Kati ya madirisha sita ya teller wa NMB, manne TEMPORARILY CLOSED. Hii tabia inakera!

Mambo vp wakuu,

NMB acheni ushamba na uzee

1. Hivi kwa dunia ya leo yenye furniture za bei chee mnashindwa hata kuweka utaratibu wa wateja wenu kuketi kwenye viti wakiwa wanasubiri huduma? Hebu jifunzeni kwa wenzenu na mtambue kuna baadhi ya wateja hawawezi kusimama kwa muda mrefu.

2. Huu utaratibu wenu wa "TEMPORARY CLOSED" kwa bank teller wenu ni fasheni au ndo kwa kuwa mna wateja wa kutosha?

Yaani madirisha 6 ya teller manne TEMPORARY CLOSED mawili tu yanafanya kazi? Na hili siyo mara moja labda tuseme dharura lakini ndio utaratibu wenu.

Acheni hizi tabia mnaboa mno!

Povu ruksa hata hivyo nitakuja kuongezea makandokando yenu mengine.
Yaani ndugu yangu inakera sana, wengine hatuwezi kusimama muda mrefu kutokana na maumivu ya miguu lakini hakuna viti tena matawi yote ya NMB nchi nzima. Halafu karibu kila siku madirisha mawili ndio yako active, unafika mahali unajiuliza hivi viongozi wa hii benki wameenda shuke kweli ?kweli NMB badilikeni kabisa. Hali hii inatuumiza sana sisi wateja wenu.
 
Kwa hiyo mnapoona foleni ndefu mnajisikia raha siyo. Hauko serious.
Huduma za kibenki zimehamia mtandaoni na mitaani.

Mawakala kila Kona, Unaweza kuhamisha miamala Kwenye simu,Unaweza kufanya direct transfer bank to bank mwenyewe.

Kwayo
Haina haja ya kua na utitiri wa TELLER ndani ya benki
 
Mi nikiona nimesimama saa moja bika huduma na teller ni mmoja naenda customer care kudai kwanini iwe hivyo.

Mara nne nimehudumiwa kiupendeleo mara mbili nime lazimisha kuonana na meneja na tellers kurudi madirishani. Mara moja nime ghairi kufanya miamala na kuondoka.

Hapa ujumbe ni kuwa tuanze kudai huduma za viwango kila mahali, hilo la benki ni mfano mdogo tu.

Mteja ni mfalme iende kwa vitendo. Tusisubiri kiongozi awe mkali mkali kunyoosha mambo.

Sasa ni wakati wa raia kuonesha hatutaki sifa za sijui watanzania wapole. Haitusaidii.
 
Yaani ndugu yangu inakera sana, wengine hatuwezi kusimama muda mrefu kutokana na maumivu ya miguu lakini hakuna viti tena matawi yote ya NMB nchi nzima. Halafu karibu kila siku madirisha mawili ndio yako active, unafika mahali unajiuliza hivi viongozi wa hii benki wameenda shuke kweli ?kweli NMB badilikeni kabisa. Hali hii inatuumiza sana sisi wateja wenu.
Kwa ufupi hawa jamaa aidha wanapuuza au hawana watu wa kuweza kufahamu washindani wao wanafanya nini.

Kuna mabenki ukiingia unatamani usitoke kwa jinsi walivyojipanga.
Nawauliza Nmb mmeshindwa hata kununua viti vya kukalia wateja wenu?
 
Huduma za kibenki zimehamia mtandaoni na mitaani.

Mawakala kila Kona, Unaweza kuhamisha miamala Kwenye simu,Unaweza kufanya direct transfer bank to bank mwenyewe.

Kwayo
Haina haja ya kua na utitiri wa TELLER ndani ya benki
Ni sawa lakini gharama ni kubwa "wallet to bank"- makato ni makubwa sana hasa kipindi hiki cha TOZO, hivyo hivyo Bank to wallet unafanya mara mbili maana yake utoe bank kupeleka kwenye simu (kuna makato kutoa bank na inaingia kwenye simu, na ukitoa kwenye simu unakutana na makato). Na ukifanya bank to bank(TISS) bado makato labda kama una hela nyingi lakini hela hizi za watumishi wa kawaida ni bora kwenda bank.
 
Yaani ndugu yangu inakera sana, wengine hatuwezi kusimama muda mrefu kutokana na maumivu ya miguu lakini hakuna viti tena matawi yote ya NMB nchi nzima. Halafu karibu kila siku madirisha mawili ndio yako active, unafika mahali unajiuliza hivi viongozi wa hii benki wameenda shuke kweli ?kweli NMB badilikeni kabisa. Hali hii inatuumiza sana sisi wateja wenu.
Kwa ufupi hawa jamaa aidha wanapuuza au hawana watu wa kuweza kufahamu washindani wao wanafanya nini.

Kuna mabenki ukiingia unatamani usitoke kwa jinsi walivyojipanga.
Nawauliza Nmb mmeshindwa hata kununua viti vya kukalia wateja wenu?
Hata crdb wanakuaga hivyo uzuri wao kuna viti vya kukalia wateja
Afadhali CRDB kuna pakukaa
 
Back
Top Bottom