Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Pasco,

..u have very good points.

..lakini nadhani huenda uliweka matumaini makubwa mno wa CDM, tena ktk mambo ambayo hawana uwezo nayo.

..hivi umejiuliza kwanini imefika mahali KANUNI ndiyo zitumike kuupinga mswada wa katiba na siyo HOJA zenye uzito?

..binafsi nadhani njia nzuri ya kuboresha mswada wowote ule ni kupitia HOJA na MAPENDEKEZO mbadala na siyo kanuni.

..kanuni can only buy u sometime, lakini at the end of the day, mswada unaboreshwa kupitia maoni, na zaidi unapitishwa kwa kura za wabunge.

NB:

..nasisitiza kwamba hoja zako ni nzuri ktk kutoa "somo" kuhusu masuala ya kanuni za bunge. wasiwasi wangu ni kwamba "somo" hili unalojaribu kutoa kwa CDM peke yao linaweza kutumika vibaya na kuwa upenyo wa kutokea kwa wale ambao hawakufanya kazi kwa maslahi ya taifa hili, yaani Raisi, Mwanasheria Mkuu,na Waziri wa Sheria.

..ukitaka kujua kwamba Raisi hana nia njema ni pale alipoamua kuwadanya wazee wa DSM, watu wazima wanaoweza kumzaa, kwamba CDM walisema wataandika katiba mpya ndani ya siku 100.
Haaa! Jokakuu, JK aliposema kuhusu CDM kuandika katiba mpya ndani ya siku 100 ametumia propaganda za CDM ktk kampeni kwa kutoa hahadi ile..Kama sikosei Dr.Slaa alisema alitoa ahadi hiyo kwa hiyo akatumia kebehi hiyo kwa jeuri kwa sababu aonyeshe he is doing the right thing...
 
Kwa yote sisi Bara tumeishi ktk Udikteta na haitakuwa kazi kubwa yenye maumivu zaidi ya yale tukokwisha yazoea...Kama mlimsoma vizuri JK katika hotuba yake, mimi nawasikitikia zaidi CUF ambao kwa fikra zao wanafikiri wamefanya jambo zuri sana ktk kukubaliana na CCM kwa sababu swala la Muungano ndilo linawagusa zaidi kuliko bara. yaani kule ndiko kuna ugonvi mkubwa wa nyadhifa, nafasi ya Zanzibar ktk Muungano, sijui Uhuru na kadhalika na JK alisema wazi kabisa kwamba swala la Muungano halipo ktk picha..

Sasa ingawa wanategemea sana viongozi wao walioungana ktk muafaka lakini nachelea kusema kwamba nguvu walomkabidhi JK nina hakika kabisa kwamba CUF wamefungiwa kanyaboya. Siku watakapo lifungua na kukuta ndivyo sivyo utawaona wakianza tena kulalama na katiba... Walikuwa wapi kutoungana na upanzani?... Hilo watalifukia...
 
Mkandara,

Kwanza kwa maelezo hapo juu, samahani maana naona nilikuelewa vibaya. Mie nilijua kuwa katika hiyo hotuba, kama limewekwa pia pingamizi, basi wataliangalia na lenyewe. Kumbe wanaangalia kanuni tu kama Jokakuu alivyodadavua hapa chini. Labda tu hapa na mie niongeze swali, hivi Pingamizi linatakiwa kuwa na MANENO/MISTARI mingapi?

Kuhusu swali lako hapa chini, jibu lake lipo kwenye Video hii chini: Ntaanza kwa maelezo kama ulikuwa hujayasoma na mwisho ni Video yenyewe ambayo ukiweza sikilia tena::>>

Baada ya kusikiliza hotuba ya Tundu Lisu, anasikika kabisa akitaja Kifungu cha 86 (3) (b) na kulitaka BUNGE likatae mjadala kusomwa mara ya pili.

Pia mwisho ni kweli alikosea na kusema ".......Muheshimiwa Spika, naomba kuwakilisha." Ila baada ya sekundi chache, alirudia ujumbe wake na kusema "...... naomba kutowa hoja muheshimiwa spika."

