Mkuu,
Mandela alisema anataka aishi maisha ya zaidi ya thamani ya pesa, yaani hata kama hana pesa lazima atapata anachotaka kwa kutumia hekima, mfano ni nchi gani duniani ambayo Mandela angeenda kuomba chakula, nguo au matibabu ikamnyima? Hayo ndiyo maisha ambayo ni zaidi ya thamani ya pesa kwasababu aliwekeza hekima mioyoni mwa watu.
Nyerere kwa kutumia hekima yake aliwekeza kwa maskini na wanyonge duniani akawa hana maadui (kwasabbu maadui wanatengenezwa toka kwenye kundi la maskini wanaotafuta kujikomboa). Nyerere nyumba ya Msasani alizawadiwa na NHC, ile ya Butiama alijengewa kwa nguvu/ulazima na JKT, hakuwahi kujenga nyumba ya thamani ama kwa ela zake au ela za Ikulu. Kwa nafasi yake kama Mshauri wa Malkia wa UK Mwl alipewa nyumba Uingereza na Malkia akaikataa. Ni tajiri yupi basi mwenye ela asiyejuwa umuhimu wa kumiliki nyumba/makazi? Nyerere hakuwa na ela.
Nkrumah alitumia hekima kuasisi harakati za kudai uhuru na ukombozi wa Afrika, ikaja kumlipa uraia wa Afrika nzima badala ya Ghana pekee.
Katika kundi la marais tajiri Afrika Mandela, Nyerere na Nkrumah hawamo.