Never ever do that. Wewe tumia hiyo process ya mahakanma, lakini nzuri kuliko vyote ni kuacha wosia. Wosia uataifanya kazi ya mahakama na msimamizi wa mirasthi kuwa rahisi. Lakini hii ya kumuamini mtu ina matatizo. Kwanza watu hubadilika. Anaweza kuwa mwaminifu leo, lakini akiona kitita cha pesa uaminifu ukamtoka. Pili, anaweza akawa mwanifu kweli, lakini akazuliwa maneno na ndugu kuwa kiasi kilichoonekana ni kidogo kuliko walichokuwa wanajuwa marehemu anacho. Kutakuwa na maneo mengine, eti alichota kwanza na ndiyo aklatuambia kiasi kilicho huko benki. Kuepuka haya yote acha wosia na msimamizi afuate wosia na uamuzi wa mahakama.