Kasi ya Rais Samia yawapoteza CHADEMA katika ramani ya siasa, hakina tena ushawishi kwa Watanzania

Vipi zile hela za join the chain? Watu wanauliza mbona kimya hakuna mrejesho? Au mmeshapigia maji Kama kawaida yenu
Kichwa imepigwa lock haiwezi kufkiri tofauti Mana ukiona opposition unafkiri Ni CDM🤣
 
Hapana mkuu wangu Mimi siwatukani chadema Ila nawaeleza ukweli naouona kwa kuiangalia chadema ya Sasa na Ile ya 2015 kurudi nyuma Hadi 2010 ambapo ndipo ilikuwa imepamba Moto na kuwavuta vijana wengi na watu wengi kuiunga mkono na kujiunga nayo
Mama hana kasi yoyote wala ushawishi kwa jamii bali kinachotokea kwa CHADEMA ni kukubsali kupata maslahi ya kutunisha mifuko yao toka kwa huyo mama, na si CHADEMA tu hata ACT na ni wale wale, Zitto Kabwe alikuwa ni mtu wa kupambana na MAgufuli, zikitoka takwimu za TRA za makusanyo ya kodi, yeye anakuja na za kwake lakini leo hii humsikii akitamka lolote, kwisha habari yao wote.
 
Now hawako free kufanya siasa kama wakati wa JK

Hayo unayoongea ingekuwa chadema wako huru kama kipindi kile sidhan kama ungesema hivyo now

Hoja ya kila Mbunge aongee kwenye Jimbo lake ndio imeua upinzani sana
 
Kwani wewe Nani amekuzuia kuja na takwimu zako? Watu wameridhishwa na utendaji kazi wa Rais Samia
 
Now hawako free kufanya siasa kama wakati wa JK

Hayo unayoongea ingekuwa chadema wako huru kama kipindi kile sidhan kama ungesema hivyo now

Hoja ya kila Mbunge aongee kwenye Jimbo lake ndio imeua upinzani sana
Mbona hata kipindi hicho mlipiga makelele kuwa mnabanwa na hampo huru?
 
CCM wanajua nguvu ya chadema ukiwaacha huru na ndio maana waleta Yale Mambo ya kila Mbunge aongee kwenye Jimbo lake

CCM wanapata fursa nyingi mfano:

Kila sehemu ambayo rais atahutubia na wao wanapata nafasi ya kupiga siasa

Kitu ambacho chadema hakuna,

Kama tunataka kupima siasa then kila mtu awe free
 
Kwani marekani wakimaliza uchaguzi ulishaona wanazulula mitaani Kama nyinyi wapinzani mnavyotaka hapa? Huu Ni muda wa CCm kuwatumikia watanzania wanyonge
 
Mbona hata kipindi hicho mlipiga makelele kuwa mnabanwa na hampo huru?

Tangu enzi ya magu chadema haiko huru, wakati wa jk ndio ilikuwa huru kufanya mikutano mikubwa mikoani na unakuta mkutano mmoja kuna wabunge 10 wakali

Which Kwa sasa hakuna, sasa watafanya siasa wapi?

CCM inajificha kwenye kivuli cha kufatilia ilani otherwise na wao wangekuwa Hoi
 
Kwani marekani wakimaliza uchaguzi ulishaona wanazulula mitaani Kama nyinyi wapinzani mnavyotaka hapa? Huu Ni muda wa CCm kuwatumikia watanzania wanyonge

US unafananisha na Africa?

Unajua unachoongea lkn? US na ss hakuna vitu tunafanana kuanzia rangi mpaka mfumo wa siasa
 
Kwani marekani wakimaliza uchaguzi ulishaona wanazulula mitaani Kama nyinyi wapinzani mnavyotaka hapa? Huu Ni muda wa CCm kuwatumikia watanzania wanyonge

Watanzania wanyonge wanatumikiwa na CCM au Kodi zetu wote?

Au Kodi mnatoa CCM tu
 
Mzee unatumia Kilevi gani?
 
Watanzania wanyonge wanatumikiwa na CCM au Kodi zetu wote?

Au Kodi mnatoa CCM tu
Hizo Kodi unazani zikikosa usimamaizi madhubuti utaziona? Unafikiri Kodi yako pekee inatosha kuendesha na kuijenga nchi hii? Tambua Kuna kazi kubwa na ya ziada inayofanywa na mh Rais katika ujenzi wa Taifa letu ikiwemo kuvutia wawekezaji hapa nchini, watalii Kama ulivyoona ubunifu wa royal Tour
 
Tatizo lako unadhani Chadema ndio tatizo la nchi. Chadema ni political competitor wa CCM. Halafu kuwa mzalendo sio kuwatukana Chadema kila siku.
Umejaza minofu tu naongeza mchuzi kidogo " Kuwa mzalendo sio kuwatukana chadema na kujipendekeza CCM.
 
Umesema katika siasa hakuna adui/rafiki wa kudumu,kama hivyo ndivyo watashindwa vipi kumkosoa waliyemsifia jana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…