Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Ingekuwa Mungu anawauliza vijana wa leo wachague kati ya Hekima na Fedha unadhani wangechagua kipi?

1640502458909.png

Mfalme Sulemani akiongoza kikao cha Baraza la Wakeze. Taswira kwa hisani ya google.
 
Suleiman hakuwa majalala! Hilo la kwanza kabisa😅...

Sikuhizi bila hela utaishia kukoka kuni jikoni na hekima zako!
Hahahaaaa...
Mkuu, kwahiyo kwa kuwa hekima haitakiwi leo, ndiyo maana Hakimu/Jaji anamfunga asiye na hatia anamuacha huru mwenye hatia kwasababu anataka ela wala siyo hekima?

Pia ndiyo maana taasisi zikiwemo za kisiasa na kiserikali zinataka wenye ela kuliko wenye hekima.

Naogopa kwa mwendo huu dunia itafika mahala ambapo inaajiri Hakimu, Jaji, Askari, Tabibu, Daktari mwenye ela kuliko mwenye hekima ya taaluma yake? Hiyo dunia isinikute ningalipo.
 
Omba ufe mapema kabla hatujafika mkuu! Hekima bila hela haithaminiki sikuhizi hasa katika nchi yetu ya dunia ya 3 iliojaa dhiki na njaa kila kona sio wanasiasa wala wananchi wa kawaida!
 
Naamini Ukiwa Na Hekima Hata Pesa Utazipata Pitia Hekima Hizo Maana Dunia Ina Watu Wapuuzi.

Kwa Hekima Utaweza Kuwa-Manupulate Hawa Wapuuzi Na Kupata Pesa.

Heri Ya Christmas Kwenu Nyote.
Hata Suleman aliomba hekima akapewa ni vingine.. Maandiko yanasema hajawahi kutokea wala hatokaa atokee mwenye utajiri kama wake.
 
Nimeandika kichina au? Ndio maisha yalipofikia mtoto wa miaka 14 mwenye hela anaheshimika kuliko baba wamiaka 45 asiye na hela😅

Tuhakikishe tunapata hela tu! Dunia haina huruma.
Ingekuwa wenye pesa zao wana ^gari-la-aunt^ (guarantee) ya kuishi years on end, au angalau makaburi yao yana JF, FB & IG kwa ajili ya kuwasiliana na wahai wakiwa wamechimbiwa futi ^sea-tar^ chini ardhini, basi mimi hapa ningekuwa wa kwanza ^car-bee-sir^ kubatilisha mtazamo na kukuunga mkono wewe ^key-po-fu^ wa bara.

#KataaWahuni
 
Wangekuwa na pesa wangevuma zaidi kwani pesa yao inaongea. Mf. Jumba kubwa la kifahari linazidi kuvumisha jina lake . Ujanga uliotumika kupata hizo pesa ndio hekima yenyewe. Ila pesa bila dhuluma inavuma zaidi.
 
Hata Suleman aliomba hekima akapewa ni vingine.. Maandiko yanasema hajawahi kutokea wala hatokaa atokee mwenye utajiri kama wake.
Mkuu,

Kwahiyo ni kanuni ya uumbaji kwamba ni lazima viende pair?

Siyo kwamba Sulemani alipewa pesa kama motivation au ahsante kwa kuchagua kimojawapo kilicho chema, lakini siyo kwamba ni sharti viende pair? Tufundishe zaidi.
 
Ni nani amekuambia hao uliowataja hapo juu walikua hawana hela? Haya maneno ya vijiwe vya kahawa yanawapotosha sana
Mkuu,

Mandela alisema anataka aishi maisha ya zaidi ya thamani ya pesa, yaani hata kama hana pesa lazima atapata anachotaka kwa kutumia hekima, mfano ni nchi gani duniani ambayo Mandela angeenda kuomba chakula, nguo au matibabu ikamnyima? Hayo ndiyo maisha ambayo ni zaidi ya thamani ya pesa kwasababu aliwekeza hekima mioyoni mwa watu.

Nyerere kwa kutumia hekima yake aliwekeza kwa maskini na wanyonge duniani akawa hana maadui (kwasabbu maadui wanatengenezwa toka kwenye kundi la maskini wanaotafuta kujikomboa). Nyerere nyumba ya Msasani alizawadiwa na NHC, ile ya Butiama alijengewa kwa nguvu/ulazima na JKT, hakuwahi kujenga nyumba ya thamani ama kwa ela zake au ela za Ikulu. Kwa nafasi yake kama Mshauri wa Malkia wa UK Mwl alipewa nyumba Uingereza na Malkia akaikataa. Ni tajiri yupi basi mwenye ela asiyejuwa umuhimu wa kumiliki nyumba/makazi? Nyerere hakuwa na ela.

Nkrumah alitumia hekima kuasisi harakati za kudai uhuru na ukombozi wa Afrika, ikaja kumlipa uraia wa Afrika nzima badala ya Ghana pekee.

Katika kundi la marais tajiri Afrika Mandela, Nyerere na Nkrumah hawamo.
 
Suleiman hakuwa majalala! Hilo la kwanza kabisa😅...

Sikuhizi bila hela utaishia kukoka kuni jikoni na hekima zako!
umesema kweli mbaba suleiman hakuwa majalala kabisaa, lakin kumbuka pia suleiman huyohuyo hakuwa boya boya alikuwa na akili (hekima)

kuwa na hela zako jaza debe lakini bila akili (hekima) zitaishia kuziyeyusha kama siagi kwenye kikaango cha moto na utafanya mambo ya ajabu ajabu kama mwehu
 
Back
Top Bottom