Mkandara,
Kwanza kwa maelezo hapo juu, samahani maana naona nilikuelewa vibaya. Mie nilijua kuwa katika hiyo hotuba, kama limewekwa pia pingamizi, basi wataliangalia na lenyewe. Kumbe wanaangalia kanuni tu kama Jokakuu alivyodadavua hapa chini. Labda tu hapa na mie niongeze swali, hivi Pingamizi linatakiwa kuwa na MANENO/MISTARI mingapi?
Kuhusu swali lako hapa chini, jibu lake lipo kwenye Video hii chini: Ntaanza kwa maelezo kama ulikuwa hujayasoma na mwisho ni Video yenyewe ambayo ukiweza sikilia tena::>>
Baada ya kusikiliza hotuba ya Tundu Lisu, anasikika kabisa akitaja Kifungu cha 86 (3) (b) na kulitaka BUNGE likatae mjadala kusomwa mara ya pili.
Pia mwisho ni kweli alikosea na kusema ".......Muheshimiwa Spika, naomba kuwakilisha." Ila baada ya sekundi chache, alirudia ujumbe wake na kusema "......
naomba kutowa hoja muheshimiwa spika."
Spika akaja na kicheko chake na kusema TL ametumia kifungu cha 86 (6) na anasema ".... Muheshimiwa TL anawasilisha hotuba maoni ya kambi ya upinzani kwa kanuni ya 86 (6).
Hiyo haitowi hoja ni maoni yake na ...... hayo ni
maoni ya kambi ya upinzani."
Ukifuatilia zaidi, unasikia sasa sauti ya
John Mnyika akisema wazi kabisa "HOJA KUAHIRISHA BUNGE." Hoja ya kuahirisha Bunge imeandikwa kwenye kifungu hicho cha 86 (3) (b) na inaweza kutolewa na mbunge yeyote. Maadamu wabunge wote hawawezi kusema pamoja, kuna uwezekano wa wenye hoja hiyo wakachelewa, kama Mnyika.