Katazo la shule kutoendelea na masomo wakati wa likizo ni la kitoto sana. Pia likizo ndefu moja ifutwe

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Pongezi kwa shule zote zinazobakiza watoto kusoma wakati wa likizo. Kama nchi tunatakiwa kufurahia watoto wakisoma sana, wasome kadri wanavyoweza.

Tangazo la kuzuia watoto kubaki shuleni kusoma wakati wa likizo lina lengo gani hasa? Maana ukiangalia siku wanazosoma watoto wa Tanzania kwa mwaka ni chache sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea.

Kwa nchi yetu ilivyo tulitakiwa kuongeza siku kama arobaini zingine kwenye mwaka wa masomo. Kuna faida nyingi sana za kusoma kwa siku nyingi.

Mwalimu hawi na mchecheto wa kumaliza silabasi na anafundisha kwa kasi ambayo hata wale watoto ambao ni wazito kuelewa wanapata muda mrefu wa kujifunza na kuelewa.

Kukataza hilo ni la kitoto na tufute likizo moja ndefu ili tuongeze siku za kusoma.
 
Maskini mwalim hapo umekaa gheto radio huna TV huna na ulizoea kushinda shule, kula msosi wa wanafunzi wewe gheto nikulala tu haya sasa vimeumana jiko huna sufuria huna pesa ulishia kushona mashati ya vitenge na suruali na kununua viatu vizuri vizuri na kuangalia TV bar haya nenda bar sasa Acha watoto wapumzike
 
Wamasoma nini? Niambie maprofesa wa Kagera wanasaidiaje jamii zao kuondokana na umasikini? Mbona kagera ni mkoa wa kwanza kwa kuwa na wasomi lakini ni mkoa wa mwisho kwa umasikini? Acha watoto wapumzike wapeleke mbugani waone wanyama live na utajiri wa nchi yetu sio kuwajaza vitabu visivyo na faida. Muda wa likizo uheshimiwe wengine hamtaki likizo mnaogopa kukaa na watoto wenu/manakwepa malezi.
 
Nafikiri huu Ujinga wa kutoruhusu watoto kupumzika wakati wa Likizo uko hapa hapa Tanzania!
Watoto wa Tz "Wanapumzika" kupita kiasi. Watoto wanasoma kama siku 180+ kwa mwaka. Wakati nchi kama za mashariki watoto wanaenda hadi siku 220 na zaidi kwa mwaka.
 
Tatizo nahisi ni kukosa uelewa kuwa kama ilivyo kusoma basi ni kupumzika ni muhimu vile vile.
Watoto wa tz wanapumzika sana. Wanasoma siku chache sana kwa mwaka ukilinganisha na nchi zilizotuacha mbali kiuchumi.
 
Maskini mwalim hapo umekaa gheto radio huna TV huna na ulizoea kushinda shule, kula msosi wa wanafunzi wewe gheto nikulala tu haya sasa vimeumana jiko huna sufuria huna pesa ulishia kushona mashati ya vitenge na suruali na kununua viatu vizuri vizuri na kuangalia TV bar haya nenda bar sasa Acha watoto wapumzike
Wewe huna akili unadhani Mwalimu ana mshahara ni mdogo ?? Kwa taarifa Mwalimu ana mshahara mzuri Sana kama hutaki acha
 
Watoto wa Tz "Wanapumzika" kupita kiasi. Watoto wanasoma kama siku 180+ kwa mwaka. Wakati nchi kama za mashariki watoto wanaenda hadi siku 220 na zaidi kwa mwaka.
Ni kweli uyasemayo mkuu ila hizo siku 180 kwa watoto wa Tz huenda ni mara mbili ya hizo siku 220, mana mtoto anaamka saa 11 alfajiri anajiandaa kabla ya saa 12 aabh anatakiwa shule, anakaa huko mpk saa 12 jioni ndio wanaachiwa, sasa tena likizo wanatakiwa waende shule kwa utaratibu ule ule, na labda nikuambie ndugu lengo kuu hapo ni pesa, mtoto kwenye hiyo likizo amatakiwa abebe hela kwa ajili ya tuition. Ufaulu lazima ushuke kwa mtindo huo.
 
Pongezi kwa shule zote zinazobakiza watoto kusoma wakati wa likizo. Kama nchi tunatakiwa kufurahia watoto wakisoma sana, wasome kadri wanavyoweza. Tangazo la kuzuia watoto kubaki shuleni kusoma wakati wa likizo lina lengo gani hasa? Maana ukiangalia siku wanazosoma watoto wa Tanzania kwa mwaka ni chache sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea.
Kwa nchi yetu ilivyo tulitakiwa kuongeza siku kama arobaini zingine kwenye mwaka wa masomo. Kuna faida nyingi sana za kusoma kwa siku nyingi. Mwalimu hawi na mchecheto wa kumaliza silabasi na anafundisha kwa kasi ambayo hata wale watoto ambao ni wazito kuelewa wanapata muda mrefu wa kujifunza na kuelewa.

Kukataza hilo ni la kitoto na tufute likizo moja ndefu ili tuongeze siku za kusoma.
Wewe ni mbumbumbuu usielewa umuhimu wa likizo, pumbavu kabisa!
 
Maskini mwalim hapo umekaa gheto radio huna TV huna na ulizoea kushinda shule, kula msosi wa wanafunzi wewe gheto nikulala tu haya sasa vimeumana jiko huna sufuria huna pesa ulishia kushona mashati ya vitenge na suruali na kununua viatu vizuri vizuri na kuangalia TV bar haya nenda bar sasa Acha watoto wapumzike
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pongezi kwa shule zote zinazobakiza watoto kusoma wakati wa likizo. Kama nchi tunatakiwa kufurahia watoto wakisoma sana, wasome kadri wanavyoweza. Tangazo la kuzuia watoto kubaki shuleni kusoma wakati wa likizo lina lengo gani hasa? Maana ukiangalia siku wanazosoma watoto wa Tanzania kwa mwaka ni chache sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea.
Kwa nchi yetu ilivyo tulitakiwa kuongeza siku kama arobaini zingine kwenye mwaka wa masomo. Kuna faida nyingi sana za kusoma kwa siku nyingi. Mwalimu hawi na mchecheto wa kumaliza silabasi na anafundisha kwa kasi ambayo hata wale watoto ambao ni wazito kuelewa wanapata muda mrefu wa kujifunza na kuelewa.

Kukataza hilo ni la kitoto na tufute likizo moja ndefu ili tuongeze siku za kusoma.
Mkuu,

Nakupinga katika hili. Kila kitu kina wakati wake.
Wanafunzi lazima wapate muda wa kupumzika, wapate muda pia wa kukaa na wazazi wao, likizo ya siku 60 hadi 74 kwa mwaka wenye siku 365 unaona kama ni vibaya?

Mimi nikadhani hata tuongeze muda wa likizo.

Psychology ya wanafunzi tutaiharibu.
Tuwaache wapumzikee
 
Back
Top Bottom