Kati ya dagaa na mlenda, Mboga gani unapendelea kula na ugali?

Kati ya dagaa na mlenda, Mboga gani unapendelea kula na ugali?

Nilikuwa Singida Pale Stendi Nikapiga Ugali Dona Na Mlenda Safi
 
Dagaa zina protein, huo mlenda unakipi cha kuupa mwili?

Napenda mlenda, japo nakula kwa hamu

Dagaa hutakiwi kukosa kwenye mlo wako kutokana na umuhimu wake kwenye mwili, hata na wali ni nzuri kula

Kwasisi tulioishi Pwani, hupenda dagaa za kuungwa nazi
 
Ili ugali upande na unoge unahitaji visindikizaji yaani mboga, kwa upande wangu mie napenda sana ugali na dagaa ukiwepo na mlenda naweza kula ugali kwa raha sana.

Kama kuna mlenda napenda dagaa wakavu au wapikwe rosti changanya nyanya chungu na bamia yaani wee acha tu.

Wakuu, wewe ugali unapenda kula na mboga gani?

Ukweli Mimi nakula sana mlenda na nnaupenda ila dagaa nkimsikia hata harufu, au mtu atumie pawa Moja kupakulia dagaa na mboga nyengine basi nikila nntatapika na tumbo kuniuma kabisa.
Lakini mlenda Huwa nakunywa kabisa.
 
Back
Top Bottom