GE2025 Kassim Majaliwa atangaza ghafla kutogombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kashasoma alama za nyakati. Maana anajua kabisa hawezi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu tena. Yupo aliyeandaliwa na anafahamika haswaaa na yeye analifahamu hilo.

Sina shaka na nafasi yake ya Ubunge angeshinda kura za maoni kwa kishindo na kuteuliwa kugombea tena.

Waliomshauri aachane na Ubunge ni busara tu ya kawaida. Yaani ulikuwa waziri mkuu na ulinzi mkali then baadae unaanza kupishana kwenye ma corridor ya bunge na akina msukuma na tale tale. Kimsingi Majaliwa hekima imemwongoza atulie ale pension yake kiulaini.

Hongera majaliwa.
 
Wewe ni mjinga yaani hao mbulula haters wa SSH ndio unawasikiliza?
Ujinga wangu uko wapi? Mimi naheshimu mawazo ya wote, naweza kua nampenda Samia BUT siwezi kuwaona wengine kua wajinga wasiomkubali. Wewe ndio utakua mjinga endapo unadhani chaguo lako ni chaguo la wote, that's more than stupidity. Tunao mpenda Samia tunazo sababu zetu but na wasiompenda nao wanazo sababi zao na ndio demokrasia
 
Syndicate imemuamrisha, ole wako uchukue form.
Kitakachokupata hutosimulia.
 
Wazaliwa wa ruangwa aha ha aha aha 😅 😆 huko arusha mnajisikiaje?
 
Bado lukuvi sasa nae atoke aache watanganyika wengine waitafune keki ya taifa kha!!! Akachukue fomu ya urais.
 
Mh! Bungeni wakati wa kufunga nagombea, baada ya wiki moja sigombei. Watanzania kaeni mguu sawa Kuna kitu kinakuja kama mzimu
 
Hili jamaa silikubali kwa sababu ya uongo wake, juzi bungeni ooh nagombea leo sigombei, mtu muongo kama huyu hafai hata ubalozi wa nyumba kumi.
 
Hili jamaa silikubali kwa sababu ya uongo wake, juzi bungeni ooh nagombea leo sigombei, mtu muongo kama huyu hafai hata ubalozi wa nyumba kumi.
Kwenye siasa za uchaguzi, huo huwa hauitwi uongo bali ni kubadili msimamo kulingana na upepo wa kisiasa unavyovuma...

Inawezekana kaiona option nyingine mpya kabisa ya kufikia malengo yake ya kisiasa na hivyo kufuta maamuzi ya awali..

Kumbukeni huyu sio Steven Wassira mwenye umri wa miaka 80 au Mkuchika aliye over 70+...

Huyu ni Kassim Majaliwa Kassim, he's just 64 years old...

Hagombei ubunge tu, lakini yumo, mtamuona tu...
 
Huyu si alitangazia umma kuwa anagombea tena.

Shikamoo CCM, nyie ni mabingwa wa siasa. Najua hii ni approach ya kwenda namba moja.

Wale wazee waliosomeshwa Cuba bado wapi kumbe.

Afu kuna watu wanailaumu TISS. Hawa jamaa wanajua nini kinafanyika
 
Au anaenda kwenye chama?..maana SG post punde tu utakuwa wazi..nawaza tu kwa sauti
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hatagombea tena ubunge katika eneo la Ruangwa kwenye uchaguzi unaofanyika Oktoba 2025.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi eneo la Ruangwa Abbas Makwetta alitangaza hilo katika mchakato wa uteuzi unaoendelea.

‘’Mheshimiwa Majaaliwa amekuja leo na kutangaza kuwa hatagombea ubunge tena,’’ Bwana Makwetta alisema.

Majaaliwa, anatamatisha miaka 15 ya kuhudumu kama mbunge tangu alipochaguliwa na wananchi kwa mara ya kwanza 2010.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za CCM umekamilika leo saa kumi jioni.
 
Ameondoshwa kwa Aibu sana!!
Kwanini waswahili mko hivi jamani?!
Si angeambiwa tu mapema hatakiwi ili aage kwa heshima?!
Ona sasa ame frustrate Hadi nywele kashindwa kuchana!
Hajui hata anachoongea!
Pole sana Majaliwa ,nitakukumbuka jinsi ulivyojaribu kuwa chawa ! Kila wakati ukuisha kutamka "Dakta"!
Ona sasa heshima imeshuka Hadi negative!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…