Kati ya mahakama na benki ni ipi ina wajibu wa kumkabidhi msimamizi wa mirathi pesa za marehemu alizoacha benki au SimuPesa?

Ishu hela ya marehemu ni ngumu Sana kupatikana kwa mrithi, inapitia hatua nyingi kiasi Kama mtu wa kukata tamaa unawaachia mapema. Kikubwa kama una nywila Ni bora kachukue kwa njia ya atm, ikibaki zero ndo uende Mahakamani kufungua kesi ya mirathi. Kama alivyo sema mdau unapeleka barua kutoka Mahakamani ili waifunge akaunti ya marehemu na kuprocess pesa kutoka akaunti ya marehemu kwenda akaunti ya mahakama. Baada ya happy mahakama ndio wanawapatie warithi wote kupitia akaunti zao baada ya kikao Cha mgawanyo wa mali za marehemu pamoja na pesa. Kama unaweza komba pesa zote then ndo uende Mahakamani kwani the process will a time and money to make follow up!
 
Benki ya posta haijawafikia hiyo haipo
OK basi ipitie AC ya mahakama pia kuweni na imani na mahakama coz si mnamakaratasi mliyofafanuliwa kiasi cha pesa kilichopo cha marehemu? So ikiingia kwenye AC ya mahakama mtajulishwa kupitia sim ili mkacomfirm km ni ndicho kiasi husika.
 
Mkuu acha upotoshaji pesa haizunguki sana almost 6weeks ishatoka
 
Nilikwenda juzi kufuatilia BANK YA POSTA wakagoma kabisa hata kunipa Bank statements!
Sikuelewa kwanini wakati niliwaonesha barua ya kuteuliwa na mahakama pamoja mihutasari ya vikao!

Walidai sheria haiwaruhusu kudisplay information kwa mtu ambaye siyo mteja wao!
Wakaomba nirudi mahakamani nikawaletee Akaunti ya mahakama!
Halafu hakimu ndo atanipatia pesa kama zimo!
Nilihisi usumbufu
Sahihi kabisa,, ulipaswa uweke AC ya posta,,, au kama NI NMB uweke AC ya NMB au ujiunge mpya yenye maji na yako kamili yanayofanana na kwenye barua ya kiapo cha mahakamani kuwa wewe ni msimamizi wa mirathi
 
Mkuu acha upotoshaji pesa haizunguki sana almost 6weeks ishatoka
Mdau kaomba ushauri, toa uzoefu wako, mi nimetoa ushauri kulingana na experience yangu kwani ni mhanga na msimamizi wa mirathi na mpaka Sasa bado nasubiria Sasa unaponiambia 6 week, ebu piga mahesabu toka August 2020 mpaka leo wiki 6 tayari au bado?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
OK basi ipitie AC ya mahakama pia kuweni na imani na mahakama coz si mnamakaratasi mliyofafanuliwa kiasi cha pesa kilichopo cha marehemu? So ikiingia kwenye AC ya mahakama mtajulishwa kupitia sim ili mkacomfirm km ni ndicho kiasi husika.
Tatizo ni kule bank hawataki kutoa bank stament ili tujue kiasi cha pesa! Wanasema kilichopo kitatumwa mahakamani!
Pia wanasema eti marehemu alikuwa na mkopo! Sasa sielewi tangu lini marehemu anadaiwa!
Ndo kwanza nimesikia TPB!
Na mikopo navyojua huwa ina bima
 
Option zipo mbili

Either apewe msimamizi kabsa au ipitie mahakama,, japo mahakamani mzunguko wake ni balaa.

Eleza in details experience yako. Ili watu wajifunze na wajue inakuwaje... ukitoa majibu nusu nusu unakuwa hujamsaidia mtoa mada.. na wala member wengine hatujui ukweli ni upi.

