Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Kichuguu, inasikitisha watu wanafikiri tunazungumzia mambo ya ngono hapa. Tunachozungumzia ni jambo zito sana. Mbunge wa Jamhuri ya Muungano anataka kuzungumza na waandishi akikimbilia haki yake ya kutoa maoni na mawazo ili kusema alichonacho halafu analazimishwa na watu wachache na kunyang'anywa simu, na kila analofanya kuwa na watu wanaomuangalia. Dereva wake amebakia kushangaa kwani hawezi kumsikiliza bosi wake na kwenda naye anakotaka kwenda... Kulifumbia macho jambo hili ni ukosefu mkubwa wa maadili kwa kuruhusu ukandamizaji mbele ya macho yetu!!

Je, hebu jiulizeni hivi Amina atapata nafasi yoyote tena ya kusimama hadharani na kusema lolote kwa uhuru wake? Je akitokea na kusema "nimebadili mawazo" huku kazungukwa na wanafamilia, mtaamini maneno yake? Je kuanzia sasa atakuwa huru tena kwenda mahali popote, kukutana na mtu yeyote, na wakati wowote bila kuwa na mtu wa karibu "kumsimamia"? Je Amina anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari akitaka kuzungumzia mambo mengine ya kijamii bila kufanya "wakubwa" waumwematumbo?

Kuna njia mbili kubwa za kumnyamazisha na ya kwanza imeshaanza kuwekewa msingi:

a. Madai ya kuwa ni mgonjwa wa kiakili/saikokojia.
Kumbukeni kuwa kwa mujibu wa sheria zetu "akili timamu" ni mojawapo ya sifa zinazomwezesha mtu kuwa Mbunge. Je, Amina bado ana "akili timamu"?

b. Ya pili ni kumrudisha kwa mumewe.

c. La tatu nitawaacha mlifikirie....

FAN FAN FAN


Mwanakijiji!

Umeongelea sana kuhusu hili Lakini nafikiri ktk swala la kushikwa kwa Mh.Amina ili asiongee na vyombo vya Habari au kuwasiliana na watu wowote wa kulaumiwa ni Mh.Amina mwenyewe kama alikuwa na la kusema lenye nia ya kuanika ukweli hivi alishindwa kupanga mikakati ya kufikisha ujumbe alionao bila ya kulitangaza kwamba ninataka kulipua bomu na badala yake kuitisha mkutano na kufika na kutoa hilo bomu alilonalo na wananchi ndiyo wangeamua ni bomu au ni mfano wa bomu.

Unajua mimi binafsi kulikuwa na ishu dhidi ya serikali ambayo nilipigwa nayo vita sana na ilikuwa miaka ya tisini na tano na nilienda studio za DTV na ITV na kuomba kuonana na wahusika pamoja na kuzuiwa Lakini nilifanikiwa kuonana na wahusika na baada ya kunisikiliza kweli waliona ni bomu na waliniambia upo tayari kuweza kulizungumzuia hili tukupe muda kwenye Taarifa ya habari inayotizamwa na watu wengi DTV ilikuwa ya saa moja na ITV ilikuwa ni ya saa mbili ,niliambiwa niongee kwa haraka ili niweze kufikisha ujumbe kwa dk 3 ni chache na niliweza kufanya hivyo na ujumbe ulifika na kile kilichochukua mwaka na zaidi bila ya kutimizwa kiliweza kutekelezwa na serikali kwa muda wa wiki tu.Kwani niliweka kila kitu bayana na kuwachambua wahusika wote na mapungufu yao kwa muda niliopewa na watu walianza kutavutana wenyewe.

Ninachotaka kusema Mh. Mbunge Amina hakutulia ktk hili na ndiyo maana anashikiliwa na wale wanaompenda,Nyinyi mnafikiri mnampenda Lakini hamuelewi ukweli ya yale yanayomsibu au ya yale ambayo yangemsibu Mzazi wake ndiye anyejua yale ambayo yangemkuta kwa yale anayoyafahamu yeye kutokana na habari alizozipata.Mzee Ametumia busara na Nyinyi mnashabikia na FREE AMINA Kwasababu hakuna anayejua kwa undani yanayomsibu huyo Mh.Amina kwasasa na Ambayo yangemsibu baada ya kuwaweka sawa wapinzani wake kwamba anataka kulipua bomu.

Kosa amelifanya yeye kwahiyo msiwalaumu wale ambao wanajaribu kumuepusha na Hatari kwa mapenzi waliyonayo.Hulka ya wanadamu waliowengi ni Ubinafsi, Mnachoshabikia nyinyi ni kutaka kusikia kile Mh.Amina alichotaka kukitoa hadharani na ndiyo kelele zote za FREE AMINA,Lakini wale wenye Mapenzi ya kweli na wenye uchungu na wanaomthamini Na watakaoathirika zaidi na matokeo ya maamuzi ya Mh Amina na Wanaolijua litakalomfika Mh.Amina endapo ataendelea kupayuka kwasasa ndiyo wanaoguswa zaidi na hiyo hatua waliyoichukua ndiyo wao wanaona ni muafaka kwasasa.Nani Kama Mzazi au Wazazi.?

Tusiyafanye ya wenzetu kuwa rahisi,tuangalie na athari za yale yanayowakuta au yatakayowakuta wenzetu kutokana na matendo wanayokusudia kuyafanya au waliyoyafanya au watakayofanyiwa au waliyofanyiwa.Fikra kila mmoja na zake Lakini wachache wenye kujaliwa BUSARA.
 
Chadema wafadhaishwa na sakata la Kabwe, Amina

*Baadhi wahofia siri za chama hicho kuvujia CCM
*Wapo waliosubiri kitoe tamko kuhusiana na hilo


Na Waandishi Wetu

BAADHI ya viongozi, makada na washabiki wa CHADEMA wameelezea kufadhaishwa na madai dhidi ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mtu hadi kuvunja ndoa yake.

Wamesema uhusiano wake na Mbunge wa Viti Maalumu (Vijana) kupitia Bibi Amina Chifupa (CCM), umekiweka njia panda chama hicho.
Wakizungumza kwa wnyakati tofauti na gazeti hili jana Dar es Salaam, wengi walieleza kuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya mambo muhimu yanayohusu CHADEMA pamoja na mikakati yake yatakuwa yamevujishwa kwa CCM kupitia kwa Bi. Chifupa.

Baadhi yao walielezea wasiwasi mkubwa kwamba huenda chanzo cha uhusiano huo kilikuwa ni mpango wa CCM kumtumia Bi. Chifupa kumshawishi Bw. Kabwe kuhamia CCM.

Bw. Kabwe amekuwa mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani ambaye amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu na CCM kuhamia chama hicho.

Wengine walielezea kusikitishwa kwao na Bw. Kabwe ambaye amewaangusha kwa kiasi kikubwa baada ya wanachama na mashabiki wa CHADEMA kuweka matumaini makubwa kwa mbunge huyo, kwamba ni kiongozi makini na mwadilifu.

"Siku zote tumekuwa tukijua kwamba kuna ufuska wakati wa vikao vya Bunge. Lakini sikuwahi kufikiria kabisa, kwamba Bw. Kabwe angekuwa mmoja kati ya watu wanaofanya vitendo hivyo. Kwa kweli ametuangusha sana," alikaririwa Bw. Pendael Macha ambaye lijitambulisha kuwa mmoja wa washabiki wa CHADEMA aliyekutwa akisubiri basi eneo la Mchikichini, Ilala.

Baadhi yao walielezea kusikitishwa kwao na kitendo cha mbunge huyo kujitetea kwa kusema kwamba atavifikisha mahakamani vyombo vya habari au watu wanaoingilia maisha yake binafsi.

"Mimi sijawahi kusikia kiongozi wa umma ana maisha binafsi. Wewe ukiwa mbunge, basi kila unalofanya linatazamwa kwa kina na linaongelewa na jamii. Cha msingi hapa ni kwa mwenzetu huyu kuja na kusema ukweli wake wa ndani na kama ni kuomba radhi, kwa familia ya Mpakanjia, kwa wana CHADEMA na umma kwa ujumla, basi tutamsikiliza," aliongeza.

Hata hivyo, wengine walilihusisha sakata hilo zima na siasa chafu zinazoendelea kuhusu nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Taifa wa CCM ambapo inasemekana Bi. Chifupa alionesha nia ya kugombea mwakani.

Hata hivyo, wengine walibainisha kwamba suala la msingi ni maadili binafsi ya wabunge hawa vijana wawili. "Hapa suala si siasa. Kama Amina angeheshimu ndoa yake na kama Zitto angemheshimu Amina kama mke wa mtu, yote haya yasingetokea".

Baadhi ya wananchi waliohojiwa, walishangazwa na ukimya wa CHADEMA katika suala hili, wakieleza kwamba CHADEMA ni chama ambacho hutoa matamko ya haraka haraka, mara linapotokea jambo lenye mjadala katika jamii.

Walisema hii ni dalili, kwamba mambo si shwari ndani ya chama hicho baada ya Bw. Kabwe kuwaweka njia panda wenzake na kuamua kukimbilia Kigoma, badala ya kubaki Dar es Salaam na kutafuta namna ya kukabiliana nalo.

Baadhi yao waliohojiwa kwa masharti ya kutotajwa majina, walitilia shaka zaidi kwamba huenda Bw. Kabwe alikuwa akivujisha siri za CHADEMA kwa Bi. Chifupa ambaye yeye na baba yake ni makada wa CCM.

"Kama kulikuwa na kupeana habari katika uhusiano huu, basi wenzetu wa CCM watakuwa ndio walionufaika. Kabwe ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na ni mtu aliye karibu sana na uongozi wa juu wa CHADEMA na anayejua mambo mengi sana ya chama chetu.

"Kwa upande wa Amina, yeye si kiongozi wa juu ndani ya chama na wala si mjumbe wa vikao vyovyote nyeti vya CCM," alisikitika kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye hakutaja jina lake litajwe kwa madai kwamba si msemaji wa chama.

Source: Majira, Ijumaa Mei 11, 2007; http://www.majira.co.tz/kurasa.php?s...bariNamba=2869

Mnyika,

Wewe ndiye Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA sasa hivi. Vipi CHADEMA hakina tamko lolote juu ya aibu hii? Hawa jamaa wamesema kweli kwamba always CHADEMA inatoa matamko chapchap kukiwa na jambo, mbona mmekaa kimya kwenye hili? Je, ni kweli mna wasiwasi kwamba Zitto alikuwa anavujisha siri za Chama?
 
YES, FREE AMINA NOW!
Hili suala sio la kifamilia tena, Mtu akishakuwa kiongozi katika jamii sio `pension` ya mzazi tena katika mambo yanayoigusa jamii. Hapa kuna jambo limeshatajwa sana. KWAMBA KUNA NAIBU WAZIRI ANAYECHOCHEA KUVUNJA NDOA ZA WENGINE(tena waheshimiwa wenzake). Hatutaki kuwa na Mawaziri wa aina hiyo hatari hata kidogo,na jee tutajuaje kama sio kwa kuwaachia wahusika waseme? MWACHENI HURU AMINA ASEME ili maswali yote yapate majibu,na Watu wa majungu na mbinu chafu wafahamike wazi.
 
Zitto Kabwe!!!!!!!! Ebwana Aminia askari wangu! kanyaga twende!hapo upo vitani ila vaa kombani! Aminiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sio kila anachosema Mzee Mwanakijiji ni gospel. Hakuna mwenye authority na accuracy ya information za Amina zaidi ya Mzee Chifupa (na Zitto labda). Kama Amina hapatikani kwa simu, Mzee Mwanakijiji kajuaje kwamba kashikiliwa kinyume cha matakwa yake na kwamba amechanganyikiwa.

LOL... wewe ukijua hili, wenzio wanajua lile...
 
Mnyika,

Wewe ndiye Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA sasa hivi. Vipi CHADEMA hakina tamko lolote juu ya aibu hii? Hawa jamaa wamesema kweli kwamba always CHADEMA inatoa matamko chapchap kukiwa na jambo, mbona mmekaa kimya kwenye hili? Je, ni kweli mna wasiwasi kwamba Zitto alikuwa anavujisha siri za Chama?


Mtego mzuri huo mugongo...
 
Amina should be free now. she dont deserve these.

Inanipa wasiwasi kama mtanzania anaweza kufanyiwa jambo hili kwa kweli Mbowe kaa chonjo kwani naona wewe waweza kuwa wa pili ili kukunyamazisha kwenye jambo hili.
 
Hizi ndio siasa chafu, ukiisoma kwa makini habari ya gazeti hilo hapo juu, bila shaka siasa chafu inatawala kuliko ukweli wenyewe.
 
nnaleta tena ombi langu, jina libadilishwe ili kujenga hoja za kimantiki, si kutoka bungeni, au tunakubalu kuwa suala hili limetokea bungeni?
 
Sio kila anachosema Mzee Mwanakijiji ni gospel. Hakuna mwenye authority na accuracy ya information za Amina zaidi ya Mzee Chifupa (na Zitto labda). Kama Amina hapatikani kwa simu, Mzee Mwanakijiji kajuaje kwamba kashikiliwa kinyume cha matakwa yake na kwamba amechanganyikiwa.

Mzee Chifupa katuambia pale Maelezo kwamba Amina ndio pensheni yake kwahiyo hawezi kumruhusu kuropoka mambo na lazima am-guide na kwamba jambo hili watalimaliza kifamilia. Kwahiyo Mzee Chifupa ni mwehu kuhatarisha maisha ya mwanae?

