Kataa ndoa. Leo wamepata point 3 ugenini, ilikuwa hivi...

Kataa ndoa. Leo wamepata point 3 ugenini, ilikuwa hivi...

Nina mwanamke mwaka wa saba huu nakaa nae na sijamuoa, kila mtu anaenijua physically anajua ni mke wangu. Kuna kipindi alileta kelele lkn akaja kugundua mimi ni mafia, ametulia anakula ugali na samaki.
Mimi nilimwambia sihitaji ndoa ya Makaratasi ndoa ni Mapenzi Moyoni hata Bibilia haijasema tuandikishane makaratasi.

Mpaka sasa tumetulia nyumbani kwa amani na Utulivu sana
 
Mambo mengine yanahitaji kufanyiwa ''update'' kila baada ya muda ili kuenda na wakati, sheria za ndoa ni mojawapo.

Imefika muda, sheria za ndoa za Tanzania zifanyiwe maboresho haraka sana, ili kuwe na uwezekano wa kufunga ndoa zenye makubaliano maalum kulingana na wanandoa wanavyokubaliana.

Kwa mfano wanaweza kukubaliana kuwa wakiwa kwenye ndoa kila mtu atachuma na atamiliki mali zake na ikitokea kuna kutengana, kila mmoja anaondoka na ''mbao zake''.
Hahaha sasa hiyo ndoa gani inaanza na vita?
 
MMH Topic kuntu hii.

Kwanza kabisa ni kweli kuna wapigaji wa kike siku hizi. Akishakuona unajiweza anatumia/anakutumia kama fursa hapa mjini, hasa hasa wanaume ambao mpaka wanajipata (wanakuwa na mali) wanakuwa hawajui mstakabali wa mahusiano yao.
Wengine unakuta walikuwa na wenza wao wakati wanazitafuta, kisha wakizipata utaona wanaanza kuwaona wale wenza wao ni kama vinyago hivi, nafikiri hii pia huleta mzunguko wa kisasi cha maisha hata kwa mpenzi mpya anaempata, nae huyo mwanamke akimfanyia unyama huyo mwanaume, nae kwa namna moja au nyingine, huenda kupigwa na anaefata. Hivyo cheini ya visasi inaendelea, Si unajua wanasema malipo hapa hapa duniani.
HIVYO USHAURI WANGU WA KWANZA TULIA NA YULE ULIECHUMA NAE, NA KAMA MUDA HUU BADO HAUJAJIPATA TAFYTA WA KUCHUMA NAE, ILI UZIBE MIANYA YA WAPIGAJI (WADANGAJI) SIKU UTAKAYOPATA.

Cha pili ni pale unapokuwa umejipata sasa huwa kwa mwanaume kunakuwa na uzuzu wa mtu kusahau kuwa wezi wa mali na majambazi wa siku hizi hawashiki bunduki wa mapanga, unaibiwa kwa ushawishi ni wewe tuu ndio hudanganywa unajikuta unatoa mali yako kirahisi kabisa. Wengine wapo tayari hadi wakuzalie ili tuu apate hizo hela za matumizi ya mtoto. Wengine wapo tayari kuelewa hata na wasikuwa na mapenzi dhidi yao ili tuu wapate unafuu wa maisha. DUNIA IMEBADILIKA SASA HIVI. Hivyo vijana inabidi tubadilike kimtazamo siku hizi, kuna namna mbali mbali za kutanza mali zako zisipigwe na hao wezi, tena njia ni za kisheria kabisa na hata akupeleke mahakama gani hatoboi. HAWA WANAWAKE TUMEAMBIWA TUISHI NAO KIAKIRI. Hivyo ukiona mtu wako humuelewi, wakati unatafuta hajali yeye anasubiri wakati wa kupokea hela tuu mzee. Weka hela zako kwenye Corporation au Fungua kampuni ya Familia yako (yaani wewe na mama yako au baba yako) kisha mtaji weka huko. Siku ya kugawana hizo mali hazitahesabiwa. Acheni ulevi wa kutafuta mali halafu unaandika majina ya wanawake zenu, demu mwenyewe ulikutana nae kidimbwi.

