Ndugu sikubaliani nawe, naomba ufanye uchunguzi zaidi.
Nikupe taarifa:-
1. Education (learning) and schooling are two different things.
2. Kusoma muda mrefu au kuwa na vipindi vingi au masomo mengi au kukaa shule muda mrefu SIO ELIMU.
3. Kupumzika na kucheza kwa mwanafunzi ni muhimu kama ilivyo kusoma.
Likizo ni muhimu kwa wanafunzi na walimu pia.
4. Mitihani sio kigezo cha kupima Elimu wala ubora wa elimu. Kwa sasa watoto wanafundishwa kukariri na kujibu mitihani; hawapewi elimu wala kujenga ubunifu, maarifa na nidhamu.
5. Tanzania ni moja ya nchi zenye masomo mengi, vipindi vingi, mitihani mingi na kiwango cha chini cha elimu.
Kuna Rasimu Mpya ya Mitaala ya elimu itakayoanza mwakani, hiyo itajaribu kupunguza baadhi ya hizi kero.
Utafute huo mtaala uupitie zaidi.