Kasi ya Rais Samia yawapoteza CHADEMA katika ramani ya siasa, hakina tena ushawishi kwa Watanzania

Wapewe kwanza ulingo sawa wa kufanya siasa majukwaani ndio sisi wananchi tuwalinganishe!!
 
Unaaandika ukiwa jirani na LUSIFA huko JEHANAM?
 
No facts. Just porojo
 

Nini kweli CCM inabadilika kuendana na wakati, ndio maana tunashuhudia ikitegemea vyombo vya dola kuendelea kukaa madarakani. Tofautisha kukubalika na kushurutisha kukubalika. Kwahiyo mabadiliko ni kuwa na sura mpya ya mwenyekiti? Au hujui mabadiliko ni nini boss? Kinachojivunia ccm ni kuwa na wananchi waoga ambao CCM inaweza kukaa madarakani bila ridhaa yao na wakatulia kwa hofu.
 
No facts. Just porojo
Facts Ni nyingi tu ,jaribu kuangalia namna habari za chadema zinavyonyimwa kipaombele kwa vituo vya TVs na hata mitandao ya kijamii Kama ilivyokuwa awali, hata wakiita waandishi wa Habari muitikio kwa Sasa Ni mdogo Sana, maazimio ya vikao vyake hasa ya kamati kuu yamekuwa yakipuuzwa na watanzania,
 
Kusema wananchi Ni waoga Ni kuwatukana watanzania, watanzania wanajitambua na wanatambua Ni chama kipi Cha kukuamini na kukupigania, kwa Sasa watanzania Wana Imani na matumaini makubwa Sana na serikali ya CCM chini ya Rais Samia
 
Tozo Ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu, lazima tuijenge nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe na tujivunie maendeleo na mafanikio yanayotokana na jasho letu wenyewe,
Wewe huwa unapewa mrejesho kuwa kiasi fulani cha fedha kimekusanywa kutokana na tozo, na kimetumika vipi!?
 
Wewe huwa unapewa mrejesho kuwa kiasi fulani cha fedha kimekusanywa kutokana na tozo, na kimetumika vipi!?
Siyo Mimi tu Bali watanzania wote tunapewa mrejesho, mfano sote tunafahamu kuwa tozo zimesaidia ujenzi wa vituo vya Afya takribani 234 hapa nchini, hapo bado sijazungumzia upande wa secta ya Elimu ambako huko Rais Samia amefanya maajabu makubwa kuwahi tokea tangia nchi hii ipate Uhuru, ambako Sasa wanafunzi wanasoma na kwenda shule kwa wakati tofauti na zamani ambapo Kuna wanafunzi walikuwa wanakwenda muhula wa pili kutokana na upungufu wa madarasa ulio kuwa unaKuwepo
 
Kusema wananchi Ni waoga Ni kuwatukana watanzania, watanzania wanajitambua na wanatambua Ni chama kipi Cha kukuamini na kukupigania, kwa Sasa watanzania Wana Imani na matumaini makubwa Sana na serikali ya CCM chini ya Rais Samia

Wananchi wanawaamini kisha polisi wanabeba mabox ya kura kujazia kura za CCM, kuwaengua wapinzani mpite bila kupingwa, kwa ule uhayawani tunaouna kwenye chaguzi zetu ili CCM watangazwe washindi kwa shuruti, mjinga wa kiwango cha juu sana ndio unaweza kumwambia huu uhuni.
 
Endelea kuandika tu kama umekaririshwa. Kuna siku utakuja kujielewa!
 
Kinachowaangusha Ni kuwa nyinyi huwa Hakuna Sera Wala ajenda za kugusa maisha ya watanzania, huwa hamna hata ilani ya kueleweka, angalia mfano 2015 mliwaambia watanzania wakasome ilani yenu mtandaoni, Sasa sijuwi huko mtandaoni wangekuwa wanapewa na majibu ya maswali yao? Kiufupi ni kuwa upinzani hamueleweki mnasimamia Nini, 2020 ndio hata haikueleweka ilani yenu ipo wapi maana Lisu ndio alikuwa ilani yeye Kama yeye ndio maana akawa anajiongelea chochote atakachojisikia
 
Kila la kheri mkuu!
Tuendelee kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani katika kuijenga nchi yetu,lakini pia tutambue kuwa Rais wetu Ni mwanadamu na siyo malaika hivyo Tumpe moyo na kumpa faraja ya Kuendelea kusonga mbele na tumombee ili mwenyezi Mungu amjalie Afya njema na nguvu za kututumikia watanzania
 
Mnajitekenya halafu mnacheka wenyewe!
ccm ndio imekataza wengine kufanya mikutano!
ccm ndio wanafanya mikutano wenyewe!
ccm ndio haohao wanasema CHADEMA kimepotea!
Shame! Shame!
 
Mnajitekenya halafu mnacheka wenyewe!
ccm ndio imekataza wengine kufanya mikutano!
ccm ndio wanafanya mikutano wenyewe!
ccm ndio haohao wanasema CHADEMA kimepotea!
Shame! Shame!
CCM haifanyi mikutano Bali inafuatilia na kukagua utekelezaji wa ilani yake maana CCM ndio iliyoomba kura kwa watanzania na ndio itakayoulizwa juu ya ahadi zake, hivyo lazima ifuatilie namna ahadi zake zinavyotekelezwa na namna serikali yake inavyowatumikia watanzania kwa utumishi wa kugusa maisha ya watu kwa kutatua kero na kutoa majibu kwa maswali ya wananchi
 
Au JF tuanzishe chama chetu, tukatoe chachu Kwa serikali.
 

Kwahiyo watanzania ni wajinga hivyo hawawezi kuingia mitandaoni kusoma mambo? We unashinda huku mitandaoni, unamuandukia nani kama watanzania wako huko mitaani? Ww lazima utakuwa ni mzee, maana wengi ndio huwa na hizi sababu za kipuuzi.

Hizo ilani mnazowapelekea wananchi huwa wanawawahoji wapi huo ubora wake, wakati hata midahalo huwa mnaikimbia, na kuishia kuwahubiria kama makanisani? Watu wamelipuuza box la kura maana mnatumia mabavu kubadilisha matakwa yao. Mmebaki kuleta propaganda mfu zisizo na kichwa wala miguu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…