Pre GE2025 Kati ya mkutano wa Lissu, Lema na Kigaila upi ndiyo msimamo wa CHADEMA?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
..yote ni misimamo ya Chadema.

..Chadema wana mfumo wa KANDA.
Wachache, na pengine ni Kigaila tu ndiye atayekuelewa hapa.
Kifupi: CHADEMA wamepoteana. Wana moja tu la kufanya ili warudi katika chati. Nalo ni kumchagua LISSU kuwa m/kiti wao wa chama. Wakati huo huo wahakikishe kuwa Kigaila hashiki nafasi yeyote ile ya uongozi ndani ya chama, hususan ukatibu mkuu.
 
kajengeni kwanza chadema yenu inakufa huko wenyekiti wanagombana ndiyo u je uhoji mambo ya nchi yanavyoenda utaambiwa
 
kwakweli chadema wamepoteana na wasipoangalia watajuta na mbowe hawezi kubali kuachia wenyekiti kirahisi hivyo
 
Hakuna mkusanyiko wowote wa kisiasa iwe chama au kikundi wenye mawazo yanayofanana.

Lissu alifanya tathmini ya hali ya kisiasa kwa kurejea matukio ya sasa ya uchaguzi wa serikali za mitaa na mlolongo mzima tangu utawala huu uingie madarakani. Kisha akaelezea maoni yake nini kifanyike hakusema Chadema itafanya hivi.
 
kajengeni kwanza chadema yenu inakufa huko wenyekiti wanagombana ndiyo u je uhoji mambo ya nchi yanavyoenda utaambiwa
Chadema ipi inakufa we fisadi? Mngekua mnahangaika nayo kila siku? Kupishana kauli ndio demokrasia yenyewe maana hamuwezi fikiri sawa, ukiona wote mna mawazo sawa ujue mmejaa uoga na kujikomba tu.
 
Gentleman,
sasa kama ni hivyo kuna haja gani ya kua na chama au familia, ikiwa kila moja anaweza kuamka asubuh akasema au akafanya atakavyo?

Kama Lisu kafanya tathmini binafsi juu ya hali ya siasa, iweje atumie mgongo wa Chadema?

Au chadema hua haifanyi tathmini juu ya mambo hayo?

kwani Lisu, Lema, Kigaila na chadema nani ni muhimu zaidi ya mwingine?πŸ’
 
Ndani ya chadema kuna vibaraka wa aina tatu.

1) vibaraka wa Mbowe

2)Vibarak Wa lissu

3) Vibaraka wa CCM.

Itoshe kusema Chadema Kushney.
 
Kuwa kiongozi maana yake sio kuwa bubu bado mtu ana maoni yake binafsi mambo ya ndio ndio ni ya wanafiki pekee. Baada ya kutoa maoni yake amesuggest way forward sasa ni juu ya chama chake watakapokutana kujadili mambo yao wataamua to what extent wayachukue maoni ya Lissu au kutoyachukua kabisa na watatoka na msimamo mmoja na ndiyo utakuwa msimamo wa chama.
 
amesagest kwa nani sasa hayo maoni yake binafsi ndrugo yangu selfish?

Juu ya chama chake tena?🀣
kwamba yeye ni useless kiongozi right?

Kwahiyo chadema ina viongozi wa kufanya kazi binafsi kupitia mgongo wa chama right?

sasa wakutane kujadili nini wakati kila moja kaishaeleza mambo yake binafsi kwenye vyombo vya habari na mitandaoni ya kijamii?πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…