Spika akaja na kicheko chake na kusema TL ametumia kifungu cha 86 (6) na anasema ".... Muheshimiwa TL anawasilisha hotuba maoni ya kambi ya upinzani kwa kanuni ya 86 (6). Hiyo haitowi hoja ni maoni yake na ...... hayo ni maoni ya kambi ya upinzani."

Ukifuatilia zaidi, unasikia sasa sauti ya John Mnyika akisema wazi kabisa "HOJA KUAHIRISHA BUNGE." Hoja ya kuahirisha Bunge imeandikwa kwenye kifungu hicho cha 86 (3) (b) na inaweza kutolewa na mbunge yeyote. Maadamu wabunge wote hawawezi kusema pamoja, kuna uwezekano wa wenye hoja hiyo wakachelewa, kama Mnyika.

Mkuu hicho kipande nilicho ki highlight unaweza kuthibitisha mbunge huyo ni nani ama tunaweza kupata hotuba nzima ya bunge siku hiyo...
 
Last edited by a moderator:
Duu, nimeuchelewa huu mjadala, kwanini umefungwa? Anyway kwangu mimi cdm walikosea.
 
Spika Makinda alikataa kwa kusema "TUNAPOTEZA MUDA". Ila Msomali kuja na kubwabwaja na kutukana wabunge wa upinzani hadi akaombwa afute maneno yake ni sawa kabisa. Ukimsikia jamaa wa CUF na huyu Mama Malecela, unaona heri wangelisikilizwa wapinzani. Sikiliza hadi pale Wabunge wa NNCR na wao wanasema "na sisi tunatoka".

Nafikiri Tundu Lisu na Chadema kwa ujumla walijua kuwa wakipoteza nafasi kwa kuweka pingamizi na pingamizi likapingwa, basi hawatapata tena muda wa kusikilizwa kwa namna ile ambayo alisikilizwa.

Namtaka Mama Malecela afute maneno yake kuwa "alikuwa akiwawakilisha wananchi wa Same Mashariki na si yeye...." Hivi hayo aliyokuwa akiongea, aliwauliza kweli wananchi wake na wao wakamtuma kuja kuongea maneno hayo?

This is too low. Ana bahati, Wapare ni mashemeji tu, maana ningelikuwa MCHAGA, ningelimtukana kwa jina la UTANI.
 
Funga basi zipu ya suruali kabla hujaingia kwenye baraza huku umechelewa........ Soma page zote na utafunga zipu.
Duu, nimeuchelewa huu mjadala, kwanini umefungwa? Anyway kwangu mimi cdm walikosea.
 
Mkandara,

Kwanza kwa maelezo hapo juu, samahani maana naona nilikuelewa vibaya. Mie nilijua kuwa katika hiyo hotuba, kama limewekwa pia pingamizi, basi wataliangalia na lenyewe. Kumbe wanaangalia kanuni tu kama Jokakuu alivyodadavua hapa chini. Labda tu hapa na mie niongeze swali, hivi Pingamizi linatakiwa kuwa na MANENO/MISTARI mingapi?

Kuhusu swali lako hapa chini, jibu lake lipo kwenye Video hii chini: Ntaanza kwa maelezo kama ulikuwa hujayasoma na mwisho ni Video yenyewe ambayo ukiweza sikilia tena::>>

Baada ya kusikiliza hotuba ya Tundu Lisu, anasikika kabisa akitaja Kifungu cha 86 (3) (b) na kulitaka BUNGE likatae mjadala kusomwa mara ya pili.

Pia mwisho ni kweli alikosea na kusema ".......Muheshimiwa Spika, naomba kuwakilisha." Ila baada ya sekundi chache, alirudia ujumbe wake na kusema "...... naomba kutowa hoja muheshimiwa spika."