Sema wewe ulilipwaje hiyo mirathi kwa njia za haraka haraka na ilikuwa mwaka gani?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mkuu acha upotoshaji pesa haizunguki sana almost 6weeks ishatoka

Dada ungetoa maelezo marefu mazuri ya experience yako kwenye mirathi.. ungewapa wengi sana mafunzo humu..
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mdau kaomba ushauri, toa uzoefu wako, mi nimetoa ushauri kulingana na experience yangu kwani ni mhanga na msimamizi wa mirathi na mpaka Sasa bado nasubiria Sasa unaponiambia 6 week, ebu piga mahesabu toka August 2020 mpaka leo wiki 6 tayari au bado?
Yeah
 
Kwa jinsi nnavyoelewa, mahakama hufungua akaunti ya mirathi na fedha zote hutakiwa kufikishwa hapo,

Kwa mfano kama marehemu alifanya kazi serikalini , basi fedha hutoka huko na kwenda kwenye hiyo akaunti pamoja na fedha za mifuko ya kijamii na bima ya maisha na vyanzo vingine vyote.

Kisha mahakama yachanganua na kuhakikisha kodi yalipwa TRA na kisha fedha hizo zaingizwa kwenye akaunti ya msimamizi wa mirathi katika benki ambayo atakuwa ana akaunti.

Benki nyingi hushauri mbali ya kuwepo msimamizi endapo wapo warithi ambao wamefikia umri wa miaka 18 wao watapaswa kuwa na akaunti zao ambapo mgao kama ulivyotanabaishwa na mahakama utaingizwa.

Ila kama wapo watoto chini ya miaka 18 fedha zao pia zaweza kuingizwa kwenye akaunti ya msimamizi au nao pia wakafunguliwa Child Account.

Msimamizi wa mirathi yupo kuhakikisha anafuatilia kila chanzo cha fedha cha marehemu na si lazima ategemee kupata windfall wakati warithi halisi wapo.
 
Okay asante kwa maelezo
 
Eleza in details experience yako. Ili watu wajifunze na wajue inakuwaje... ukitoa majibu nusu nusu unakuwa hujamsaidia mtoa mada.. na wala member wengine hatujui ukweli ni upi.

Sema wewe ulilipwaje hiyo mirathi kwa njia za haraka haraka na ilikuwa mwaka gani?
Niulize usipopaelewa
 
Mkopa inategemea na mashart aliyosign marehemu ni haki yao kudai ikiwa masharti yalielekeza hivo kipindi cha uchukuaji mkopo.

Pili bank statement itatolewa mpaka upeleke nyaraka za mahakamani zenye uthibitisho kuwa wewe ndie mrithi ukiambatanisha na barua ya mahakama inayowataka watoe pesa za marehemu.

Read above dmkali
 
Mdau kaomba ushauri, toa uzoefu wako, mi nimetoa ushauri kulingana na experience yangu kwani ni mhanga na msimamizi wa mirathi na mpaka Sasa bado nasubiria Sasa unaponiambia 6 week, ebu piga mahesabu toka August 2020 mpaka leo wiki 6 tayari au bado?
Sijajua ulipokwama,,, na ulipoanzia na ikawaje mpaka sasa usipewe hata nusu ya mirathi.

So I need an explanation
 
Mikopo mara nyingi ina bima, nafikiri bima ndo itafanya kazi yake
 
Kwa jinsi nnavyoelewa, mahakama hufungua akaunti ya mirathi na fedha zote hutakiwa kufikishwa hapo,

Kwa mfano kama marehemu alifanya kazi serikalini , basi fedha hutoka huko na kwenda kwenye hiyo akaunti pamoja na fedha za mifuko ya kijamii na bima ya maisha na vyanzo vingine vyote.

Kisha mahakama yachanganua na kuhakikisha kodi yalipwa TRA na kisha fedha hizo zaingizwa kwenye akaunti ya msimamizi wa mirathi katika benki ambayo atakuwa ana akaunti.

Benki nyingi hushauri mbali ya kuwepo msimamizi endapo wapo warithi ambao wamefikia umri wa miaka 18 wao watapaswa kuwa na akaunti zao ambapo mgao kama ulivyotanabaishwa na mahakama utaingizwa.

Ila kama wapo watoto chini ya miaka 18 fedha zao pia zaweza kuingizwa kwenye akaunti ya msimamizi au nao pia wakafunguliwa Child Account.

Msimamizi wa mirathi yupo kuhakikisha anafuatilia kila chanzo cha fedha cha marehemu na si lazima ategemee kupata windfall wakati warithi halisi wapo.
Utaratibu ni kwamba mkishakaa kikao cha familia na kupendekeza msimamizi anakwenda Mahakani kufungua shauri la mirathi, Mahakama ikijiridhisha kuwa anafaa inamteua na inampa form ya uteuzi inaitwa form Na Iv ambayo inakuwa na picha ya mtu huyo baada ya hapo Sasa.

1. Kama marehemu alikuwa na Akaunti Banki, then, kadi za benki zinapelekwa Mahakamani na Mahakama inaandika bafua kwenda Benki huska ikiambatanisha na kadi hizo na kuitaka funge akaunti hiyo na kupeleka fedha zilizom kwenye Akaunti ya Mirathi ya Mkoa huska iliyoko B.O.T.

Wakishafunga akaunti Benki wanatuma Benki statement Mahakani na kuonyesha kiasi kilichomo wakati wa kufunga akaunti hiyo na kuthibitisha kuwa wameituma kwenye Akaunti hiyo ya hazina. Baada ya hapo Mahakama inamtarifu msimamizi na kumueleza akaunti imefungwa na ina fedha au laa, Kama inafedha masimamizi atatakiwa kukaa kikao na warithi na kukubaliana namna ya kugawana fedha hizo na kupeleka muhtasari na mchanganuo Mahakamani. Then wanajaza form Na VI ambayo itaambana na viambatanisho vya kila mrithi ambavyo ni Na. Ya Akaunti, vyeti vya kuzaliwa, vendor form ya benk huska, nakala za kadi za benki, N.k. vikishapelekwa huko hazina kwenye mkoa huska, na kama havina kasoro, fedha inaingizwa moja kwa moja kwenye Akaunti.( Mara nyingi kuchelewa kulipwa husababishwa na warithi Kama nyaraka zao zinazotakiwa kuambatanishwa hazijatimia au haziko sahihi). Lakini njia nyepesi mara nyingi kuondoa ususmbufu hasa kama fedha siyo nyingi ni bora kumchagua mmoja na kukubaliana fedha yote iingie kwake, so viambatanisho vinakuwa vya mtu Mmoja na akaunti inakuwa moja.

2. Kama Marehemu alikuwa mtumishi, hapa Mahakama inahuska
(A) kwenye uteuzi wa msimamizi ambaye atawajibika kwenda kwenye mfuko huska akiwa na hati ya uteuzi na huko atapewa form ambazo kila mrithi atajaza na ataambatanisha Na. ya Akaunti kadi yake ya Benki na vendor form ya Benki yake, pia atalazimika kupitia kwa mwajiri wa Marehemu kuna Sehemu anajaza na Kuna Sehemu Mahakama inajaza na hiyo form inakuwa na paspoti karibia tatu ambazo lazima zigongwe mhuri wa Mahakama na kusainiwa na hakimu na inaambatanishwa form na VI ambayo itakuwa inaonyesha mgao kwa Kila mrithi na Mara nyingi mgao unakuwa kwa % kwakuwa fedha inayokuwa kwenye mfuko Mara nyingi inakuwa haifahamiki na viambatanisho vingine ikiwemo vyeti vya kuzaliwa vya kila mmoja(Hapa kila mrithi lazima aweke akaunti Na yake hata Kama ni mtoto mdogo lazima afunguliwe akaunti na hata warithi wakubaliane vipi fedha hii mifuko ya jamii haikubali kuingiza kwenye Akaunti ya mtu mmoja), viambatanisho vyote mhimu ikiwemo vyeti vya kuzaliwa vya kila mrithi( Na hapa ndipo Mara nyingi kunakuwa na tatizo na kusababisha warithi kuchelewa kulipwa kutokana na kushindwa kutimiza au kuwa na baadhi ya nyaraka). Kama nyaraka zimekamilika fedha inalipwa moja kwa moja kwenye Akaunti husika ya kila mmoja.
 
Sijajua ulipokwama,,, na ulipoanzia na ikawaje mpaka sasa usipewe hata nusu ya mirathi.

So I need an explanation
Hatua iliyofikia ni kusubiri akaunti ya mahakama kuweka pesa kwenye akaunti za warithi
 
Back
Top Bottom