Kuna mawili, aidha hukusoma ama hujui kabisa hesabu ama la ulisoma na ukapata zero.
Kama tuna barabara za lami zinazofikia urefu wa km 5,000 na kuna wakandarasi wanajiandaa kuanza ujenzi ili tufikishe barabara zenye urefu wa km 10,000 hapo ni kusema takribani barabara za urefu wa km 5,000 ndio ziko kwenye maandalizi ya kujengwa, sasa sijui hiyo km 14, 000 umeitoa wapi!
Nimesema kwa mujibu wa waziri magufuli, hadi sasa tuna barabara za lami zinazofikia km 5,000. Hapo kwenye km 5,000 unazungumzia barabara zote alizojenga Nyerere, Mwinyi, Mkapa na alizomalizia Kikwete kutoka kwa mkapa. Na ni ukweli uliodhahiri kwamba Mkapa ndiye kajenga barabara nyingi za lami unazomsifia kikwete. Kama unataka kumsifia kikwte kwamba ndiye kajenga, subiri 2015 atakapokuwa ameondoka madarakani, na kama hizo ambazo ziko kwenye mobilization stage zitakuwa zimekamilika, kwakuwa tumewazoea mnapeleka wakandarasi site bila kuwalipa kwa ajili ya kujitafutia sifa za kijinga na umaarufu wa bei chee, lakini mwisho wa siku wanaishia kuondoka na barabara kubaki na mahandaki kama kawaida.
Narudia kusema kwenye barabara kikwete hawezi kuchukua credit yoyote hadi hapo atakapokamilisha miradi aliyoianzisha mwenyewe! wala usimtafutie kusifiwa kwa kazi nzuri ya Ben Mkapa.