Spika akaja na kicheko chake na kusema TL ametumia kifungu cha 86 (6) na anasema ".... Muheshimiwa TL anawasilisha hotuba maoni ya kambi ya upinzani kwa kanuni ya 86 (6). Hiyo haitowi hoja ni maoni yake na ...... hayo ni maoni ya kambi ya upinzani."

Ukifuatilia zaidi, unasikia sasa sauti ya John Mnyika akisema wazi kabisa "HOJA KUAHIRISHA BUNGE." Hoja ya kuahirisha Bunge imeandikwa kwenye kifungu hicho cha 86 (3) (b) na inaweza kutolewa na mbunge yeyote. Maadamu wabunge wote hawawezi kusema pamoja, kuna uwezekano wa wenye hoja hiyo wakachelewa, kama Mnyika.

Mkuu nimeisikia video nzima vizuri sana tu..Hata mimi nimeelewa hivyo hivyo lakini alichosema Pasco ni kwamba maelezo haya yalifuatia hotuba yake aloitoa bungeni...Huu ulikuwa ni wakati wa MAONI sio PINGAMIZI.. Pingamizi lilitakiwa kutoka kwanza na bunge lisingeendelea na mjadala. Mimi sikuwapo bungeni na kusema kweli sijui hizi kanuni zinatumika vipi na wakati gani lakini kulingana na Pasco, Kesi ikisha anza kusomwa hata iwe mahakamani huwezi kubadilisha no contest kwa kutoa maelezo yanayolenga ku plea guilty or not...

Kinachonishinda kuelewa ni kwa nini Anna Makinda alikataa mwongozo kwa wabunge wengine waliosimama na kuomba HOJA ya kuahirisha Bunge. na wala sii Mnyika tu, wengi walipiga makelele ya kuomba hoja lakini Makinda alisikika akisema hakuna HOJA..Huku akisema tuendelee na kumwita mjumbe mwingine..
1. Je wakati wajumbe wanaomba mwongozo (baada ya TL) yalikuwa makosa pia ya kanuni?..
2. Je wabunge wa CDM na NCCR wangepewa nafasi muda wowote kutoa hoja ama ndio wakati wa maoni hakuna tena nafasi ya Pingamizi...
3. Na mwisho, kama hakuna wabunge wa CCM wangeweza vipi kutoa hoja ikiwa pingamizi halikubaliwi kwa wabunge wa CDM na NCCR...

Mimi naona tujifunze zaidi kuelewa bunge letu maana haki zetu zinapotoshwa sana na mfumo wa bunge ambao kama alivyosema Jokakuu haulindi maslahi ya wananchi bali ya vyama.
 
Last edited by a moderator:
Haya haya nguvu ya UMMA - muda mfupi uliopita Mkuu wa majeshi ya EGYPT amekubali yaishe, amekubali kuundwa kwa Serikali ya kiraia ya muda ambayo itapelekea utunzi wa katiba mpya..
 
Hapana Mkandara,

Dr. Slaa na Chadema kwa ujumla, walisema kuwa WATAANZA MCHAKATO WA KATIBA ndani ya siku 100.

Kikwete kawadanganya Wazee wa DSM kuwa "Chadema walisema, watatengeneza katiba ndani ya siku 100.

Ukiangalia hiyo BOLD NYEKUNDU, hapo ndipo uongo ulipo au Propaganda ilipo.

Hii habari ya EGYPT, ni habari nzuri sana kwani inatupa hata sisi mwanga kuwa katiba nzuri ya Wananchi inaweza kabisa kupatikana. Watauwa raia kadhaa na siajabu nikawa mmoja ya waliouawa au kujeruhiwa. Ila mwisho wa siku kama TUKIDAI haki yetu, hakuna Mjeshi yeyote ATATUNYIMA.

HAKI INADAIWA NA HAIOMBWI.
Haaa! Jokakuu, JK aliposema kuhusu CDM kuandika katiba mpya ndani ya siku 100 ametumia propaganda za CDM ktk kampeni kwa kutoa hahadi ile..Kama sikosei Dr.Slaa alisema alitoa ahadi hiyo kwa hiyo akatumia kebehi hiyo kwa jeuri kwa sababu aonyeshe he is doing the right thing...
 
Yah nakuelewa sana mkuu wangu narudia tu maneno ya JK kama alivyotaka wazee waelewe...

Duh, Mkuu wa majeshi ya EGYPT amekataa kujiuzulu. Ngoma imebadilika sasa hivi watu wanataka yeye aondoke.. maanadamano ni makubwa sana yaani sijui kama kuna amani tena.. watu wamezidikuwa na hasira hata baada ya kuvunja kwa baraza la muda. Wanajeshi bana huwa hawajifunzi kuachia madaraka kilaini..
 
Naomba ipitie ile update 3 kwenye maandishi mekundu.

Baada ya hotuba ya mtoa hoja, serikali, mbunge yoyote atasimama na spika atakampa nafasi, atatangulia kusema yale maneno kwenye red. Spika atasimamisha kila kitu na kusikiliza hilo pingamizi na sababu za pingamizi hilo.
Naomba kama kumbukumbu yangu haiko sawa nisahihishwe.. Siku ile Mnyika
alisimama mara mbili, baada ya kombani kumaliza na baada ya Lissu kumaliza... Alitakiwa afanyeje zaidi??!
 
Mkuu hicho kipande nilicho ki highlight unaweza kuthibitisha mbunge huyo ni nani ama tunaweza kupata hotuba nzima ya bunge siku hiyo...

Mkuu, sikumbuki alikuwa ni nani. Sina hakika ila ilisikika sauti: "Mwongozo wa spika kuhusu kuahirisha bunge..." Kupata uhakika zaidi nasubiri vijana waliokuwa kuwa bungeni siku hiyo nadhani wataweza kusema alikuwa nani. Nipe muda kidogo...
 
Kuna mawili, aidha hukusoma ama hujui kabisa hesabu ama la ulisoma na ukapata zero.

Kama tuna barabara za lami zinazofikia urefu wa km 5,000 na kuna wakandarasi wanajiandaa kuanza ujenzi ili tufikishe barabara zenye urefu wa km 10,000 hapo ni kusema takribani barabara za urefu wa km 5,000 ndio ziko kwenye maandalizi ya kujengwa, sasa sijui hiyo km 14, 000 umeitoa wapi!

Nimesema kwa mujibu wa waziri magufuli, hadi sasa tuna barabara za lami zinazofikia km 5,000. Hapo kwenye km 5,000 unazungumzia barabara zote alizojenga Nyerere, Mwinyi, Mkapa na alizomalizia Kikwete kutoka kwa mkapa. Na ni ukweli uliodhahiri kwamba Mkapa ndiye kajenga barabara nyingi za lami unazomsifia kikwete. Kama unataka kumsifia kikwte kwamba ndiye kajenga, subiri 2015 atakapokuwa ameondoka madarakani, na kama hizo ambazo ziko kwenye mobilization stage zitakuwa zimekamilika, kwakuwa tumewazoea mnapeleka wakandarasi site bila kuwalipa kwa ajili ya kujitafutia sifa za kijinga na umaarufu wa bei chee, lakini mwisho wa siku wanaishia kuondoka na barabara kubaki na mahandaki kama kawaida.

Narudia kusema kwenye barabara kikwete hawezi kuchukua credit yoyote hadi hapo atakapokamilisha miradi aliyoianzisha mwenyewe! wala usimtafutie kusifiwa kwa kazi nzuri ya Ben Mkapa.

Magufuli sasa hivi ITV anaoneshwa akifunguwa ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mayamaya Dodoma.: Kilomita 11,600 wakati huu wa Kikwete Tanzania nzima ama zimeshaanza kujengwa ama mikataba imesha sainiwa, ni nyingi kuliko nchi yoyote ya Afrika kwa sasa, 80% ya gharama kutoka bajeti ya ndani.

Sasa hizo elfu tano zako ulizitowa wapi? Hivi kwanini mnapenda kudanganya hata kwenye ukweli? tena amesema wale wanaopenda kuandamana waandamane kwenye barabara za lami.
 
Huyo Mwita kazi yake ni kusema uwongo...JK is above all presidents hawataki hilo...wanataka wale wenzao..
 
Kwasababu madai ya Pasco yalikuwa ni kwanini CDM hawaku exhaust ile procedure ya kupinga muswada kwa kutumia kifungu cha 86,nimeona kama madai yake kuhusu hiyo mistake ya CDM ni ya ukweli kwakuwa wapenzi na wanachama wa CDM walipingana naye kwa kusema mwishowe Speaker ndiye mwamuzi kwani anaweza kuitisha upigaji kura miongoni mwa wabunge,na kwasababu wabunge wa CCM ni wengi zaidi,basi waka assume kuwa hawatafika mahali...Pia kuna waliosema ni jambo ambalo lilishawahi kutokea huko nyuma.

Swali linakuja,je hakuna nyakati ambazo upinzani umefanya kikao na rais?CUF walishawahi kuwa na viao vya aina hiyo pia wakati wa Mkapa...

Kwa upande mwingine,CDM wameomba kuonana na Mh Rais,je hilo lina tofauti gani na situation iliyopita ya kujaribu kuupinga muswada bungeni pale walipokuwa na opportunity hiyo bila kujali kama watafanikiwa ama la?Given ukweli wa wazi kabisa kuwa JK hawezi kula matapishi yake?

Je kama ni kweli kuna wapenzi wa CDM humu wanadai kuwa hata akikataa basi CDM itatumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia ila "akaweka pamba masikioni"

Je kwanini hawakutumia standards hizo hizo wakati walipokuwa bungeni ili waje kuwaambia wananchi kuwa tulimwambia spika na bunge lakini "wakaweka pamba" masikioni?

Mimi siendi all the wa kuwaambia kwamba mkubali yaishe kama Pasco alivyosema, kwamba muwaachie CCM waandae utaratibu wa kupata katiba mpya,however nakubaliana na Pasco kwamba that was a mistake.

Kama nikizichukulia hizi issue within the same standards,then ni kweli CDM walikosea.

So Pasco was definetly right...

Kama walijuwa hoja yao haitashinda bungeni, ni nini kinawafanya wadhani kuwa itapita kwa Rais?

Ni vigezo gani?Binafsi siamini kabisa kuwa Rais atabadili mawazo kwenye kikao hicho,just kama vile ambavyo wao hawakuamini kwamba hoja yao itafanikiwa bungeni, kwani whats the diference?
 
JMushi1, Nijuavyo mimi CDM wancxhokifanya ni wajibu wao kwa maslahi yako wewe mwananchi. Hawana ulazima kama chama kwenda kukutana na JK zaidi ya maswala ya uchaguzi ambayo kuna dalili kubwa CDM wakazizoa kura za wananchi mwaka 2015. Aws a fact CDM inawasaidia CCM kufufuka hasa pale JK atakapoweza kuwapatia wananchi katiba bora..

Kama kulikuwepo na makosa Bungeni yamefanywa na Spika kwa makusudi kabisa kukataa HOJA za wabunge ambao walitaka bunge liahirishwe na kwa jeuri alisema hakuna HOJA kwa kila aliyedai mwongozo!..Kwa hiyo, tusonge mbele kila siku huja na mema zaidi na huu sio mwisho wa kuendeleza madai yetu iwe CDM au NCCR- Mageuzi hawa wote ni watumishi wa Umma kama alivyo rais wetu.

Na muhimu kwanza tukumbuke kwamba JK ni rais wa nchi na kila analofanya ni kwa maslahi ya Taifa hata kama anakosea wenye kuathirika ni sisi sio CCM wala CDM kwa sababu hawa wote ni binadamu na maamuzi mabaya yanaweza pia athiri maisha yao wakiwa ndani ya chama au nje....
 
Back
Top Bottom