Kati ya Ford Ranger Double Cabin na Land Cruiser Double Cabin, lipi ni gari bora zaidi kwa kazi za "porini"?

Mimi nimefanya kazi mgodi wa makaa ya mawe huko kusini, unamilikiwa na wazungu wa Uingereza. Pale mgodini mwaka 2014 walileta Ford Rangers 10 PX/ XRT na Land Cruiser 10 za field 1HZ engine zote pick up. Sikua Dereva wala mtu logistics ila mpaka naondoka pale 2020 Ford Rangers zinazotembea zilikuwa 3 zingine zote zimepaki yard mbovu, na zingine vipuri vyake ndo wanavichomoa huku wanaweka huku, Land Cruiser 1HZ zipo zipo 8 moja ilipiga chini, nyingine ilitumbukia mtoni. Nimekupa ninachikijua mkuu utaamua wewe.
 
Basi! Imetosha!!!

Umemaliza kiiila kitu!!!
 
cruiser kwenye maintenance ni cheap kuliko ford, interms of spare parts na mafundi ila kwenye durability ford ranger Hana mpinzani

Cruiser amempita Ford Ranger kwa mbali sana kwenye swala la maintenance, durability na spare parts isipokuwa kwenye speed, ford anachomoka hatari.
Ila kwa shughuli za pori cruiser hana mpinzani
 


Kazi ya kufananisha fisi na Simba kwenye uwezo wa kuwinda, no one can beat toyota Landcruiser porini.
 
Bado natafuta mwalimu wa kufundisha courses za computer kama vile word excel PowerPoint publisher adobe acrobat chatgpt windows operating system etc.kama una hiyo skillset usisite kunicheki
 
Ford itakupasua achana nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…