuata sheria za western world wenzenu wamejiuzulu. haya ya kukaa na wake za watu kwa uaminifu yameshinda mnataka tuwape nchi?

ustaadh....za siku kadhaa!

yaani hii.....ni typical mswahili talk!....ushasahau unaishi nyumbani kwa watu....tamaduni yao tafauti na ya kwetu....au?
 
Mzee Mwanakijiji uliye ughaibuni. Amina yuko kwao Mikocheni! Infact nasikia kisaikolojia hali yake haitangengamaa...hasa ukizingatia kwamba alikuwa amepania sana kushusha nondo kwenye press conference wakamweka plasta mdomoni.

Naafikiana na wewe kwa kukubali kufunga mjadala wa ngono!hauna tija!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom