Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Ndo maana mie saa zingine huwa naeda kule chumbani kwa MWANAKIJIJI tuu maana kule mambo kidogo yako tofauti
 
Well hata mimi sikuwa nimemtukana ila nimesema ukweli lakini kazuka na ya kuzuka nayo . katukana wengi kisa katajwa Malecela.Muda wa kutishana hakuna Tanzania ni yetu sote .Nasema I a ready to face you popote uwe ughaibuni ama nyumbani . More to come si unajifanya unajua ? kaa mkao wa kusikia umma watajua mengi .Nitakuvua nguo ubaki uchi hadi uwe unaongelea issue badalaya kua attack personalities akitajwa Malecela. Back you spent time ukimtukana Mwalimu (RIP) hadi kusema kafa na ukimwi . Kila siku unamtukana Mzee Mkapa , umesha mtukana sana Mzee RO bado hujakamatwa wala kutishiwa na he knows all maana anasoma hapa leo kusema Malecela unakuja juu na uongo na matusi ? Twende sasa tuone . Stay tuned
 
watu tungezingatia mambo ya "hoja hujibiwa kwa hoja" hata kama hoja hizo ni za kipuuzi tungefika mbali. Anytime, unapovuka mpaka wa hoja na kuingia kwenye mambo binafsi, unajiruhusu kuingia kwenye tetesi, udaku, wivu, husuda, uzandiki, na visasi.
 
Huwa mara zote ana nia ya kuua hoja zinazo mgusa yeye na Malecela lakini lazima ajue kaa alitueleza we Tanzanians we can go to helll hatutamuacha aende hivi hivi. Mzee baada ya umakamu atasahaulika kama Msuya .
 
Aaaah kule chumbani kwa Mwanakijiji mi nimewaomba ufunguo weee lakini naona wameamua kunichunia tu. Basi bwana faidini nyinyi wenyewe.......
 
I wish this was made much clearer.

(a) Majira ni spinning machine; OK, nitaiondoa kwenye boomarks zangu. Kwana huwa wanachelewa ku-update news kwa karibu wiki nzima. Kwa nini ichukuliwe na Manji? Ili aweze kupambana na Mengi?

(b) hii sehemu ya pili niyo sikupata
Kuna mtu anaweza kufafanua? Ni kama ninakosa conection mahala fulani hapa.

(i) Alikuwa akifanya mwanzoni na wenzake: akina nani? JK dhidi ya SAS
(ii) Mwanadada aliendelea kuvuma pamoja na kumwaga sumu: ipi, "list ya madawa ya kulevya?" au hii ya "kugawa free samples"
(iii) Kutumia hiyo nyuklia: ipi hii ya juzi ya AC Vs ZK? Kuna taarifa kuwa wabunge wengi wametafuna huyu binti, kwa hiyo ni kwamba EC alitafuta nafasi ya kumwaibisha AC kwa kutumia mbunge wa nje ya CCM? na hivyo kuhoji uwezo wake kiuongozi kuficha SIRI? Kwanza: Siri ni ninini na siri kwa nini na ni kwa nini ni siri.
(iv) Imeanza kumrudi: Hapa ndipo sielewi kabisa. Inaanza kumrudi nani AC, EC au ZK. Na inamrudi vipi?


MKJJ na Tanzanianjema

Tahafadhalini jamani na mimi pia nasubiri majibu ya hili.
 
Huwa mara zote ana nia ya kuua hoja zinazo mgusa yeye na Malecela lakini lazima ajue kaa alitueleza we Tanzanians we can go to helll hatutamuacha aende hivi hivi. Mzee baada ya umakamu atasahaulika kama Msuya.


Mzee JM is now over 75 hebu niambie kwa nini asisahaulike...amekuwa strong muda wote huo (hongera sana kwake) ni wakati sasa akapumzika na yeye jamani..iwe kwa yeye mwenyewe kupenda au kuondolewa...new vision inahitajika.
 
japo si pahala pake na mie mwaweza nifanyia favor ya huo ufunguo nshachoka kugonga, MKJJ ntu nzima mwenzio usiniache nnaazirika
 
Bob Mkandara,
Thank you, man. Kama Mzee ES anakusikiliza basi mimi sina noma. I am ready to forgive and forget---na kuendelea kukata issues.
 
