Pre GE2025 KATAVI: Wajumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA Taifa watangaza kumuunga mkono Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hadi leo najiuliza, kwanini Mbowe amejitakia aibu hii? Kwanini asingestaafu kwa heshima?
Na akileta uhuni katika sanduku la kura ndio ataiua CDM kabisa!

Heshima kwenu wajumbe wa Katavi na wote mnaomuunga Lissu mkono, mabadiliko ni sasa.
Shida moja mbowe anakitumia siasa kama sehemu ya platform kwenye mambo yake hata hizo biashara zake, muda utasema.Huwezi kung'ang'ana miaka 20+ bure tu kwenye siasa.
 
Ndo maana Jana mbowe analalamikia tu kuona lissu anagombea uwenyekiti badala ya umakamu mwenyekiti
 
Imekuwaje Mbowe ameshindwa kusoma alama za nyakati?
Tatizo Mbowe na wapambe wake wachache walitaka kupindua meza kibabe Kwa kuwaondoa kwenye nafasi zao Msigwa,Lema,Heche na Lissu ili wapate maingizo mapya watakao kuwa machawa kama SUGU na WENJE...Lissu chap kwa haraka akamoandilia huko huko juu basi imekuwa taflani Kwa sababu Mbowe na machawa wake hawakutegemea hii manoeuvre ya Lissu...Vyoyote itakayokua chadema watahitaji maridhiano ikiwa dhamila ya kuendelea kubaki ndani ya chama wote wanayo
 
Nilisema juzi hapa jf na naludia kama umekula pesa za upande ule na upo chadema jiandae kuzitapika
 
Usiwaa.ini sana wanadamu.
Mbowe jana ameongea akiwa amejaa sumu kali, najua atatembeza sana pesa na fitina
 
Wanachadema wengi hawapigi Kura...Ukiwa mjinga unaweza kuficha uso na kuacha makalio wazi
Nashangaa kampeni ya timu Lisu ohhh Mbowe kakaa muda mrefu sana

Chama tawala ambacho mimi pia ni mwanachama wake kazi yake kusimamia katiba ya nchi na vyama vyote vya siasa kuzingatia katiba zao

Chama tawala hakitawali nchi tu bali kinatawala na vyama vyote vya siasa kuhakikisha vina zingatia katiba zao ikiwemo Chadema
Team Lisu wanataka kuvunja katiba ya Chadema kwa hoja ooh Mbowe kakaa sana mimi kama CCM nasimama na mbowe kumtetea katiba ya Chadema inamruhusu kugombea
Katiba ya Chadema iheshimiwe Lisu na timu Lisu mnaotaka katiba ipindishwe Mbowe asigombee Lisu apate ushinde wa mezani go to hell

Katiba ya Chadema izingatiwe
 
Hali ni mbaya kwa bwana Mbowe hiyo ni Kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…