Kati ya Kimara, Kigamboni na Kinondoni wapi ni bora zaidi kuishi?

Kati ya Kimara, Kigamboni na Kinondoni wapi ni bora zaidi kuishi?

Habari za mida hii wakuu

Poleni na Majukumu,

Poleni pia na maswaibu ya DPworld

Nimepata kibarua maeneo ya Posta.
Kwa sasa ninaishi Kibaha.

Hivyo nataka nihamie sehemu ambayo nitapunguza gharama ya usafiri na muda wa kusafiri.

Maeneo ambayo nashawishiwa ni Kimara, Kigamboni na Kinondoni.
Kati ya sehemu hizi ni wapi patakuwa bora zaidi.

Ukizingatia

Gharama ya chumba( <100K/month)
Usalama.
Urahisi wa kufika eneo la kazi(posta)
Hali ya hewa(joto).

Asanteni.

AbaMukulu Accumen Mo adden Aelknes Africa Yangu Aaliyyah Half american
Mabula Msirikale Mwachiluwi Saint Anne @Mwifa National Anthem Mzee wa kupambania mzabzab rikiboy
mshamba_hachekwi @
Kimara shida ni Usafiri, Kigamboni shida ni Uhalifu na Kinondoni utaambukizwa Uvivu na kupenda Starehe.

Chagua kwenye Unafuu Kwako Mkuu.
 
Omba usichelewe kuamka afu unatakiw uwahi kazin utaomba poo tulize tulisoma ifm afu una pepa ndo utajua kigambon ya wanafunz panton inajaa kama tenga la nyanya

Kinondoni-kuna mwendokasi zisipokuwepo kuna daladala
Kimara bei rahisi lakini usafiri asubuhi na jioni ni tabu
Duuh, kwhy mkuu kimara vyumba bei nafuu kuliko kigamboni.
 
Njoo kinondoni mkuu.huku akili yako itafunguka mkuu.huko kwengine akili yako italemaa.pia kinondoni ni rahisi kufika hapo poster mzee yaani usafiri bwelele ukitaka boda ukitaka mwendokasi ukitaka daladala wewe tu.halafu utaepukana na kuamka saa kumi na moja kuwahi usafiri...kinondoni ndio daslamaa ipo centa ya kotee
 
Kama una familia Kigamboni ni unapata nyumba kubwa na cheap kama kigetogeto kino is the best chumba master na sebule unakua karibu na mjini
 
Njoo kinondoni mkuu.huku akili yako itafunguka mkuu.huko kwengine akili yako italemaa.pia kinondoni ni rahisi kufika hapo poster mzee yaani usafiri bwelele ukitaka boda ukitaka mwendokasi ukitaka daladala wewe tu.halafu utaepukana na kuamka saa kumi na moja kuwahi usafiri...kinondoni ndio daslamaa ipo centa ya kotee
Tatizo kinondoni bei yao iko juu ya bajeti yangu.
Master room ndogo 150K.
 
Back
Top Bottom