Yohimbe bark
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 2,160
- 5,728
Kweli mkuu mwenyewe nilishangaa kuwaona mamba ziwani.Ziwa victoria la miaka ya hivi karibuni siyo lile la miaka ya 60 hadi 70 ambapo vijana walikuwa wanaweza kuogelea karibu siku yote. Miaka ya themanini ziwa lilianza kuharibika kwa uoto fulani likawa halifai kwa kuogelea tena na maji yake yakawa machafu kwa matumizi ya binadamu. Kuanzia miaka ya tisini mamba wakazagaa sana ziwani kutokana na serikali ya Uganda kuharibu makazi yao huko mto Nile wakahamia ziwani na kusambaa Afrika ya Mashariki yote. Kuna haja ya kuwadhibiti wasiendelee kuzaliana. Makazi ya asili ya Mamba huwa ni mitoni siyo ziwani.