Kati ya Wizara ya Fedha na TRA mmoja kadanganya mahesabu kwenye ripoti ya mapato 2022/23

Weka ushahidi.

Mimi binafsi sijali serikali ya nani anaefanya vizuri namsifia, anaefanya vibaya naeleza wapi naona anakosea kwa muono wangu.

Mwendazake nimemsifia sana, pitia nyuzi zangu kuhusu yeye. Nilipoona watu wanapotea potea hovyo nikajiogopea na mimi nikawa kimya sana hapa JF.

Magufuli alikuwa na nia njema kwa Tanzania lakini tatizo lake alijimwambafai sana na alilewa madaraka mapema.
Asante kwa ufafanuzi.
 
Habarini waungwana!

Kama kichwa Cha mada kinavyojieleza.

Kipindi waziri wa fedha anaiwasilisha hotuba ya bajeti mwaka 2023/2024 katika kipengele 'IV. Tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya serikari kwa mwaka 2022/23 alieleza serikali ilitaraji kukusanya trilion 41.48 kutoka vyanzo vya ndani na nje Hadi Aprili 2023 jumla ya shilingi Trilion 32.43 zilipatikana kutoka vyanzo hivyo.
Mchanganuo wa mapato yaliopatikana ni kama ifuatavyo

Mapato yaliopatikana kupitia mamlaka ya mapato Tanzania yalikuwa ni shilingi Trilion 18.81 ambapo lengo la mwaka ni shilingi Trilion 23.65.' Naiweka nukta hapa Tuje kwenye Ripoti iliotolewa na TRA TRA walitoa taarifa kwa umma.

Ripoti ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Julai 3, 2023 Ambapo mamlaka ya mapato iliutaarifu umma katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2022/23 mwezi Julai 2022 Hadi Juni 2023 mamlaka imefanikiwa kukusanya kiasi Cha shilingi Trilioni 24.11 sawa na ufanisi wa 97.1% katika lengo la kukusanya shilingi Trilioni 24.76.

Naiweka nukta Swali la kwanza TRA katika bajeti ya mwaka 2022 alipewa jukumu la kukusanya shilingi Trilioni 23.65 Nani alitoa jukumu kwa TRA la kukusanya Trilioni 24.76 kama mamlaka ilivyo tutaarifu kwenye taarifa yake kwa umma?

Swali la pili Wizara ya fedha kwenye Hotuba ya Bajeti 2023/2024 kwenye kipengele Cha tathimini ya Bajeti 2022/23 Wizara inasema TRA ilikusanya shilingi Trilioni 18.81 kuanzia Julai 2022 Hadi Aprili 2023. Wakati Ripoti ya TRA kwenye jedwali namba 1: makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Ukijumrisha makusanyo yote kutokea Julai 2022 Hadi Aprili 2023 unapata trilioni 20.00 Kuna nini hapa?

Nawasilisha

View attachment 2679986View attachment 2679987
Kwani pesa zote za serikali zinakusanywa na tra peke yake? Mie nadhani Kuna taasisi nyingi tu ambazo zinapeleka pesa serikali kuu bila kupitia tra ndio maana Kuna utofauti wa hizo taarifa.
 
Soma tena Uzi vizuri na pitia hizo attachment utaelewa msingi wa mada
 
Kwani pesa zote za serikali zinakusanywa na tra peke yake? Mie nadhani Kuna taasisi nyingi tu ambazo zinapeleka pesa serikali kuu bila kupitia tra ndio maana Kuna utofauti wa hizo taarifa.
Kwa maana hiyo data za wizara ndio zilipaswa kuwa kubwa, lakini hapa inaongelewa data za tra kuea kubwa kuliko za wizara. Sijui kama umenielewa?
 
Ni makosa tu sometime hutokea kulingana na uharaka wa taarifa,mfano hiyo taarifa ya utekelezaji aliyoisoma Waziri ili uweze kuiandaa inakubidi kupewa taarifa na taasisi Mama (TRA) kisha ndio uandae.

