Kwasababu ukitazama kwa jicho lingine tafsiri ya ndoa kwangu naweza kusema ni challenge ya watu wawili kupambana kuweza kuishinda asili.
Asili gani hapa nayoizungumzia.
Maisha ya binadamu yamezungukwa na mambo mengi na katika hayo mambo yapo ambayo hayatoki nje yake bali yapo ndani yake kwa maana ni asili ambayo inaishi ndani yake.
Na moja ya hiyo asili ni "kinai"
Kukinai ni jambo la kiasili la mtu kupunguza matamanio dhidi ya jambo fulani.
Kwasababu mahusiano ni kitu ambacho kinaishi kwenye circle ya hisia, hisia ambazo zinaweza kuwa affected na "Kinai" basi hapa ndio tunaweza kuona outcome ya mambo mengi ikiwemo cheating, Talaka nk.
Kinai inaweza kutokea kwa mazingira mengi lakini ile iliyo kuu mara nyingi hutokea baada ya mtu kukizoea sana kitu.
Ukikizoea sana kitu automatically unapunguza hisia za kimshangao na ule msisimko unapotea kabisa.
Ukimpenda sana mtu akakuvutia na hisia zako zitakuwa juu sana hususan pale ambapo unakuwa na shauku ya kutaka kufanya jambo fulani litaloweza kustawisha upendo wako kwake halafu hiyo nafasi ikawa haipatikani kirahisi.
Mfano siku ya kwanza kumzimikia manzi unakuwa na hisia kali sana na pale ambapo unamvizia ili uteme sumu halafu ukakutana na mazingira yake kuwa ni geti kali na ulinzi mwingi.
Hapo ndio hisia zinazidi kuwa juu kwasababu ile desire ya kutaka kumuona halafu nafasi hiyo hauipati ndio inayochochea hisia zizidi kupanda.
Hii ndio moment ambayo wengine wanasema hawawezi kuishi bila hao wenza wanaowafukuzia.
Lakini suddenly ukamuoa, na sasa ukawa unapata airtime ya kutosha ya kumuona kila siku na sio tu hivyo mkawa mnala kila kitanda kimoja, mnazagabuana na vitu kama hivyo.
Baada ya miezi michache mbele ukikaa chini utagundua zile hisia ambazo ulikuwa nazo kipindi chenu cha dating ni tofauti na hizi hisia ulizonazo baada ya miezi kadhaa ya ndoa.
Kipindi chenu cha dating inawezekana alikuwa anaku turn on kwa tabasamu lake tu. Lakini saizi hata akuvulie unaweza usidise.
Umemchoka.
Hata awe Beyonce au Miss world utamchoka tu na kuna time unaweza ukawa unajiona mjinga ukikumbuka kipindi unamfukuzia uliwahi kumwambia upo tayari kufa kwa ajili yake.
Ukifikia hatua ya kukinai utajiona mjinga ukikumbuka kipindi unamfukuzia uliwahi kukosana na rafiki zako wa tangu utotoni kisa yeye.
Ukimchoka ndio kinai yenyewe hiyo.
Kwa kiwango kipi? Hii SI Unit ya kiwango ndio maana halisi ya ndoa.
Wapo waliokinai ila wakaweza kutulia kwenye ndoa zao ili kutunza maadili ya ndoa na kiapo.
Wapo waliokinai wakashindwa kuendelea na mahusiano ambayo kila mmoja hana hisia na mwenzake hivyo wakaafikiana kupeana talaka. (Na muda mrefu wa talaka ambao watakuwa separated unaweza ku restore hisia zao tena)
Na hao wengine ndio hao ambao wana cheat.