In any case, I am impressed by your devotion to this issue to a point of spending time kwenye photoshop kutengeneza fulana. Duh, kweli kuna watu wana mapenzi na nchi!

You are wrong.Mzee Chifupa alisema yeye mwenyewe HAJUI mwanae alipo.Hivi unaweza kuwa accurate kama hujui kitu?So,count Mzee Chifupa out.By the way,kama huyo Mzee angekuwa na authority unayotaka tuamini angemdhibiti mwanae atulie kwenye ndoa.Au what kind of authority are you talking about.

Pengine ni kweli kwamba sio kila anachosema Mwanakijiji ni gospel,lakini mara nyingi nashawishika kuamini hoja zake kwa kigezo kimoja kikuu:anajua kutafuta habari,na uthibitisho unapatikana ukisikiliza podomatic yake.Pengine kabla ya kumpinga ungejaribu kumuuliza amejuaje kuwa Amina kashikiliwa.

Naamini hata wewe ungekuwa public figure kama Amina then majambazi flani wakakushikilia basi Mwanakijiji angeanzisha kampeni ya FREE MUGONGOMUGONGO NOW and would possibly spend his time kwenye photoshop kutengeneza flana zenye ujumbe huo.The guy deserves our compliments.
 
Asalam aleykum,

Ebana hii scandal ya hawa waheshimiwa inanitatiza sana maana inaonekana ni mambo ya kisiasa sana na hakuna vidhibitisho vya kutosha. Mi namuomba bwana mpakanjia asikubali kupelekeshwa na baadhi ya watu ambao wanajaribu kumtumia wakijua kabisa udhaifu wake uko wapi, angekuwa mtu wa busara angemsikiliza sana mkewe kuliko watu wa pembeni na angefanya utafiti kuhusu mambo yake binafsi na mkewe na kutafuta msaada wa kifamilia kuliko kulipeleka sula lake la ndoa bungeni hii inaonekana kabisa kuna watu wanaomshauri vibaya mzee mpakanjia pasipo yeye mwenyewe kujua na labda kwa sababu ya elimu ndogo aliyokuwa nayo hawezi kupima yote hayo. Napenda kumwambia mzee mpakanjia kabla ya kufanya maamuzi yoyote ni vyema aangalie nini madhara yake baadae , nampa pole Amina namtakia uvimilivu ila mzee mpakanjia awe makini maana kuna wenzetu wazungu wanasema: U CAN ONLY PUSH A GIRL AWAY FOR SO LONG/ UNTIL SHE WALKS OUT OF YOUR LIFE ON HER OWN/ SO BE CAREFUL AND MAKE SURE THIS IS WHAT U WANT/ 'COS ONCE SHE TURNS AROUND, SHE ISN'T COMING BACK... NIMEMALIZA.
 
Alichokifanya Nchimbi leo katika kujaribu kugeuza kibao cha mjadala wa Amina-Zitto ni kitu ambacho kinaonesha yeye ni mtu wa aina gani... !! Nimeamini kuwa "he'll do anything" kulinda mkate wake, hata hivyo... shoka limeshainuliwa!!!
 
Alichokifanya Nchimbi leo katika kujaribu kugeuza kibao cha mjadala wa Amina-Zitto ni kitu ambacho kinaonesha yeye ni mtu wa aina gani... !! Nimeamini kuwa "he'll do anything" kulinda mkate wake, hata hivyo... shoka limeshainuliwa!!!

Aisee mbona unaongea kimafumbo? Kada kafanya nini tena leo, mbona wadau hatujainasa hiyo?
 
Alichokifanya Nchimbi leo katika kujaribu kugeuza kibao cha mjadala wa Amina-Zitto ni kitu ambacho kinaonesha yeye ni mtu wa aina gani... !! Nimeamini kuwa "he'll do anything" kulinda mkate wake, hata hivyo... shoka limeshainuliwa!!!


Kafanya nini tena jamaa yule DOKITA mikupuo
 
Alichokifanya Nchimbi leo katika kujaribu kugeuza kibao cha mjadala wa Amina-Zitto ni kitu ambacho kinaonesha yeye ni mtu wa aina gani... !! Nimeamini kuwa "he'll do anything" kulinda mkate wake, hata hivyo... shoka limeshainuliwa!!!


MKJJ: umezidi mafumbo mshikaji! hebu weka mambo sawa, wengine hatukusoma Ngugi wa Thiongo!
 
mzee makompyuta.. maneno mazito hayo.. ila ndani yake yamejaa kila chembe ya hekima.
 
hili la sasa naogopa hata kusema (na mimi si mwoga hivyo...)... Mwe Majira haya ni ya kiangazi huku kijijini, na joto limezidi..!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom