Katavi: RC Mwanamvua Mrindoko awataka walimu kuwapo shuleni saa 24

Katavi: RC Mwanamvua Mrindoko awataka walimu kuwapo shuleni saa 24

Huyo Mzazi anayepeleka mtoto kumuandikisha uski wa manane atakuwa ana matatizo....


Huyu angesema tu uwepo muda wa kazi wa kutosha au watu kufanya overtime ili kuhakikisha watu wanapata huduma haya mambo ya 24/7 hata serikali tunayoigharamikia haifanyi hivyo (ukichelewa sekunde tu) unaambiwa muda wa kazi umekwisha wengine jmosi nusu siku (labda angewashauri wenzake waanzia kwanza huko)

By the way yeye anafanya kazi masaa mangapi au ofisi yake ipo wazi masaa mangapi ?
 
"Think before you do" Dr.Alban
1.kuna ulinzi huko shule?
2.Kuna posho?
3. Hivi kweli kuna wazazi watakao kwenda kuwa andikisha watoto wao usiku wa manane??????
4. Au majani ya chai ya huko ni makali sana kiasi chai haikoi sukari????
 
Huyu ni mke wa yule mrindoko mpiga dili nene nene enzi za JK? Somebody Bashiru Mrindoko?
 
Kuna viongozi wa serikali huwa wanatamani watoe matamko ya kuua watu wote ili wabaki wao wenyewe,nadhani huyu bado Yuko usingizini,zama za matamko zilishapitwa na muda,unless nijitolee au walau angewaomba,unatamka watu wafanye 24 hrs kwa Sheria ipi?

Mimi huku niligombana na mkuu wangu wa shule kwa kunilazimisha nifundishe muda wa saa 10-12 jioni eti Ni tamko la mkoa,huu upuuzi siwezi ,Ila yataka moyo ,maaana tangu hapo sijawahi kwenda kusimamia mitihani Wala hata kuitwa halmashauri .

Watu Hawa wanapenda kujichukulia point hata nje ya utaratibu,muda wa kazi Ni saa 8 sasa huyu 24 hrs kazitoa wapi?

Siwezi fanya huu upuuzi,nadhani kama mungu atanisaidia kwa miaka ijayo niachane na ualimu,huku upuuzi umejaa,ukiwa mtu wa kufuata utaratibu utaishia kugombana na wakuu wako wa idara maana ni miungu watu kweli kweli.

Kwa tamko la RC siwezi hata kupoteza muda wa kulitafakari,maana ni upuuzi mtupu

Ninachompendea Rais wetu wa sasa anafuata Sana utawala wa sheria,Mungu ambariki,utawala wa sheria huondoa manung'uniko na migongano ya Mara kwa Mara!!

Hl
 
Kuna watu Hadi unajiuliza mara 2 wanaishi vipi mbona akili ndogo tu hawana. Unaweza Fanya Kasi 24hrz

Kwamba kuna mzazi atakuja andikisha mtoto saa 8 usiku

Anzia mkuu wa mkoa na wakuu wake wa wilaya katavi wapuuzi watupu tangu aondoke homera mkoa haueleweki
 
Ndg waandishi penye utata, muwe mnawahoji vzr kabl ya kukimbia kwenye keyboard na hivyo vikamera na Vitape recorder vyenu.
Nao ni binadam ukizingatia public speech zina changamoto nying kw wengi, nao ni binadam,
Hii ni sahihi,wanahabar wamepoteza ubunifu badala yake wanatafuts chochote tu hata Cha makosa y kibinadamu wanakomaa nacho mfano suala la yesu na ndugai,hii inajulikana kabisa haiwezekani kufanya kazi masaa 24 kwa walimu
 
Kama mshahara utakuwa mkubwa na posho juu ya muda wa ziada hapo sawa, kama mshahara ni huo huo ya nini kujichosha mpaka usiku?
 
Masaa 24 wakiwa shuleni genye zao atawatoa nani na muda upi?
Awe serious na matamko yake japokuwa tunajua analinda kibarua chake.
 
Back
Top Bottom