Mtumwitu,

kama hawataki kukufungulia vunja mlango, si unalo lile shoka lako unalo katia miti mwituni???
 
Anza mimi ni kumaliza tuu, tena anytime wewe nivue mimi nitakuvalisha nguo tena za kisasa, kama vile za leo na bado ninazo ndio kwanza nimerudi kutafuta some more wewe kaa mkao wa kuchuchumaaa!

Bob ni mshikaji wangu damu damu, lakini ndugu yangu kwenye hili ninakuomba ukae pembeni, mtoto akililia wembe dawa ni kumpatia, sina suluhu kwenye hili, anayetaka personal waaah! anayetaka ishu tutakata ishu na siendi kokote nipo hapa mpaka mwisho wa dunia, anayezunguka kwenye pm kuwaambia watu kuwa ananijua he better know me, maana so far sijamuona anayenijua na mimi pia sijui mtu!

William ni mshikaji angu damu damu, na nimemuahidi kuwa pamoja na ufuatiliaji wake mimi nipo imara wala sitetereki!

Ngoma ni nzito mno hiii bro!
 
Tuafahamu kwambaq baadhi ya wanaforum hapa mnajuana binafsi, hata hivyo kumbukeni kuwa forumites wengi hatufahamiani na mtu kabisa. Forum hizi utamu wake ni pale mnapochambua jambo bila kuogopa lolote, ndiyo maana watu wengi hawatumii majina yao halisi ili kusudi wale dona la ishu bila hata kunawa. Sasa wale mnaojuana, msituharibie uhondo sisi wale ambao hatujuani na forumite yeyote. Tunataka kujadili "nukta" zinazotolewa na mtu bila kujali background yake.
 
Makundi ya kusaka urais 2015 yaanza

*Mawili yanatoka katika mtandao
*Kauli za Nyerere zatumiwa vibaya
* Vigogo wawekeana vigingi kuingia NEC
*Wengi waiga mbinu ya Kikwete

Na Boniphace Makene

HARAKATI za kusaka madaraka ndani ya chama tawala (CCM) katika ngazi tofauti, zimeanza kuchukua sura mpya, huku kukiibuka makundi yenye uchu wa kujaza nafasi mbalimbali, wote wakilenga kujijengea mtaji wa kisiasa hasa katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, umebaini kuwa makundi yaliyopo yanaiga mtindo alioutumia Rais Jakaya Kikwete, ambaye mpaka alipoukwaa urais katika uchaguzi uliopita, alitumia takribani miaka kumi kujiimarisha katika chama na kujenga mtandao uliomuwezesha kuukwaa uteuzi wa chama.

Rais Kikwete mwenyewe aliwahi kukiri kuwa katika harakati za kusaka urais, alijiandaa kwa takribani miaka kumi, hali ambayo imewafanya wenye dhamira ya kutaka kumrithi amalizapo muda wake, kuanza kujipanga kufuata nyayo hizo.

Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni ya 33 (1) ya uchaguzi ya CCM toleo la mwaka 2005, mwanachama yeyote haruhusiwi kuanza kampeni za aina yoyote kabla ya kuteuliwa.

"Wanachama wenye nia ya kugombea hawaruhusiwi kufanya kampeni ya aina yoyote kabla ya majina yao kuteuliwa na kikao kinachohusika," kanuni hiyo inaelekeza.

Hivi sasa kuna habari kwamba tayari yapo makundi mawili yanayotafuta fursa za kuukwaa urais baada ya Kikwete. Makundi haya yalikuwa pia yakimuunga mkono Kikwete katika harakati zake na yanafahamu vema mbinu alizotumia, hali inayowapa fursa ya kuzitumia bila kumezwa na mkondo wa sheria na kanuni za uchaguzi za CCM.

