Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwakweli hawana kazi ya kueleweka kwani Maafisa Watendaji wa kata wanatosha. Unajua kipindi kile cha chama kimoja maagizo au utekelezaji ulikuwa unapitia kW DC. Sasa hivi unapitia kwa DED anashusha kwa WEO na Village Executive Officers.Mbona shughuli zao nyakati hizi wala hazionekani. Kipindi cha Nyuma nadhani kuanzia miaka ya tisini kurudi nyuma, ukisikia Katibu Tarafa anakuja kijijini ujue ni 'kimuemue'!!
Mkuu nafikiri unamaanisha DAS. RAS ni Boss wa watumishi wote katika Mkoa including wa mashirika na Taasisi zote za Serikali na za umma.DED mkubwa japokuwa sio bosi wa RAS, Ila ni mkubwa kwa kuwa pale wilayani DED hana bosi wake Ila yeye ndo top, Ila RAS pale wilayani ana bosi wake ambaye ni DC.
Anzisha uzi wako,Swali la msingi hapa ni.. Je kuna haja ya kuwa na DED pamoja na DAS kwa wakati mmoja? au nyadhifa mojawapo ingefutwa tu.
Hakuna wilaya zenye halmashauri mbili, bali wilaya yenye majimbo mawiliKwenye awamu hii wote wameteuliwa na rais.
Zamani TAMISEMI ilipokuwa ofisi ya waziri mkuu ndio ilikuwa DED anateuliwa na PM.
Siku hizi tamisemi IPO ofisi ya rais.
Zipo wilaya zenye halmashauri zaidi ya moja, DED -2, but DAS mmoja.
Wana majukumu tofauti, at one point DED anareport kwa DAS.
DAS anahudhuria vikao vya CMT kama mshauri, pia anahudhuria vikao vya baraza LA madiwani but hawajibiki kwao.
DAS line yake ya utendaji wa kila Siku iko sana kwa maafisa tarafa na wenyeviti wa vijiji/ vitongoji na mitaa , vyombo vyote vya ulinzi na usalama wilayani. He can surmon all government agencies in the district ( TRA,tanesco na taasisi nyingine zote kutoka wizara mbalimbali zilizo wilayani kwake) wakati DED anadeal zaidi na watumishi wa idara mbalimbali wakiwemo watendaji kata/ vijiji + madiwani. Na mamlaka ya DED yanaishia kwenye taasisi zilizo chini ya tamisemi tu.
Kisiasa imedeatelty juu ya DED yupo mwenyekiti wa halmashauri/ meya wakati kwa DAS yupo DC.
DAS yupo kidola zaidi wakati DED yuko kiutumishi/ umma zaidi.
DED ana nafasi kubwa ya kufa akiwa tajiri wakati DAS ana nafasi kubwa sana ya kufa maskini.
Wilaya gani ina halmashauri mbili na ded wawili?Kwa dhana ya "Wilaya" dhidi ya "halmashauri," mimi nadhani DAS yuko juu kiitifaki kuliko DED kwa mchanganuo ufuatao:-
DAS ni mtumishi wa wilaya. (Wilaya moja, DAS mmoja).
DED ni mtumishi wa halmashauri (kwenye Wilaya moja kunaweza kuwa na halmashauri zaidi ya moja).
Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba "Wilaya moja, DAS mmoja".
Na pia tunaweza kusema, "Wilaya moja halmashauri moja au mbili na hivyo DED mmoja au wawili"
Katika mazingira haya simuoni DED akiwa juu ya DAS.
Awamu iliyopita ded alikuwa anateulisa na PM chini ya upembuzi yakinifu ya waziri tamisemiTangu lini DED akateuliwa na waziri
Rc, RAS zipo chini ya wizara gani? Sio tamisemi? (Tawala za mikoa na serikali za mitaa?)DAS ni mfanyakazi wa mkuu wa Mkoa.
DC ni mfanyakazi wa mkuu wa Mkoa.
RAS ni mfanyakazi wa mkuu wa mkoa.
DED ni mfanyakazi wa TAMISEMI ambaye yupo chini ya Halmashauri ya wilaya/manispaa/mji (council as a whole).
DED hawezi kuwa chini ya DAS wala DAS kuwa chini ya DED.
DED hawezi hata kuwa chini ya DC, wala RC au RAS. Hawamuhusu kihivyo, bali katika kuwapa ripoti.
DED anaweza kumweka mtu selo kama DC anavyoweza au RC anavyoweza. Haingiliani na DAS,
Serikali kuu chini ya wizara gani?Mmoja ni mtumishi wa serikali kuu (DAS) mwingine ni mtumishi wa serikali za mitaa (DED)
Dc sio boss wa RAS,DED mkubwa japokuwa sio bosi wa RAS, Ila ni mkubwa kwa kuwa pale wilayani DED hana bosi wake Ila yeye ndo top, Ila RAS pale wilayani ana bosi wake ambaye ni DC.
Upo sahihi, mie nimesema kiitifakiSio tu kwa kuwa ana mafungu ila ki protocal DAS hana malka ya kumuagiza DED Lolote.
Leo umeamua kuja kivingine Moderators wakakugundua!😀😀😀Nimepata mkanganyiko kujua nani bosi wa mwenzake kati ya DAS na. DED naomba kuelemishwa mwenye kujua.
DED na DAS wanapoteuliwa wote kwa pamoja na kuanza kazi kwa pamoja nani anakuwa juu kimshahara.?
DAS wa wilaya ya nyamagana na DAS wa wilaya ya ilemela. Tambua halmashauri ya jiji la mwanza iliundwa na wilaya mbili tajwa hapo juu na baraza la madiwani lilikuwa moja, meya mmoja na mkurugenzi mmoja.
Wilaya gani ina halmashauri mbili na ded wawili?
Nisaidie link mkuu!!Zipo nyingi tu mkuu, ila kwa kukujibu tu ngoja nitumie Mkoa wa Mtwara kwa mujibu wa takwimu za wizara ya TAMISEMI za leo hii tarehe 08-08-2018 ni kama ifuatavyo:-
Takwimu za Haraka
Soma hapo kwenye idadi ya wilaya (5) dhidi ya idadi ya halmashauri (9).
- Idadi ya Watu = 1,356,800
- Ukubwa wa Eneo = 16,720 (Km square)
- Eneo la Kilimo = Hekta 1,400,000
- Idadi ya Wilaya = 5
- Idadi ya Halmashauri = 9
- Idadi ya vyuo Vikuu = 02
- Idadi ya Shule za Sekondari = 147
Na moja kati ya wilaya zenye halmashauri zaidi ya moja mkoani Mtwara ni Wilaya ya Mtwara (halmashauri ya manisapaa ya Mtwara almaarufu kama Mikindani na halmashauri ya mtwara vijijini) pia wilaya ya Masasi inazo halmashauri mbili.