ILA HAPA SISEMI KAMA WANAWAKE WOTE WAPO HIVO WENGINE NI WEMA TUU TENA HULETA BARAKA KWAKO ZAIDI NA HULETA MBINU ZA UTAFUTAJI UKAPATA ZAIDI. NA WENYWE HUA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA WEW UNAFANIKIWA HAO NDIO UNATAKIWA USHIKILIE. ACHANA NA WADANGAJI.

Njia ambazo nazijua za kulinda mali zako dhidi ya wanawake wapigaji.
1. Mali andika jina la watu wengine (mfano mama au baba)
2. Weka mkataba wa ndoa (hapa ni kama wakati unajipata ndo umekuja kupata mdangaji)kuwa mali zako alizokukuta nazo hatazigusa endapo mtaachana.
3. Fungua kampuni ya familia yako (yaani ya baba yako au na ya mama yako) kisha weka mtaji wako weka huko. Maana mahakama hawatahusisha mali za kampuni kwenye mgao.
4. Kama kuna njia nyingine wengine wataongezea.

Napita hivo
Akumbukwe shujaa Ashraf Hakim.
 
Msioe msioe msioe. Kwani nini kigumu kukaa na mwanamke ndani bila kumuoa? Kama utalazimika kuoa mpe mwanamke prenup asije kugusa mali zako
Haya ndio maisha ambayo mm nimeyachagua. Hakuna anayeweza kubadili mindset yangu, hata ndugu wameshindwa, najaribu sana kuepuka huo utumwa kwa badae
 
😂😂😂 kaa kwenu, nikae kwetu. Ila sio kama hivyo ulivyosema. Utamaduni wa kitanzania hauruhusu,,
Unaongea tu wewe, ukimpenda mwanaume utakubali kuishi nae kiroho safi tu. Na anagonga ngozi miaka dahari tu mpaka atapojiskia kuja kwenu. Huwezi force ndoa kwa style hio utazeekea kwenu tu.
 
Nina mwanamke mwaka wa saba huu nakaa nae na sijamuoa, kila mtu anaenijua physically anajua ni mke wangu. Kuna kipindi alileta kelele lkn akaja kugundua mimi ni mafia, ametulia anakula ugali na samaki.
Naijua hio, hata mimi nimeishi na huo mfumo for 6 years.. Mwanamke akikupenda anatulia zake tu.
 
Matatizo mnajitakia wenyewe. Unatumia fedha kumshawishi mwanamke akupende ili umuoe! Hii inaonyesha kabisa jamaa yako alitumia ''misuli'' ya fedha ili kumvuta huyo demu.

Na mara nyingi unakuta ni hawa ''wenzangu'' na mimi wenye elimu ndogo na pengine washamba na ulimbukeni hapo hapo, wanapofanya biashara na kupata fedha za ghafla wanakimbilia kuoa wanawake ''wavaa vimini'' ili nao waonekane ni wajanja.
Kosa kubwa kinoma yani
 
Kuoa oa ila usifanyie uchaguzi instagram. Trust me. Bado kuna wanawake wenye adabu sana. Nimekumbuka mjomba wangu siku moja alinichekesha kweli kweli. Alimpata mke wake alipokuwa chuo cha ualimu enzi hizo, basi akawa ananimbia kuwa yeye akiwa mwaka wa tatu, walikuja wanachuo wa mwaka wa kwanza. Akasema akafanya uchunguzi na kuchagua mmoja aliyekuwa mshamba mshamba hivi hata kuvaa hajui kupangilia. Fast foward, huyo mke wako naye mpaka sasa hivi na wana wajukuu na maisha yao yamekuwa mazuri sana.
Mjomba Six kumbe alikuwa mjanja toka akiwa chuo. Dawa ni kuchagua mwanamke ambaye mnaendana malezi yenu. Huyo ndio anaweza kufaa kuishi nae. Ila ukikurupukia mwanamke ilimradi mrembo sana jua disaster ni jambo haliepukiki.
 
Sure.

Akimkosa kote ataenda kumkamatia kwenye ahadi ya ndoa. Hapo ndio ataona dunia haina huruma.

