Kathrin Steinbrenner, Naibu Balozi wa Ujerumani kamwambia Mbowe ‘Never Give Up’

Kathrin Steinbrenner, Naibu Balozi wa Ujerumani kamwambia Mbowe ‘Never Give Up’

Kesi hii ya Mbowe, Tanzania imejidhirisha kuwa tunahitaji Katiba mpya, Katiba ya sasa ni mbovu imejaa viraka kiasi ambalo viraka vinakanyagwa, sheria hazifuatwi. Mihimili ya Dola imekamatana, hii mihimili lazima itenguliwe, mahakama, Usalama, Bunge na office ya Rais .

Au watanzania tutaendelea kupotea kama komandoo
 
Kwa nini Magaidi ya kiarabu uko USA wazungu hawakwenda kutoa hizo statement never give up . Huyo barozi mjinga sana. Magaidi wanaowakamata uko kwao barozi zetu au nchi nyingine walishaenda kuwaona hao Magaidi na kuwambia never give up.

..sasa hivi usa kuna kesi ya khalid sheikh mohammed mastermind wa shambulizi la 9/11. Balozi wetu marekani anaweza kuhudhuria kesi hiyo na hata kumtia moyo bwana khalid.
 
Mbowe angekuwa ni mtu wa ku'give up', angekuwa ameshafanya hivyo siku nyingi sana wakati akipata dhoruba, huku waTanzania wengi wakionekana kama anayopigania yeye na chama chake hayawahusu kabisa wao.

Kinondoni risasi zinalengwa kuelekezwa kwake na wenzake na kuwaondoa kwa bahati mbaya(?) akina Akwilina; na kutungiwa kesi iliyowaweka jela, bado haku'give-up'.

Wabunge wananunuliwa, hadi Makatibu wakuu wa chama wanakisaliti chama, bado haku'give-up'

Itakuwaje leo, wakati ambapo waTanzania wameweza kuelewa matatizo ya nchi yao yapo wapi ndipo aanze ku'give-up'?

Kilichobaki mbele yake ni kujua njia za kuwaongoza waTanzania kupigania HAKI zao ili waondokane na manyanyaso ya watu waliojigeuza kuwa wenye haki zaidi ya wengine. Watu wanaokiuka sheria wakati wowote bila hofu ya kuhojiwa na mtu yeyote. Watu walioamua kuvitumia vyombo vya kulinda haki za wananchi na kuvifanya viwe vya ukandamizaji wao.

Mbowe hawezi na wala hatakiwi ku'give-up' wakati mapambano ndiyo kwanza yameanza.

Kushindwa kwa CCM kumwondoa Mbowe katika uongozi wa CHADEMA ili isambaratike kirahisi kunaonekana dhahiri sasa hivi ikiwa ni pamoja na kioja hiki cha kesi ya kutunga.
Wananchi sasa wameelewa kinachoendelea. Mbowe hawezi ku'give-up' sasa wakati juhudi zake na wenzie zinapoanza kuonyesha matumaini.
 
Mambo ya aibu😁😁😁

MoGJh.jpg
 
Hii kesi tunaelewa kuwa FREEMAN MBOWE atafungwa kwa maelekezo ya Bibi wa shungi,lakini tumtia moyo ndugu yetu MBOWE kuwa kwa muda wowote atakaokaa gerezani Ni Imani yetu kuwa Siku moja atatoka,wetesi wake watakuwa bado wapo duniani ,kwa aina yoyote ile ya uwepo wao hapa duniani hatuta walipiza kisasi.Mbowe hakika umekuwa mbuzi wa sadaka na kafara ili kuuzima Moto wa KATIBA MPYA, tunakuombea Sana huko uliko BWANA MUNGU AKIPENDA hakika utatoka salaama Kama ulivyoingia.
 
Kwa nini Magaidi ya kiarabu uko USA wazungu hawakwenda kutoa hizo statement never give up . Huyo barozi mjinga sana. Magaidi wanaowakamata uko kwao barozi zetu au nchi nyingine walishaenda kuwaona hao Magaidi na kuwambia never give up.
Ni maoni yangu tu...."Unahitajika kupata khabari za uhakika mara kwa mara kuhusu hao waarabu magaidi huko kwa Mabeberu."
 
..sasa hivi usa kuna kesi ya khalid sheikh mohammed mastermind wa shambulizi la 9/11. Balozi wetu marekani anaweza kuhudhuria kesi hiyo na hata kumtia moyo bwana khalid.
Atafukuzwa US kwa kukiuka diplomatic code. Nasubiri kuona kama huyo balozi wa Ujerumani atachukuliwa hatua na serikali hata kwa kuitwa na kulalamikiwa tu.
 
Mkuu "Behaviourist" with due respect, kuvunjana mbavu asubuhi asubuhi siyo vizuri! Kilangila.
 
Naibu Balozi wa Germany nchini Tanzania KATHRIN STEINBRENNER akamsogelea Freeman Mbowe na kumueleza "never, never, never Give up!" Freeman akasema "I will never give up". ikapigwa ngeli ya kutosha hapo. MaCCM wanalalamika koridoni, wanasema Germans wanasapoti ugaidi wa FREEMAN.
View attachment 1959863
Mama anatupeleka pabaya taratibu.
 
Back
Top Bottom