Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Naona mnaaza kusagiana kunguni wenyewe kwa wenyewe. Huu mvurugano wenu, ni sehemu tu ndogo ya ule uhuni mlioufanya mwezi Oktoba Mwaka 2020!Baadhi ya wavuvi waliochomewa nyavu zao wakati Mpina akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wameomba achukuliwe hatua na kuwalipa fidia.
Wakati hilo likiendelea baadhi wametaka CCM isimpe tena nafasi ya kugombea Ubunge mwaka 2025 baada ya kushiriki kupora ardhi zaidi ya hekari elfu moja na kujimilikisha yeye na marafiki zake.
Eneo la ardhi linalotajwa ni la maelfu ya familia masikini katika vijiji vya Dalla na Mbwade mkoani Morogoro.
Chanzo: Cheche Times
Na ikikaribia 2025, tunatarajia kuona mvurugano zaidi baina yenu.