Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 1,211
- 233
Kichuguu, inasikitisha watu wanafikiri tunazungumzia mambo ya ngono hapa. Tunachozungumzia ni jambo zito sana. Mbunge wa Jamhuri ya Muungano anataka kuzungumza na waandishi akikimbilia haki yake ya kutoa maoni na mawazo ili kusema alichonacho halafu analazimishwa na watu wachache na kunyang'anywa simu, na kila analofanya kuwa na watu wanaomuangalia. Dereva wake amebakia kushangaa kwani hawezi kumsikiliza bosi wake na kwenda naye anakotaka kwenda... Kulifumbia macho jambo hili ni ukosefu mkubwa wa maadili kwa kuruhusu ukandamizaji mbele ya macho yetu!!
Je, hebu jiulizeni hivi Amina atapata nafasi yoyote tena ya kusimama hadharani na kusema lolote kwa uhuru wake? Je akitokea na kusema "nimebadili mawazo" huku kazungukwa na wanafamilia, mtaamini maneno yake? Je kuanzia sasa atakuwa huru tena kwenda mahali popote, kukutana na mtu yeyote, na wakati wowote bila kuwa na mtu wa karibu "kumsimamia"? Je Amina anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari akitaka kuzungumzia mambo mengine ya kijamii bila kufanya "wakubwa" waumwematumbo?
Kuna njia mbili kubwa za kumnyamazisha na ya kwanza imeshaanza kuwekewa msingi:
a. Madai ya kuwa ni mgonjwa wa kiakili/saikokojia.
Kumbukeni kuwa kwa mujibu wa sheria zetu "akili timamu" ni mojawapo ya sifa zinazomwezesha mtu kuwa Mbunge. Je, Amina bado ana "akili timamu"?
b. Ya pili ni kumrudisha kwa mumewe.
c. La tatu nitawaacha mlifikirie....
FAN FAN FAN
Mwanakijiji!
Umeongelea sana kuhusu hili Lakini nafikiri ktk swala la kushikwa kwa Mh.Amina ili asiongee na vyombo vya Habari au kuwasiliana na watu wowote wa kulaumiwa ni Mh.Amina mwenyewe kama alikuwa na la kusema lenye nia ya kuanika ukweli hivi alishindwa kupanga mikakati ya kufikisha ujumbe alionao bila ya kulitangaza kwamba ninataka kulipua bomu na badala yake kuitisha mkutano na kufika na kutoa hilo bomu alilonalo na wananchi ndiyo wangeamua ni bomu au ni mfano wa bomu.
Unajua mimi binafsi kulikuwa na ishu dhidi ya serikali ambayo nilipigwa nayo vita sana na ilikuwa miaka ya tisini na tano na nilienda studio za DTV na ITV na kuomba kuonana na wahusika pamoja na kuzuiwa Lakini nilifanikiwa kuonana na wahusika na baada ya kunisikiliza kweli waliona ni bomu na waliniambia upo tayari kuweza kulizungumzuia hili tukupe muda kwenye Taarifa ya habari inayotizamwa na watu wengi DTV ilikuwa ya saa moja na ITV ilikuwa ni ya saa mbili ,niliambiwa niongee kwa haraka ili niweze kufikisha ujumbe kwa dk 3 ni chache na niliweza kufanya hivyo na ujumbe ulifika na kile kilichochukua mwaka na zaidi bila ya kutimizwa kiliweza kutekelezwa na serikali kwa muda wa wiki tu.Kwani niliweka kila kitu bayana na kuwachambua wahusika wote na mapungufu yao kwa muda niliopewa na watu walianza kutavutana wenyewe.
Ninachotaka kusema Mh. Mbunge Amina hakutulia ktk hili na ndiyo maana anashikiliwa na wale wanaompenda,Nyinyi mnafikiri mnampenda Lakini hamuelewi ukweli ya yale yanayomsibu au ya yale ambayo yangemsibu Mzazi wake ndiye anyejua yale ambayo yangemkuta kwa yale anayoyafahamu yeye kutokana na habari alizozipata.Mzee Ametumia busara na Nyinyi mnashabikia na FREE AMINA Kwasababu hakuna anayejua kwa undani yanayomsibu huyo Mh.Amina kwasasa na Ambayo yangemsibu baada ya kuwaweka sawa wapinzani wake kwamba anataka kulipua bomu.
Kosa amelifanya yeye kwahiyo msiwalaumu wale ambao wanajaribu kumuepusha na Hatari kwa mapenzi waliyonayo.Hulka ya wanadamu waliowengi ni Ubinafsi, Mnachoshabikia nyinyi ni kutaka kusikia kile Mh.Amina alichotaka kukitoa hadharani na ndiyo kelele zote za FREE AMINA,Lakini wale wenye Mapenzi ya kweli na wenye uchungu na wanaomthamini Na watakaoathirika zaidi na matokeo ya maamuzi ya Mh Amina na Wanaolijua litakalomfika Mh.Amina endapo ataendelea kupayuka kwasasa ndiyo wanaoguswa zaidi na hiyo hatua waliyoichukua ndiyo wao wanaona ni muafaka kwasasa.Nani Kama Mzazi au Wazazi.?
Tusiyafanye ya wenzetu kuwa rahisi,tuangalie na athari za yale yanayowakuta au yatakayowakuta wenzetu kutokana na matendo wanayokusudia kuyafanya au waliyoyafanya au watakayofanyiwa au waliyofanyiwa.Fikra kila mmoja na zake Lakini wachache wenye kujaliwa BUSARA.