Kasi ya wanandoa kutoka nje ya ndoa zao inatisha na kutishia uhai wa taasisi ya "NDOA"

Kasi ya wanandoa kutoka nje ya ndoa zao inatisha na kutishia uhai wa taasisi ya "NDOA"

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za muda huu waungwana wa hapa jukwaani.

Sijui ni mimi peke yangu tu ama ni macho ya wengi pia yanatazama kama nitazamavo mimi....

Nimekuwa nikishuhudia matukio kadhaa ya kustaajabisha, kushangaa lakini pia yana hudhunisha kuhusu matukio ya wanandoa kutoka nje ya na vile vile namna ambavyo walengwa wanavyochukulia kuwa ni hali ya kawaida kabisa..

Katika mikusanyiko ya watu na vijiwe vya kahawa nasikia baadhi ya watu wakitoa mitazamo yao kuhusu jambo hilo yenye kushangaza kuogofya kwenye masikio ya waungwana..

Jamaa anasema..." siku hizi hakuna mwanamke wa peke yako kaka, kikubwa kuheshimiana tu afanye nisije Tu"

Dada mmoja naye anasema kuwa.."Hakuna mwanaume asiyetoka na mwanamke nje ya mkewe... kikubwa heshima tu akafanyie huko uchafu wake"

Yaani imefikia hatua mpaka wanandoa wanajua kabisa kuwa kwenye muunganiko huu kuna wengine wa ziada na nafsi zao zimeridhika na hilo

Thamani ya muunganiko mtakatifu wa ndoa iko wapi?

Dhumuni hasa la ndoa liko wapi ikiwa mtu anaweza kuyafanya machafu yaliyomsukuma kufunga ndoa ili apate stara?

Ni heshima ipi inayozungumziwa na hawa wanandoa Hali ya kuwa unajua fika kuwa unafanya lile lisilompendeza mwenzi wako?

Muendelezo wa matendo machafu haya yanapelekea vijana kutoona umuhimu wa kuoa ikiwa anawaona wanandoa wanafanya yale wanayoyafanya wao.

Tumefikaje huku..?
 
Kuna siku nilienda one stop center TMK.. hakimu akawa anasikitika ndoa zinavunjika sanaa, kiasi kwamba inatishia
Kwa kweli hata mimi nimepata kuona takwimu ya ndoa zinazovunjika mahakamani......achilia mbali wale wanaoachana mitaani kimya kimya..... achilia mbali kesi za ndoa zilizojazana huko BAKWATA na kwenye mabaraza ya wazee wa usuluhishi makanisani ni balaa.....
 
Kwa kweli hata mimi nimepata kuona takwimu ya ndoa zinazovunjika mahakamani......achilia mbali wale wanaoachana mitaani kimya kimya..... achilia mbali kesi za ndoa zilizojazana huko BAKWATA na kwenye mabaraza ya wazee wa usuluhishi makanisani ni balaa.....
Hali ni mbaya sana, na mtu akishavunja anaenda kuwa mwalimu wa kuvunja ndoa za watu wengine
 
What is the solution je utaish peke ako mkuu
CHAPA ILALE kama huwezi kuvumilia kuchapiwa!!!

Unaogopa kuishi mwenyewe huo ushamba wenu ndio mnaanza kufa na mawazo kisa kulazimisha kuishi na washenzi au unajikuta unafanya mauaji wakati ukiishi mwenyewe unachapa unasogeza unachapa mwendo mdundo. Tena kama hutaki JAM UNAENDA UNAFUNGA KIZAZI🤗

Hutapata kesi za kijanga jinga mara dawati la jinsia mara sijui mahakamani mnakabana mashati kuhusu CHILD SUPPORT.Wewe mtu akikubambikia straight mbaenda mahakani na vithibitisho na daktari anatoa ushahidi kuwa wewe unatumia uzazi wa mpango🤗🤗🤗

Ni humu tuuu kwanza faida ya uzazi iko wapi watu wanakufa kila siku huko Gaza na pia kuna majanga ya kidunia kila uchwao so wewe kuzaa au kutokuzaa ni nothing huongezi wala hupunguzi chochote dunia tiyari iko balanced ,ukichoka KUZICHAPA unatulia unasubiri kufa kwa amani!!!

📌Kataa ndoa,ndoa ni utapeli!!!
 
Back
Top Bottom