Habarini wakuu,
Hivi karibuni kumeibuka mjadala wa baadhi ya wanaume kukataa NDOA, (
dronedrake ) muda huohuo pia kua baadhi ya wanaume wanakimbilia NDOA.
Jambo hili linaibua hisia za wanaume na wanawake wengi pia, na vilevile linapelekea wengine kubaki kwenye kitendawili cha kufuata NDOA au kukataa NDOA. Wenye uzoefu wa NDOA tunaomba msaada wenu wa kwanini mliweza kuikimbilia NDOA. Na wale pia KATAA NDOA, mtueleze pia sababu zipi zinapelekea MKATAE NDOA.
Lengo tushare EXPERIENCE kwa sisi ambao hatujaoa tujue ambayo tusiyoyajua juu ya FAIDA/HASARA za KATAA na KUBALI NDOA.
View attachment 2760726View attachment 2760727
Ndoa ni mkataba na mkataba huwa una malengo mahsusi
Mfano mkataba wa ajira, mwajiri huwa anataka ujuzi/nguvu yako na mwajiriwa huwa anataka pesa
The same kwenye ndoa, mwanaume huwa ana malengo yake (matarajio) na mwanamke huwa ana matarajio yake
Changamoto kubwa ni kwamba kabla hatujaoa au kuolewa huwa tuna matarajio/feeling kubwa na ndoa lakini uhalisia huja kuwa tofauti baada ya kuoa au kuolewa
Mfano, wanaume wengi huoa kwa ajili ya kupata mgegedo, lakini si kweli kuoa ni guarantee ya kupata mgegedo, unaweza ukawa unanyimwa au unapangiwa ratiba nk
Unaweza ukaoa mwanamke ambaye yeye hapendi kugegendwa wewe unapenda Mara kwa Mara
The same Kuna Mambo mengineyo mengi ambayo hutokea kwenye ndoa ambayo husababisha mwanamke au mwanaume kutotamani ndoa
BINAFSI UKINIULIZA KWA NINI WATU WANAKATAA NDOA
Jibu langu ni kwamba, watu wengi wameingia kwenye ndoa wakajikuta wanakosa walichokitegemea (mapenzi, tabia, usaliti, uchumi nk)
Mwisho wa siku watu wengi huwa wanapata mateso kwenye ndoa na kuiona haina thamani, kuvunja ndoa na kutotamani kuoa tena
KATAA NDOA WENGI wamepitia maumivu ya ndoa au uchumba au mahusiano 😂😂
Kumbuka pia Kuna watu wengi wanalazimika kubaki kwenye ndoa kwa kuwa hamna namna, kwa ajili ya kulea watoto, heshima nk
Watu wengi ambao wanakimbilia ndoa ni wale wenye mategemeo makubwa wakioa😂😂 bado hawajapata maumivu au wapo katika ndoa huku wanaenjoy ndoa zao
HITIMISHO
_ Tafuta pesa kwanza, ndoa bila pesa utaishia kuja kulalamika lalamika tu humu JF na kuwa mfuasi mkubwa wa KATAA NDOA
_ Hakikisha mnapendana Sana ndio muoane
_ Kabla ya kuoa fanya tathmini juu ya malengo yako na huyo partner wako, je mtafanikisha malengo yenu?? Mahitaji ya ndoa, uchumi nk
_ Usiweke mategemeo (matarajio) makubwa sana kwa mke /mume wako 😂😂😂
_ Kuwa tayari kukabiliana na changamoto za ndoa, kila mtu huwa anaface changamoto zake (hapa ndio pagumu)
NAOMBA KUWASILISHA