Gazeti hili pia limebaini kuwepo kwa kutofautiana kuhusu nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama(NEC). Baadhi ya makada wa CCM walio nje ya serikali wanaitazama NEC kama Bunge la chama, na wamedhamiria kuingia ndani ya chombo hicho ili waweze kutoa changamoto za uhakika kwa serikali.

Kundi hili linaamini kuwa uwakilishi katika NEC unahitaji watu walio nje ya serikali ili waweze kuipangia serikali agenda za kufuata na sio kukubaliana na kila mpango wa serikali.

"Ni vigumu kwa waziri kumueleza ukweli rais wa nchi wakati anafahamu kuwa yuko katika Baraza. Hapa Rais anaingia kama Mwenyekiti na anatakiwa kutokuta wajumbe ambao si mawaziri ili kuweza kujenga mipango mizuri ya kuendesha nchi," alisema kada mmoja wa CCM huku akibainisha pia dhana ya chama legelege kuzaa serikali legelege.

Mkakati huo unaoonekana kuwa umelenga zaidi kuwakwamisha mawaziri na waandamizi wengine wa serikali ili wasiingie katika NEC.

Lakini kundi la mawaziri na viongozi wengine waandamizi ndani ya serikali nao wana lengo mahsusi la kuhakikisha kuwa chama kinafanya yale serikali inayoyapenda na sio vinginevyo. Hawa wanataka ujumbe wa NEC na ule wa Kamati Kuu(CC) kwa ajili ya kuhakikisha kuwa chama katika ngazi hizi muhimu za juu kinashikiliwa na watu wenye utii usio na shaka kwa serikali.

"Huu ni wakati mzuri wa kukirejesha chama nyumbani. Tunataka kuwa na chama kinachotii maamuzi ya serikali hivyo hiki ni kipindi kizuri kwetu kutumia mbinu za aina yoyote kufanikisha hili," waziri mmoja mwenye nia ya kuwania ujumbe wa NEC amelidokeza gazeti hili.

Wakati haya yakiendelea, hali ya kujitangaza na kujipigia chapuo kwa wanachama wa CCM inazidi kuchukua kasi. Wapo baadhi ya wajumbe ambao wametangaza nia na kukutana na ukuta pale walipowafikia vigogo wanaodhani kuwa wanaweza kuwasaidia kupata nafasi wazitakazo.

Mmoja wa mhanga wa hali hii ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Chifupa, ambaye ameweka bayana nia yake ya kutaka kuongoza Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya chama hicho (UVCCM) katika uchaguzi wa mwakani, na hivyo kwenda kumuomba kigogo mmoja wa umoja huo ampigie debe, lakini akagonga mwamba.

Kigogo huyo naye kuonyesha namna alivyo na nafasi muhimu, akatumia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere, aliyoitumia wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Nyerere alisema; "siwezi kuruhusu mbwa kubweka katika nchi yangu." Kauli hii iliwalenga viongozi dhaifu kutoka kambi ya upinzani waliokuwa wakitaka urais.

Kigogo huyo wa UVCCM yeye akamwambia Chifupa kuwa; "siwezi kukuruhusu kuongoza UVCCM labda mauti yanikute." Kigogo huyo alipoulizwa maana ya kutumia kauli hiyo nzito inayofinya haki na uhuru wa demokrasia, alishindwa kutoa sababu za aina yoyote huku akisisitiza tu kuwa Chifupa hana sifa za kuiongoza UVCCM.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Amos Makalla, alikaririwa na vyombo vya habari baadaye akisema kuwa; "anayetamani madaraka sasa ni mtu asiyejiamini." Kauli hii haikutazama wala kulenga kuvunjwa kwa taratibu na kanuni za uchaguzi za CCM, ambazo Chifupa anaonekana tayari kuzivunja na kuzikiuka.

Ngome ya UVCCM inaelezwa ilitumiwa vilivyo na kambi ya Kikwete katika kufanikisha kupata kiti cha urais mwaka 2005. Kuna vigogo wanaotamani nafasi mwaka 2015 ambao wanaitazama UVCCM kama eneo muhimu kabisa linaloweza kumfanikisha mgombea yeyote kupata uteuzi katika chama.

Kwa sasa kuna taarifa kuwa kigogo mmoja kutoka UVCCM ana nia ya kusaka urais 2015 na anachofanya yeye na mtandao wake kwa sasa ni kuhakikisha wanapata warithi ambao watakuwa wagumu kurubuniwa na kuiasi kambi iliyowaingiza madarakani.

Kuonyesha kuwa harakati za kujipanga kwa uongozi ndani ya chama hicho zimeshika hatamu, hivi karibuni Kamati Kuu ya CCM iliwasimamisha makada watano wa chama hicho na kuwaweka katika uangalizi kwa miezi 18 kwa madai kuwa wamekiuka kanuni kwa kuanza kampeni kabla ya wakati.

Mjumbe mmoja wa NEC alipoulizwa mazingira ya kutolewa kwa adhabu kama hizo alisema ingawa zipo mara kwa mara, lakini mara nyingi zinawalenga watu ambao hawatakiwi katika chama au mfumo wa kipindi hicho.

"Kilichopo hapa kuna mambo kama kulipa visasi na pia suala hili la makundi kudumu hata baada ya chaguzi. Ni wazi wengi sasa wanafanya kampeni kupitia mikutano ya serikali na shughuli nyingine za kijamii lakini hatujaona wakiadhibiwa," kilieleza chanzo hicho.

Kitendo cha Kamati Kuu kutoa adhabu kinatoa picha tu ya namna kulivyo na papara za kusaka madaraka kwa makundi kadhaa huku kampeni za kuvunjana nguvu zikishika kasi chini kwa chini. Kila kundi lina nia na malengo yake lakini kubwa ni kutofautiana kulikoambatana na harakati za urais 2005.

Kuna makundi yanayotaka kurejesha heshima baada ya kuonekana yanabaguliwa katika shughuli za chama na serikali, huku kundi la mtandao likijivunia kutumia nguvu zake kubakia serikalini na pia kukiweka mkononi chama.

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Phillip Mangula, alipoulizwa na Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalum yaliyofanyika katikati ya wiki alisema; "chama kinatoa adhabu pale anapopatikana mtu wa kutoa shtaka na kisha kufuatiwa na uchunguzi. Huenda kuna matukio yamefanyika lakini hakukuwa na mtu wa kushtaki au ushahidi kukosekana."

Kauli hiyo ya Mangula ilitokana na swali lililotaka kujua nini kilifanya kambi mojawapo ifanye kampeni kwa zaidi ya miaka kumi bila kugundulika huku ikiwa imevunja utaratibu wa kanuni za uchaguzi namba 33 hasa vifungu vya 1, 4 na 7.

Vifungu hivyo kwa ujumla wake vinaelezea, mwiko wa kuundwa vikundi visivyo rasmi ndani ya chama na kushiriki katika kampeni za kichinichini, kutumia jumuiya ya chama ili kumjenga mgombea mmoja na kubomoa wengine na kuanza kampeni kabla ya wakati.

Ni jambo lililo wazi sasa kuwa kundi la mtandao lililomuunga mkono Kikwete bado lipo huku kukiwa na taarifa zinazoeleza kugawanyika kwa kundi hilo kuwa mawili yaani mtandao maslahi na mtandao matumaini.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaeleza pia kuwa, hata makundi yanayotamani urais mwaka 2015 yanatoka katika kundi hili huku sifa zilizotumika kuangusha wagombea wenye umri mkubwa sasa zikibadilishwa kufuatia kuwepo makundi yanayotofautiana kiumri.

"Mtu yeyote anaweza kugombea la msingi ni umri wa kuanzia ambao ni miaka 40. Unaweza kuongoza hata ukiwa na miaka 80 japokuwa mimi naona ni muda mzuri wa kupumzika badala ya kung'ang'ania kuwa madarakani," anasema Mangula ambaye sasa kaamua kuwa mkulima baada ya kutumikia CCM kama Katibu Mkuu kwa miaka 10, kipindi kirefu kuliko Katibu yeyote mwingine aliyewahi kuratibu kazi za chama hicho.

CCM inafanya uchaguzi wake mkuu mwaka huu kuanzia ngazi za shina hadi taifa. Uchaguzi huo utaendelea mwakani ambapo jumuiya mbalimbali zilizomo katika CCM zitafanya chaguzi zake kuanzia ngazi za chini kabisa hadi taifa.

SOURCE: http://www.mwananchi.co.tz/habari/habari0.asp
 
CCM yanyemelewa na kashfa ya makundi

na Charles Mullinda

KUNA kila dalili za wazi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa kinanyemelewa na kashfa nzito ya viongozi wake kutokuwa na maadili mema ya uongozi, ambayo chanzo chake ni makundi yaliyoota mizizi ndani ya chama hicho.
Ingawa hakuna ushahidi wa wazi wa kulithibitisha jambo hilo, ushahidi usio na tone la shaka unaothibitishwa na hali ya mambo inavyoendelea sasa ndani ya chama hicho wakati kikielekea katika uchaguzi wa viongozi wake, unaonyesha hivyo.

Kuibuka kwa kashfa ya ufuska inayomwandama Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Amina Chifupa, ambayo imesababisha atalikiwe na mumewe, Mohamed Mpakanjia, ni mlolongo wa vita ya kuchafuana na kukashifiana, kwa nia ya kuwania madaraka.

Vita hiyo chafu ambayo imekuwa ikiendeshwa na kundi la wanamtandao, sasa inaonekana kushika kasi tena wakati chama hicho kikielekea katika uchaguzi wa viongozi wake, baada ya kutulia kwa muda, ulipomalizika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Amina, mmoja wa wabunge vijana wanaoibukia, na mwenye ushawishi katika kundi lake la vijana, anadaiwa kuundiwa kashfa ya kutokuwa mwaminifu katika ndoa yake na kundi la wanamtandao, ambalo limekuwa na sifa ya kuwaengua katika mchuano wa kugombea nafasi za uongozi wale wanaotofautiana na kundi hilo.

Amina, ameingia katika mtego wa wanamtandao baada ya kuonyesha nia ya kugombea nafasi ya juu ya uongozi wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, UVCCM, nafasi ambayo inadaiwa kuwa tayari amekwishaandaliwa mtu wa kuirithi na wanamtandao, baada ya mwenyekiti wa sasa wa umoja huo kumaliza muda wake hivi karibuni.

Mwenyewe alikiri hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, alipozungumza na vyombo vya habari kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake, na kueleza kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM walikuwa wameamua kwa makusudi kuiharibu ndoa yake ili kupunguza kasi yake ya kuwania uenyekiti wa UVCCM.

Ingawa aliahidi kumtaja mmoja wa viongozi waliohusika na mpango huo, adhima yake hiyo haikufanikiwa baada ya kushindwa kufika Idara ya Habari (MAELEZO) kwa ajili ya kulipua bomu kama alivyopanga, kwa kile kilichoelezwa na baba yake mzazi, Hamis Chifupa, kuwa familia imemkataza.

Hata hivyo, Amina alikaririwa na vyombo vya habari akieleza kuwa kashfa ya ufuska iliyomfanya aachike kwa mumewe iliundwa na mmoja wa viongozi wa juu wa CCM, ambaye pia ni Naibu Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.

Kwamba, mumewe kabla ya kumpa talaka alionekana akitoka ofisini kwa kiongozi huyo wa CCM na serikali, kiongozi ambaye alikwisha kuonyesha nia ya kutomuunga mkono katika azima yake ya kuwania uenyekiti wa UVCCM.

Jambo hilo lilitafsiliwa na Amina mwenyewe pamoja na baadhi ya mashabiki wake kuwa kiongozi huyo ndiye aliyezusha uongo huo, lengo likiwa kumchafua ili ashindwe kutekeleza azima yake.

