Utaratibu ni kwamba mkishakaa kikao cha familia na kupendekeza msimamizi anakwenda Mahakani kufungua shauri la mirathi, Mahakama ikijiridhisha kuwa anafaa inamteua na inampa form ya uteuzi inaitwa form Na Iv ambayo inakuwa na picha ya mtu huyo baada ya hapo Sasa.
1. Kama marehemu alikuwa na Akaunti Banki, then, kadi za benki zinapelekwa Mahakamani na Mahakama inaandika bafua kwenda Benki huska ikiambatanisha na kadi hizo na kuitaka funge akaunti hiyo na kupeleka fedha zilizom kwenye Akaunti ya Mirathi ya Mkoa huska iliyoko B.O.T.
Wakishafunga akaunti Benki wanatuma Benki statement Mahakani na kuonyesha kiasi kilichomo wakati wa kufunga akaunti hiyo na kuthibitisha kuwa wameituma kwenye Akaunti hiyo ya hazina. Baada ya hapo Mahakama inamtarifu msimamizi na kumueleza akaunti imefungwa na ina fedha au laa, Kama inafedha masimamizi atatakiwa kukaa kikao na warithi na kukubaliana namna ya kugawana fedha hizo na kupeleka muhtasari na mchanganuo Mahakamani. Then wanajaza form Na VI ambayo itaambana na viambatanisho vya kila mrithi ambavyo ni Na. Ya Akaunti, vyeti vya kuzaliwa, vendor form ya benk huska, nakala za kadi za benki, N.k. vikishapelekwa huko hazina kwenye mkoa huska, na kama havina kasoro, fedha inaingizwa moja kwa moja kwenye Akaunti.( Mara nyingi kuchelewa kulipwa husababishwa na warithi Kama nyaraka zao zinazotakiwa kuambatanishwa hazijatimia au haziko sahihi). Lakini njia nyepesi mara nyingi kuondoa ususmbufu hasa kama fedha siyo nyingi ni bora kumchagua mmoja na kukubaliana fedha yote iingie kwake, so viambatanisho vinakuwa vya mtu Mmoja na akaunti inakuwa moja.
2. Kama Marehemu alikuwa mtumishi, hapa Mahakama inahuska
(A) kwenye uteuzi wa msimamizi ambaye atawajibika kwenda kwenye mfuko huska akiwa na hati ya uteuzi na huko atapewa form ambazo kila mrithi atajaza na ataambatanisha Na. ya Akaunti kadi yake ya Benki na vendor form ya Benki yake, pia atalazimika kupitia kwa mwajiri wa Marehemu kuna Sehemu anajaza na Kuna Sehemu Mahakama inajaza na hiyo form inakuwa na paspoti karibia tatu ambazo lazima zigongwe mhuri wa Mahakama na kusainiwa na hakimu na inaambatanishwa form na VI ambayo itakuwa inaonyesha mgao kwa Kila mrithi na Mara nyingi mgao unakuwa kwa % kwakuwa fedha inayokuwa kwenye mfuko Mara nyingi inakuwa haifahamiki na viambatanisho vingine ikiwemo vyeti vya kuzaliwa vya kila mmoja(Hapa kila mrithi lazima aweke akaunti Na yake hata Kama ni mtoto mdogo lazima afunguliwe akaunti na hata warithi wakubaliane vipi fedha hii mifuko ya jamii haikubali kuingiza kwenye Akaunti ya mtu mmoja), viambatanisho vyote mhimu ikiwemo vyeti vya kuzaliwa vya kila mrithi( Na hapa ndipo Mara nyingi kunakuwa na tatizo na kusababisha warithi kuchelewa kulipwa kutokana na kushindwa kutimiza au kuwa na baadhi ya nyaraka). Kama nyaraka zimekamilika fedha inalipwa moja kwa moja kwenye Akaunti husika ya kila mmoja.