Hivyo,basi kama ni makosa walifanya watu wa TRA wakati wanatoa hizo taarifa na sio Wizara ya Fedha.Hata hivyo taarifa ya Mwaka ndio taarifa complete.
Hizo taarifa za kwenda Bungeni huwa tunazindaa kwa zimamoto sana and under pressure sana-kukidhi mahitaji ya walaji.
Tafsiri fupi Wizara uwaga inapewa taarifa za uhongo?
 
Wanajua watanzania huwa hawajishughulishi na taarifa kwa kina,hivyo huwa wanaburuza tu,hakuna wa kugundua hilo

Huwa tunagundua sana na ndio maana tunasema mara kibao huku kuwa ni serikali ya wapika data. Tatizo letu sio kujua uongo wao, bali sisi ni makondoo hata tukijua tutawafanya nini?
 
Taarifa ya Wizara ni mpaka April
TRA ni mpaka 3 Julai. Figure zinawezaje kuwa sawa?
Hoja yako ina kasoro
 
Kwahiyo Wizara Mpaka inaandaa Tathimini ya Bajeti Ilishindwa kuweka hiyo Adjustment kwenye Data zao?
Siyo mtaalamu sn lakini ni kwamba Wizara inadeal na budget kuu lakini TRA wanadeal na kodi pekee so hata council huwa zinafanya adjustment
 
Target ya TRA makusanyo ya mapato kwa mwaka anapangiwa na nani?
 
Yes Wizara ya fedha ndio inampa Target TRA... Sasa kilichopo Target ya Wizara hipo chini kuliko target waliotolea Ripoti TRA ndio swali la kwanza limelenga hapo
Huwa wanapewa hata councils zinapewa lakini wanaruhusiwa kufanya adjustment mkuu
 
Habarini waungwana!

Kama kichwa Cha mada kinavyojieleza.

Kipindi waziri wa fedha anaiwasilisha hotuba ya bajeti mwaka 2023/2024 katika kipengele 'IV. Tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya serikari kwa mwaka 2022/23 alieleza serikali ilitaraji kukusanya trilion 41.48 kutoka vyanzo vya ndani na nje Hadi Aprili 2023 jumla ya shilingi Trilion 32.43 zilipatikana kutoka vyanzo hivyo.
Mchanganuo wa mapato yaliopatikana ni kama ifuatavyo

Mapato yaliopatikana kupitia mamlaka ya mapato Tanzania yalikuwa ni shilingi Trilion 18.81 ambapo lengo la mwaka ni shilingi Trilion 23.65.' Naiweka nukta hapa Tuje kwenye Ripoti iliotolewa na TRA TRA walitoa taarifa kwa umma.

Ripoti ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Julai 3, 2023 Ambapo mamlaka ya mapato iliutaarifu umma katika kipindi Cha mwaka wa fedha 2022/23 mwezi Julai 2022 Hadi Juni 2023 mamlaka imefanikiwa kukusanya kiasi Cha shilingi Trilioni 24.11 sawa na ufanisi wa 97.1% katika lengo la kukusanya shilingi Trilioni 24.76.

Naiweka nukta Swali la kwanza TRA katika bajeti ya mwaka 2022 alipewa jukumu la kukusanya shilingi Trilioni 23.65 Nani alitoa jukumu kwa TRA la kukusanya Trilioni 24.76 kama mamlaka ilivyo tutaarifu kwenye taarifa yake kwa umma?

Swali la pili Wizara ya fedha kwenye Hotuba ya Bajeti 2023/2024 kwenye kipengele Cha tathimini ya Bajeti 2022/23 Wizara inasema TRA ilikusanya shilingi Trilioni 18.81 kuanzia Julai 2022 Hadi Aprili 2023. Wakati Ripoti ya TRA kwenye jedwali namba 1: makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Ukijumrisha makusanyo yote kutokea Julai 2022 Hadi Aprili 2023 unapata trilioni 20.00 Kuna nini hapa?

Nawasilisha

View attachment 2679986View attachment 2679987
Hapa Mkuu umemkamata Simba kwenye kudevu

Tumepigwa sana
 
Back
Top Bottom