Tunajitahidi sana kutaka kuzuia mali zetu zisiwe mali za ndoa ila ni swala gumu sana.

Mnaweza mkaandikishiana kutenga mali za ndoa na mali binafsi ila baadae Mahakama ikasema hoyo makubaliano hayakuwa na nia njema. Ikayafutilia mbali, mkagawana mali zote zilizopo.

Ni swala tu la mtu kuwa na wakili smart atakayeisaidia Mahakama kuona namna gani wanandoa hao waliingia makubaliano wakiwa na ajenda za siri. So hakukuwa na taarifa sahihi kwa pande zote.

Ni bora tu mtu ukaamua kukaa kimya na kustawisha ndoa yenu bila kuibua ghasia hadi kifo kiwatenganishe.
Mwanamke wa kibongo akiwa kwenye zone ya uhawara au uchumba huwa anakuwa on her best behaviours akitarajia ndoa. Its time to make the most of it ukiwa nae. Siku ukishamuidhinisha kwa makaratasi tu ndio mambo ya ajabu ajabu yanaanza kuchipukia. Utapangiwa muda wa kurudi home, ratiba za kugonga zinaanza na migogoro kibao.
 
Nami naomba nichangie jinsi ndoa ilivyomtoa kwenye reli rafiki yangu wa karibu nimuite bro.
Ni wa kitaa, nazionq hustle zake from scratch. Akapata kazi ya maana. Akaoa. Shem mpole tu kwakweli tena mama wa nyumbani.
Myaka ikakatika wakapata one kid maisha yakasonga akajitafuta akamalizia mjengo wake wakahamia na ndio balaa lilipoanzia.
Mume akitoka shem anampigia mpenzi wake wanakuja kufanya yao ndani ya nyumba, majirani wakamtonya bro. Akaweka mtego haukunasa koz alichelewa kurudi akakosa ushahidi eye witness koz jamaa alikua ashasepa.
Akaamua amrudishe shem kwao akajisikilizie (mistake).
Mwanamke akaenda ustawi kuwa katekelezwa na bro na mtoto .
Bro alikamatwa aliwekwa lockup sababu shem alistate mambo mengi ikiwamo kutishiwa uhai.
Kesi ilifunguliwa wakati bro yuko busy na kufollow up mambo ya kesi na upatanisho kazini walimtema!
Nyumba iliamriwa iuzwe wagawane.
Bro alirudi tena to scratch.
Maisha yamemnyoosha. Mentali hayuko sawa tena! Kazi imekua ngumu kupata. Anaishi kwa kujihifadhi kwa pagale.
Shem yupo town anaishi na ile njemba gawio lilimpush akaanza na biashara.
 
Nami naomba nichangie jinsi ndoa ilivyomtoa kwenye reli rafiki yangu wa karibu nimuite bro.
Ni wa kitaa, nazionq hustle zake from scratch. Akapata kazi ya maana. Akaoa. Shem mpole tu kwakweli tena mama wa nyumbani.
Myaka ikakatika wakapata one kid maisha yakasonga akajitafuta akamalizia mjengo wake wakahamia na ndio balaa lilipoanzia.
Mume akitoka shem anampigia mpenzi wake wanakuja kufanya yao ndani ya nyumba, majirani wakamtonya bro. Akaweka mtego haukunasa koz alichelewa kurudi akakosa ushahidi eye witness koz jamaa alikua ashasepa.
Akaamua amrudishe shem kwao akajisikilizie (mistake).
Mwanamke akaenda ustawi kuwa katekelezwa na bro na mtoto .
Bro alikamatwa aliwekwa lockup sababu shem alistate mambo mengi ikiwamo kutishiwa uhai.
Kesi ilifunguliwa wakati bro yuko busy na kufollow up mambo ya kesi na upatanisho kazini walimtema!
Nyumba iliamriwa iuzwe wagawane.
Bro alirudi tena to scratch.
Maisha yamemnyoosha. Mentali hayuko sawa tena! Kazi imekua ngumu kupata. Anaishi kwa kujihifadhi kwa pagale.
Shem yupo town anaishi na ile njemba gawio lilimpush akaanza na biashara.
Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom