Kati ya Mama na Mke Nani anapaswa kukaa Siti ya mbele wakati unaendesha Gari?

Yani kushindana na mtu ambae hatuwezi kushea utamu huwa ni uzwazwa, mi naona ndg na rafiki wanawaweza niweka roho juu ila so mama mkwe na mawifi
 
Principle of nature, baba au mama yako hakuanza kukupenda kwanza wewe, baba alimpenda kwanza mke wake( mama yako) na mama alimpenda kwanza mume wake( baba yako) ndipo wewe ukazaliwa. Kwa hiyo always wa kwanza ni mke au mume ndio wafate wengine
 
Kwanza unipe tafsiri ya maana ya familia.
Sisi wengine extended.

Nafasi ya mke ni mkamwana tu.

Familia ni Baba, Mama na watoto. Hiyo ndio maana halisi ya Familia.
Hizo zingine ni maana za ziada,

Mke ni mkamwana Kwa wazazi wako sio kwako au Kwa Watoto wako.

Baadaye wake zenu wakiwachukulia kama nanyi Watu wa ziada wakiwa na watoto mnaanza kuwaona Wanawake ni wabaya.

Kumbe ubaya umeanzia Kwa Mume.
Mama yako Hana mamlaka na ushawishi wowote Kwa Watoto wako utakaowazaa.
Hivyo kama utamu- undermine Mkeo sio ajabu baadaye Watoto wako nao wakaku- Undermine.
 

Umeongea ukweli kabisa.
Ila wapo Wamama wanawachokoza Wakamwana wao Kwa kutaka kujionyesha kuwa wao ndio wananafasi kubwa katika Maisha ya kijana.
Wadada wengi wanawaheshimu Mama Wakwe hasa wakiwa wanapendwa na Waume zao na kuheshimiwa na Wakwe zao.

Lakini kuna Mama Wakwe hutoa maneno ya kashfa Kwa Wakamwana wao huku wakiwanyanyasa, unategemea MKE atafanyaje?
Mimi huwaga napenda Haki, hata kama ni Mama yangu, akitaka apewe Heshima sharti naye atoe Heshima.
Masuala ya kusema sijui yeye ni Mama au Baba au Mkwe haina maana asitende Haki.

Mwanaume lazima Watu wakujue kuwa wewe ni MTU wa Haki Hii itakusaidia kutatua mambo mengi.
Mke afanye sehemu yake, katika utawala wake, akiwa nyumbani kwake.

Sitokubali MKE wangu asitende Haki alafu nimuache kisa ATI ni MKE wangu tumefunga ndoa sijui ya kifungo cha Maisha.
Wala sitokubali Mama yangu akiwa katika utawala wangu akitenda kinyume cha Haki Kwa kisingizio cha kunizaa. Hiyo haipo.

Ishu ya wakukaa SITI ya MBELE ni ishu ndogo mno. Wala haiwezi kufikiriwa na watu wenye Akili na waungwana.
Mama Mwema hawezi kugombea SITI halikadhalika na MKE Mwema.
Upendo ukitawala yeyote anaweza kukaa MBELE. Lakini kama ubinafsi ulianza kujitokeza basi sheria na Kanuni zitafuatwa
 
Said it all.
 
Kuna wanaume wema wengi
Waliotenda mema kwa wake zao
Zaidi ya Siti karibu na usukani.

Ila Sasa uzeeni wanakufa peke Yao
Wanakufa kihayawani
Wanadhalilishwa na Wake zao
Ambao kwao waliwaona tunu

Wapo wanaume waliowatweza Wazazi
Wakapapalikia Mke, Wakwe
Ila walipopata maswahibu wakabaki na
Wakwao.

Wapo wanaume walioona walio wekeza
Kubwa kwa watoto
Nao wakajisahau maendeleo yao
Nao mbunga likapita,
Wakajikuta wanyonge, wakiwa wakati Wana wao wakitumbua maisha.

Hawa silika hii ya wanawake kizazi hiki
Mwana akiwa mdogo ni wako
Utasikia Mtoto wako
Mimba yako
Baba naniiii

Hii silika ya Wanawake mtoto akikua
Anakuwa kashapandikiza sumu
Mtoto ni wake
Na jamii yake
Mabaya yako yatatangazwa
Hata ikiwa ni urongo

Usimwone Mkeo ni wa tofauti
Fuata haki
Na subiri
Asili iongee
Ila huna uhakika kama watakuwa nawe uzeeni kwako Wala huo upendo
Ila wazazi wako unajua washajitoa kwa mangapi?

N.B Wanaume tutakaa mbele
Kila mtu ana umuhimu wake
Ila mpe mzazi kile roho inapenda.
View attachment 2448457
 
Siku hizi kuna wanawake wanaambatana na wazazi wao kuliko hata waume zao.
 

Ukitenda Haki uzee wako hauwezi kuwa Mbaya, niamini Mimi.

Unaweza kuwa Mwema Kwa Mkeo na Mama yako. Lakini ukawa unawadhulumu Watu wengine Haki zao. Hapo lazima uonje joto la jiwe.

Asilimia kubwa na maanisha 90% wanaoteseka mwishoni I mean uzeeni wengi walifanya dhulma sehemu Fulani na Kwa Watu Fulani.

Kila MTU mpe Haki yake Kwa nafasi yake.
Unampa Haki Mama yako kupitiliza alafu unampunja Mkeo. Lazima ulipie.
Unampa Mkeo Haki kupitiliza alafu unampunja Mama yako. Lazima ulipie.
Unaipenda familia yako na wazazi wako lakini unaipunja Haki jamii inayokuzunguka lazima ulipie. Tena Hii ndio ipo Sana. MTU inafikia hatua anafanya ufisadi na kudhuru jamii kisa familia yake. Lazima Ngoma ijibu. Kwa namna yoyote Ile.
 
Siku hizi kuna wanawake wanaambatana na wazazi wao kuliko hata waume zao.

Hii ipo Sana.
Dawa ya Mwanamke wa namna Hii ni kuachana naye tuu.
MTU asiyeelewa maana ya familia hawezi kuijenga familia yake
 
Wote wakae nyuma!

Ila kama ni mama mwenye busara hawezi kukaa mbele atakuambia kaa mbele na mwenzako.

Yeah!

Pia kama ni mgeni ni vizuri akae Mbele ili umuonyeshe Jiji vizuri.
Yote yatafanyika Kwa upendo
 
Yani kushindana na mtu ambae hatuwezi kushea utamu huwa ni uzwazwa, mi naona ndg na rafiki wanawaweza niweka roho juu ila so mama mkwe na mawifi
Kabisaaa yaani Mimi akae mbele aendeshe whatever yeye itampa faraja afanye,Mimi mama mkwe alikua anaingia chumbaniii kabisa kwetu asubuhi na Wala sijawahi kuchukia niliona tu Hana mwiko na hawana maadili ya kwetu baasii...
Yaani wanatoka na mwanawe miye Wala sijali,Wanakaa wanaongea miye nalala habari sipati...mpk leo ananipendaga yule mama

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ngoja nikuulize kitu,hivi Kuna tofauti kati ya mama mzazi na mama mkwe?
Km amezaa Mume Kwa Nini nisimheshimu?kuchokozaje Kwa mfano? as a wife mama angu mzazi akinichokoza narespond vipi?km namjibu au nagombana nae baaasi I will do the same to mama mkwe but if not I won't dare to quarrel with her,siwezi shindana na Pepo ya Mume wangu maana mwanaume Pepo yake Iko chini ya nyayo za mama yake na Mimi peoi yangu Iko chini ya Mume wangu.

Shida Moja tu wengi wengu hatunaga adabu kwa watu wasotuzaa na Kwa kesi ya mkwe tunamchukulia km outsiders while not yule ni mama wa Mume wangu hvyo ni mzazi wangu pia...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…