Kuna viongozi wa serikali huwa wanatamani watoe matamko ya kuua watu wote ili wabaki wao wenyewe,nadhani huyu bado Yuko usingizini,zama za matamko zilishapitwa na muda,unless nijitolee au walau angewaomba,unatamka watu wafanye 24 hrs kwa Sheria ipi?
Mimi huku niligombana na mkuu wangu wa shule kwa kunilazimisha nifundishe muda wa saa 10-12 jioni eti Ni tamko la mkoa,huu upuuzi siwezi ,Ila yataka moyo ,maaana tangu hapo sijawahi kwenda kusimamia mitihani Wala hata kuitwa halmashauri .
Watu Hawa wanapenda kujichukulia point hata nje ya utaratibu,muda wa kazi Ni saa 8 sasa huyu 24 hrs kazitoa wapi?
Siwezi fanya huu upuuzi,nadhani kama mungu atanisaidia kwa miaka ijayo niachane na ualimu,huku upuuzi umejaa,ukiwa mtu wa kufuata utaratibu utaishia kugombana na wakuu wako wa idara maana ni miungu watu kweli kweli.
Kwa tamko la RC siwezi hata kupoteza muda wa kulitafakari,maana ni upuuzi mtupu
Ninachompendea Rais wetu wa sasa anafuata Sana utawala wa sheria,Mungu ambariki,utawala wa sheria huondoa manung'uniko na migongano ya Mara kwa Mara!!
Hl