Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

DED mkubwa japokuwa sio bosi wa DAS, Ila ni mkubwa kwa kuwa pale wilayani DED hana bosi wake Ila yeye ndo top, Ila DAS pale wilayani ana bosi wake ambaye ni DC.
 
Mbona shughuli zao nyakati hizi wala hazionekani. Kipindi cha Nyuma nadhani kuanzia miaka ya tisini kurudi nyuma, ukisikia Katibu Tarafa anakuja kijijini ujue ni 'kimuemue'!!
Kwakweli hawana kazi ya kueleweka kwani Maafisa Watendaji wa kata wanatosha. Unajua kipindi kile cha chama kimoja maagizo au utekelezaji ulikuwa unapitia kW DC. Sasa hivi unapitia kwa DED anashusha kwa WEO na Village Executive Officers.

Hawa WEOs ni wasomi. Qualification zao ni diploma na baadhi ni degree holders. VEOs ni certificate. Kwa hiyo wanauwezo wa kumudu kazi zao na hawahitaji msaada wa Afisa Tarafa.

Ikumbukwe kuwa Afisa Tarafa anareport kwa DAS na Afisa Mtendaji wa kata (WEO) anaripoti kwa DED. Ila baadhi ya council wanawashirikisha Maafisa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri.
 
DED mkubwa japokuwa sio bosi wa RAS, Ila ni mkubwa kwa kuwa pale wilayani DED hana bosi wake Ila yeye ndo top, Ila RAS pale wilayani ana bosi wake ambaye ni DC.
Mkuu nafikiri unamaanisha DAS. RAS ni Boss wa watumishi wote katika Mkoa including wa mashirika na Taasisi zote za Serikali na za umma.
 
Hakuna wilaya zenye halmashauri mbili, bali wilaya yenye majimbo mawili
 
Wilaya gani ina halmashauri mbili na ded wawili?
 
Rc, RAS zipo chini ya wizara gani? Sio tamisemi? (Tawala za mikoa na serikali za mitaa?)
Niliona Jafo akiagiza Ma RC.

Pia mbona nilishaona RC akimsimamisha ded kwa uchunguzi?
 
DED mkubwa japokuwa sio bosi wa RAS, Ila ni mkubwa kwa kuwa pale wilayani DED hana bosi wake Ila yeye ndo top, Ila RAS pale wilayani ana bosi wake ambaye ni DC.
Dc sio boss wa RAS,
RAS ni mkubwa sana kuliko DC
 
DED na DAS wanapoteuliwa wote kwa pamoja na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara.?
 
Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
Leo umeamua kuja kivingine Moderators wakakugundua!πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kwa nini una obsession sana na issue ya DED na DAS?


DED na DAS wanapoteuliwa wote kwa pamoja na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara.?
 
DAS wa wilaya ya nyamagana na DAS wa wilaya ya ilemela. Tambua halmashauri ya jiji la mwanza iliundwa na wilaya mbili tajwa hapo juu na baraza la madiwani lilikuwa moja, meya mmoja na mkurugenzi mmoja.

Basi hiyo ni special case mkuu WILAYA MBILI kuwa na HALMASHAURI moja, BARAZA LA MADIWANI moja na MKURUGENZI kwa maana ya DED mmoja. Japokua kwenye pointi ya DAS naona bado tupo pamoja kwa maana ya kwamba DAS ni wa wilaya (wilaya moja, DAS mmoja) kama ambavyo idadi ya wilaya mbili ulizozitaja inavyokwenda sawa na idadi ya maDAS uliyoitaja pia.
 
Wilaya gani ina halmashauri mbili na ded wawili?

Zipo nyingi tu mkuu, ila kwa kukujibu tu ngoja nitumie Mkoa wa Mtwara kwa mujibu wa takwimu za wizara ya TAMISEMI za leo hii tarehe 08-08-2018 ni kama ifuatavyo:-

Takwimu za Haraka
  • Idadi ya Watu = 1,356,800
  • Ukubwa wa Eneo = 16,720 (Km square)
  • Eneo la Kilimo = Hekta 1,400,000
  • Idadi ya Wilaya = 5
  • Idadi ya Halmashauri = 9
  • Idadi ya vyuo Vikuu = 02
  • Idadi ya Shule za Sekondari = 147
Soma hapo kwenye idadi ya wilaya (5) dhidi ya idadi ya halmashauri (9).
Na moja kati ya wilaya zenye halmashauri zaidi ya moja mkoani Mtwara ni Wilaya ya Mtwara (halmashauri ya manisapaa ya Mtwara almaarufu kama Mikindani na halmashauri ya mtwara vijijini) pia wilaya ya Masasi inazo halmashauri mbili.
 
Nisaidie link mkuu!!
Idadi ya madc ni 5 pia?
 
DED na DAS wanapoteuliwa na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara kumzidi mwenzake.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…