Mumewe Amina, naye amekwisha kukiri kufika ofisini kwa kada huyo wa CCM muda mfupi kabla ya kwenda kumtaliki mkewe, ingawa hajaweka wazi kitu walichokiongea na kada huyo wa CCM anayedaiwa kuwa mwanamtandao.

Kashfa hii inayodaiwa na Amina kuwa ni ya kuunda, inaingia katika orodha ndefu ya kashfa za aina hii zilizowahi kuwakuta wana CCM wengine waliokuwa wakipambana na kundi la wana mtandao katika chaguzi mbalimbali na kuonekana kuwa tishio.

Tuhuma za ufuska wa Amina zinaingia katika rekodi ndefu ya siasa za kuchafuliana majina zilizoanza kujitokeza waziwazi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, baada ya wagombea waliokuwa wakilipinga kundi la wanamtandao, kuandamwa na kashfa nyingi nzito, ambazo kwa kiasi kikubwa ziliwachafulia majina na kusababisha waonekana kuwa viongozi wasiofaa kushika hatamu za uongozi wa taifa hili.

Miongoni mwa waliokumbwa na makali ya joto la kuundiwa kashfa na kundi la wanamtandao ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu Tatu, Frederick Sumaye, aliyekuwa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Sumaye alikabiliana na wakati mgumu baada ya kuanza kuandamwa na vyombo vya habari ambavyo wakati akiingia madarakani vilimpamba kama kiongozi mchapakazi, vilipoanza kumshambulia kwa kuanika kashfa mbalimbali zilizodaiwa kufanywa naye, huku ikiwa haifahamiki chanzo cha kashfa hizo.

Kiboko kilichotumiwa na wanamtandao kumpiga Sumaye kilitumiwa pia kumchapa Profesa Mark Mwandosya ambaye alihusishwa na uuzaji mbaya wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), akidaiwa kuhongwa na wawekezaji walionunua kampuni hiyo.

Prof. Mwandosya alijikuta akichafuka vibaya mbele ya macho ya jamii baada ya kudaiwa kuwa kampuni iliyonunua TTCL ilimpa kazi mwanawe wa mwisho, na baadaye akadaiwa kuchangisha fedha za chama huku akiwa si mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Wengine waliokwisha kushughulikiwa na kundi hili la wanamtandao na kuonekana watu wasiofaa kushika nafasi za uongozi walizokuwa wakizitaka ni pamoja na Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye alidaiwa kuwa Mwarabu, pamoja na kashfa nyingine nyingi mbaya ambazo ziliharibu kabisa sifa yake ya utumishi uliotukuka kwa taifa hili.

John Samuel Malecela, naye ni muhanga wa vita hii na alijeruhiwa kwa kukashifiwa kwamba Mwalimu Nyerere tangu awali hakumkubali kuwa kiongozi wa juu wa taifa na pia umri nao ulitumiwa kama kigezo cha kummaliza.

Kuibuka kwa vita ya kuchafuana ndani ya CCM kulianza kuonekana katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ambayo ina wanachama wengi katika kundi la wanamtandao, baada ya Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo, Dk. Emmanuel Nchimbi, kutofautiana na aliyekuwa Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Frank Uhalula.

Mgogoro baina ya viongozi hao wa UVCCM ulimlazimisha Rais Mkapa kuamua kuwatenganisha kwa kuwapangia majukumu makubwa yaliyowafanya wasikae pamoja makao makuu ya umoja huo kwa muda mrefu.

Dk. Nchimbi ambaye alikuwa tayari amekwishamvua madaraka ya Katibu Mhamasishaji, Uhahula, na kuyakabidhi kwa Dk. Diodorus Kamala, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Uhahula aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.

Kinachoashilia kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanakerwa na tabia hiyo ya kukashifiana ambayo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na kuwapo kwa makundi, ni hatua ya hivi karibuni ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuyavunja makundi ndani ya chama hicho.

SOURCE: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/13/habari1.php
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom