Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Nadhani inabidi utafakari zaidi matumizi ya hizi kanuni, kanuni kuruhusu kuweka pingamizi haimaanishi pingamizi kukubaliwa, mwisho wa yote walio wengi ndio wanaokubali pingamizi kupita au la. Nadhani suala la muhimu hapa ni uwepo wa nia thabiti ya kuandika katiba yenyewe au kufanya vinginevyo vyovyote wanavyotaka. kwa waliomsikia rais akiwahutubia wazee (wanaoitwa wazee wa Dsm), mantiki nzima aliyoielezea katika uandishi wa katiba (inayoitwa mpya) inachanganya kidogo, nadhani nia dhahiri waliyo nayo katika serikali siyo kuandika katiba mpya kama wengi wanavyodhani, bali kitachofanyika ni kuifanyia marekebisho hii iliyopo katika maeneo wanayodhani hayatakuwa na athari (kwao) na pia kuitafutia uhalali kwa kura ya maoni! na si vinginevyo
 
sulphadoxine, ili mjadala huu uishe, lazima tutafika mahali tukubaliane kutokubaliana, mimi nasema Chadema walikosea. Sheria ikishasainiwa nakuhakikishieni, there is nothing Chadema can do!.

Dawa ni kukubali walikosea.
Aaaaaah hoja haiwezi kumalizwa kienyeji kwa namna unavyofikiri wewe...Maana umeshindwa kueleza ni jinsi gani CDM wamekosea na badala yake unaweka terms za kuudhi tu mara sijui manazi wa CDM,,Wanawaona viongozi wao watakatifu...Acha hizo kama ulileta hii topic maji yakiwa yako kichwani sasa yameisha fafanua ni kwa namna gani CDM Ingeweza kuokoa huu muswada usisomwe kwa mara ya pili pale bungeni.
 
Ngongo,
Siasa za chadema kwako na Pasco ni kina kirefu,hamuwezi kuziogelea na mkijaribu tu lazima mzame. Na hapa pasco ameshazama sasa amebaki anatapa tapa.
Chadema ilipowatimua madiwani wasaliti alikuja na hoja kama hii na wewe ukamuunga mkono kama kawaida lakini sasa kiko wapi? Ni kweli chadema si malaika lakini katika hili pasco amechemka tena vibaya.
Mwita Maranya,
Chadema ni kama mtoto mtukutu, wazazi wanaompenda mtoto wao kwa dhati, watamkanya tena kwa kumchapa bakora haswa, wale wazazi wengine ambao humchelea mwana kulia, mwisho wa siku, watalia wao.

Kunauwezekana kwa sisi tunaorodhesha mapungufu ya Chadema, ndio kinakisaidia chama zaidi, kuliko nyie mnaokipigia nyimbo za sifa na mapambio!.
 
Mwita Maranya, ubishani wetu mkubwa humu ni jee TL alifanya alichopaswa kufanya kwa mujibu wa kanuni?.
Hoja yangu nimewaambia alikosea, kanuni inayo sehemu ya kutoa pingamizi na kutoa sababu ambayo TL hakuitumia, na badala yake, akatoa hotuba yake kukamilisha process!.

Kama na wewe umo kwa ile ile ya viongozi wetu ni watakatifu, tangu mwanzo nimewaambia, kama mambo yenyewe ndio haya, msije humu kutulilia, 2015 sio mbali!

Pasco,
Hii nchi ni yetu sote kwahiyo tunahaki ya kusikilizwa, hata kama ccm wako wengi bungeni hicho si kigezo cha kuendesha bunge wanavyotaka na wakichemka tutawaambia tu.

Hiyo paragraph ya mwisho inadhihirisha kwamba wewe si mwenzetu, kwakuwa unajua tutakuja kukulilia wewe chama twawala hapo 2015! Na bado unasema wewe ni independent?!
 
@Pasco, napingana na hoja ya kwamba CHADEMA wamekosea:
1. Kama umesoma huu muswada na kuuelewa vizuri (nasisitiza kama umeuelewa huu muswada between the lines) utagundua CCM wameshaamua katiba iweje na hofu yao ya kuupeleka kwa wananchi ni kwa sababu watu wangefumua kila kitu!. hilo moja

2. Kama umemsikiliza Lissu, mambo aliyosema bungeni kwa niaba ya kambi ya upinzani ndiyo hayo hayo anayesema sasa. Na leo hii kasema pia alitoa hoja zote hizo kwenye kamati ya bunge ambayo yeye ni mjumbe. Lakini tunajuwa mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa kamati hii ya katiba na sheria ni wabunge wa ccm wa VITI MAALAM na wako pale kwa kazi MAALUM = kusimamia katiba ya CCM na sio katiba ya watanzania wengine!

3. Baada ya hotuba ya Mh Lissu mwakilishi wa kambi ya upinzani, Mnyika alisimama kutoa hoja ya kutaka kusitisha mjadala ili hili swala lirudi kwa wananchi lakini Spika wa CCM (wanamuita spika wa bunge) wazi wazi akakataa kusikiliza. Na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa mambo huko Dodoma CCM walishaamua huu muswada utasomwa kwa mara ya pili.

4. Kwa mtindo wa uendeshaji wa bunge chini ya spika Makinda ni vigumu sana tena sana kwa CHADEMA kushinda hoja ambayo imeshaamuliwa na CCM. Nadhani unajua mtindo wa 'sasa nitawahoji' na wengi wape. Statistically wabunge wengi ni CCM na sasa wameungana na CUF hivyo kwa vyoyote vile wawili hawa wakishakubaliana kupitisha hoja CHADEMA wanashindwa kwa sababu ya uchache wao. Tuliona wakati wa hoja ya Lissu ya kutoruhus mhimili mmoja (serikili/wakuu wa wilaya/mkoa) kusimamia nidhamu ya mhimili mwingine (mahakama). Pamoja na kwamba ni kinyume cha mgawanyo wa madaraka nchi hii CCM walipitisha hii hoja. Hivyo kusema kuwa Lissu na wenzake toka CHADEMA wangeweza kusitisha muswada huu bungeni kwa kutumia kifungu ni ndoto za mchana. Mtindo wa sasa ni wabunge wanahojiwa na wengi wape. ZIPPED!

5. Kususia kwa CHADEMA- watu wanaweza kubeza na kuona kuwa ni kazi bure! Nahisi unasema haya kwa sababu ulikuwa Dodoma lakini ungekuwa huku mtaani utagundua CHADEMA wanafanya 'people's politics'. Wanaonekana kugusa hisia za wananchi wa kawaida.Wanasoma alama za nyakati. Chama chochote cha kisiasa kinaposhindwa kujua hisia za wananchi ziko vipi kinajitafutia balaa. CCM wanaendeleza siasa za 'kuwaamulia wananchi' lakini wasilo tambua wananchi wa sasa (ambao wengi ni vijana) wanataka waamue hatma ya maisha yao wenyewe baada ya kuchoshwa na mfumo butu unaowanufaisha wachache.

6. Huu muswada umejaa makengeza na CHADEMA wanajua exactly makengeza yote yako wapi, na wana uwezo wa kueleza (articulate) kwa wananchi. Hadi sasa CCM hawajadili huu muswada wameamua ku-advertise Lissu pamoja na kuanika uwezo wao wa kutukana! Na hii itawapa wananchi hamu ya kusikia CHADEMA wakichambua muswada maana wabunge wa ccm wamepoteza hiyo opportunity (siku 4 ya mipasho).

6. Kwa nini wananchi wanawasikiliza zaidi viongozi wa CHADEMA? Wamepatwa na wazimu?

7. Lakini swali muhimu kabisa ambalo CCM wanatakiwa wajiulize ni hili: CHADEMA ni nani? Ni Lissu? Ni Dr. Slaa? Ni wabunge wa CHADEMA kwa ujumla wao? Who is CHADEMA?

Kwa maoni yangu, kitendo cha wabunge wa CHADEMA kutoka nje kimeufanya huu muswada uwe haramu kuliko mbele ya wananchi. Safari ndio imeanza na bila haya ya kuwa na nguvu za Sheikh Yahya CCM wana kazi nzito kama sio kaburi na huu muswada.

Nimependa majibu haya kwani yametoa ufafanuzi mzuri sana. Ukweli utaonekana tu. Dhambi ya ushabiki wa wabun
ge wa ccm kwenye suala hili la mchakato wa uundwaji katiba mpya itawatafuna wao wenyewe 2015. Katiba si jambo la kufanyia mzaha hata kidogo,wanaweza kufanya ushabiki kwa wake zao au waume zao, lakini si kwa jambo hili linalogusa maisha ya kila mtanzania.
 
Nadhani inabidi utafakari zaidi matumizi ya hizi kanuni, kanuni kuruhusu kuweka pingamizi haimaanishi pingamizi kukubaliwa, mwisho wa yote walio wengi ndio wanaokubali pingamizi kupita au la. Nadhani suala la muhimu hapa ni uwepo wa nia thabiti ya kuandika katiba yenyewe au kufanya vinginevyo vyovyote wanavyotaka. kwa waliomsikia rais akiwahutubia wazee (wanaoitwa wazee wa Dsm), mantiki nzima aliyoielezea katika uandishi wa katiba (inayoitwa mpya) inachanganya kidogo, nadhani nia dhahiri waliyo nayo katika serikali siyo kuandika katiba mpya kama wengi wanavyodhani, bali kitachofanyika ni kuifanyia marekebisho hii iliyopo katika maeneo wanayodhani hayatakuwa na athari (kwao) na pia kuitafutia uhalali kwa kura ya maoni! na si vinginevyo
tempo_user1, kanuni ni rules of the game, hazihitaji kufanyiwa tafakari wala tafakuri, zinahitaji kufuatwa tuu, "rules must be obeyed" Mh. TL hakufuata kanuni, Chadema lost, na sio Chadema, wapenda demokrasia ya kweli wote pia wamewaangusha!.
Kama kanuni ilihitaji pingamizi, kwa nini Chadema hawakuweka pingamizi?. Au ndio walitafakari wakaona bora waendelee?.
 
Mwita Maranya,
Chadema ni kama mtoto mtukutu, wazazi wanaompenda mtoto wao kwa dhati, watamkanya tena kwa kumchapa bakora haswa, wale wazazi wengine ambao humchelea mwana kulia, mwisho wa siku, watalia wao.

Kunauwezekana kwa sisi tunaorodhesha mapungufu ya Chadema, ndio kinakisaidia chama zaidi, kuliko nyie mnaokipigia nyimbo za sifa na mapambio!.

Chadema si chama cha malaika kwahiyo kukosea si jambo la ajabu.

Tatizo la ''mzazi'' wewe unachapa bakora hata pasipo na kosa. Halafu unalazimisha kwamba mtoto amekosa, hapa lazima mzazi ndiye gaidi!
 
Nadhani inabidi utafakari zaidi matumizi ya hizi kanuni, kanuni kuruhusu kuweka pingamizi haimaanishi pingamizi kukubaliwa, mwisho wa yote walio wengi ndio wanaokubali pingamizi kupita au la. Nadhani suala la muhimu hapa ni uwepo wa nia thabiti ya kuandika katiba yenyewe au kufanya vinginevyo vyovyote wanavyotaka. kwa waliomsikia rais akiwahutubia wazee (wanaoitwa wazee wa Dsm), mantiki nzima aliyoielezea katika uandishi wa katiba (inayoitwa mpya) inachanganya kidogo, nadhani nia dhahiri waliyo nayo katika serikali siyo kuandika katiba mpya kama wengi wanavyodhani, bali kitachofanyika ni kuifanyia marekebisho hii iliyopo katika maeneo wanayodhani hayatakuwa na athari (kwao) na pia kuitafutia uhalali kwa kura ya maoni! na si vinginevyo
Naungana nawe mia kwa mia, tulishatoa angalizo mapema huko kuwa hii inaweza kuwa ni nia ya kutaka kurekebisha katiba kuruhusu mabadiliko ya yaliyotokea Z'bar kwa mgongo wa katiba mpya.
 
nilitatazama mchakato wote kupitia tbc lakini nilichokiona na kusikia wabunge waliobaki mjengoni walikuwa wanajadili hotuba ya tindu lisu zaidi ya 95% ,sasa nini mawazo yako nani alikuwa zaidi? na kwa nini hawakujadili mswaada kwa kina badala yake wakajadili hotuba ya lisu kuanzia mwana sheria na waziri wa sheria wote wanatukana kama utakumbuka rage alisema wahuni mpaka spika akamwambia afute kauli ,wengine ooo lisu mchochezi anataka kuvunja muungano,
hatuwezi kusonga mbele tunarudi nyuma pasco sijui unaweza kunijibu haya ili tusonge mbele ni kweli tukinunua vitu used ,kama ndege na treni au kama unakumbuka tulikuwa na ndrge mpya ngapi ,viwanda vingapi vyama vya ushirika kina shirecu ,uda. viwanda vya nyama nguo aaaaaaagh au wewe unaona maendeleo ni hayo magorofa na magari used toka japan? aibu yako kushabikia vitu vya hovyo hovyo sikutegemea mtu kama wewe huna mtazamo wa maendeleo ya jumla....miji mibovu haipimiki bora enzi za ukoloni weupe kuliko nyie weusi
 
Mwita Maranya,
Chadema ni kama mtoto mtukutu, wazazi wanaompenda mtoto wao kwa dhati, watamkanya tena kwa kumchapa bakora haswa, wale wazazi wengine ambao humchelea mwana kulia, mwisho wa siku, watalia wao.

Kunauwezekana kwa sisi tunaorodhesha mapungufu ya Chadema, ndio kinakisaidia chama zaidi, kuliko nyie mnaokipigia nyimbo za sifa na mapambio!.
Pasco naona upo kwa ajili ya kubishana ila si kusikiliza hoja zinazotolewa na upande mwingine,Mzee Mwanakijiji kakupa maelezo mazuri sana ambapo mimi nlitegemea kama great thinker ubase kwenye hizo hoja,cha ajabu naona unaangalia upande hasi dhidi ya chadema tu,kwa nini hukosoi kitendo cha spika siku hiyo kukataa kupokea muongozo kutoka kwa Mnyka?
Je unafahamu kitu ambacho mnyika alitaka kuuliza?lets be ralistic rather than defending the other side.....kama wewe hauegemei upande wowote nlitegemea uje na hoja yenye mashiko inayopingana na maelezo hayo yaliyotolewa na wendine...kumbuka jamii forums ni sehemu ya kuelimishana...tusiwe kama Faiza Foxy ambaye huwa anaongea propaganda muda wote.
Work on that my brother.
 
Ngongo,
Siasa za chadema kwako na Pasco ni kina kirefu,hamuwezi kuziogelea na mkijaribu tu lazima mzame. Na hapa pasco ameshazama sasa amebaki anatapa tapa.
Chadema ilipowatimua madiwani wasaliti alikuja na hoja kama hii na wewe ukamuunga mkono kama kawaida lakini sasa kiko wapi? Ni kweli chadema si malaika lakini katika hili pasco amechemka tena vibaya.

Tena nakumbuka vizuri jinsi alivyokuwa akitabiri kuwa wanachama na wapenzi wa CDM Arusha wataawadhibu,leo hii Pasco hataki hata kugusia suala la madiwani Arusha baada ya kila kitu kwenda kinyume na utabiri wake,na kwa hili la katiba soon or later atakuja gundua anachokiamini sicho!
 
Pasco,
Sitaki kuamini kwamba umetumwa na mtu ama chama fulani, naamini kwamba hii ni hoja yako mwenyewe kwa mtazamo wako mwenyewe.

Je umefanikiwa kuisoma hotuba ya TL? NA UMEONA KWAMBA HAKUTOA HOJA KWA KANUNI HIYO UNAYOISEMA? Je ulitazama bunge siku hiyo? Je uliwaona wabunge wa chadema wakisimama kuunga hoja mkono? Je uliwasikia wabunge wakijaribu kuomba mwongozo wa spika lakini akakataa? Hebu nijibu hayo maswali ili twende pamoja.
Mwita, tafuta thread ya hotuba ya TL usome comments zangu!.

Sio tuu nilitazama bunge siku hiyo, natazama bunge kila nipatapo nafasi na siku moja moja uchumi ukiruhusu, huwa natinga kabisa mjengoni. Siku hiyo nilitazama, soma hiyo kanu ya 86 ujue TL alipaswa kusema nini, utaona ni wakati gani muongozo wa spika unaruhusiwa kuombwa, na ni wakati gani, there is no room ya muongozo wa spika, utaelewa na tutakwenda pamoja!.
 
Pasco naona upo kwa ajili ya kubishana ila si kusikiliza hoja zinazotolewa na upande mwingine,Mzee Mwanakijiji kakupa maelezo mazuri sana ambapo mimi nlitegemea kama great thinker ubase kwenye hizo hoja,cha ajabu naona unaangalia upande hasi dhidi ya chadema tu,kwa nini hukosoi kitendo cha spika siku hiyo kukataa kupokea muongozo kutoka kwa Mnyka?
Je unafahamu kitu ambacho mnyika alitaka kuuliza?lets be ralistic rather than defending the other side.....kama wewe hauegemei upande wowote nlitegemea uje na hoja yenye mashiko inayopingana na maelezo hayo yaliyotolewa na wendine...kumbuka jamii forums ni sehemu ya kuelimishana...tusiwe kama Faiza Foxy ambaye huwa anaongea propaganda muda wote.
Work on that my brother.
Makamuzi nakubali udhaifu wa kutojibu hoja za msingi, nimejikuta naanza kujibu recent comments huku nikirudi nyuma, nakubali sasa narudi mwanzo kuanza kuzijibu zile hoja zilizotangulia.
Makamuzi asante kwa angalizo hili, tuendelee kukamua.
 
Twende kwenye muswada wenyewe tusije tukawa kama bunge lililoacha kujadili muswada likaijadili cdm!
Je mnaona mamlaka aliyopewa raisi kuwa ni sawa katika nchi inayotegemewa kujenga demokrasia?
Kifungu cha 5: Raisi ataanzisha hiyo tume
Kifungu cha 6(1): Raisi atawateua wajumbe wa hiyo tume
Pamoja na vigezo vya kuteua wajumbe wa tume kuwekwa, bado kifungu 6(3)(e) kinamruhusu huyo raisi kuweka vigezo atakavyoona inafaa! Ukisoma vyema kifungu hiki cha 6 ni wazi tume itakuwa ni ya rais; ni vyema ingeitwa the presidential commission of...
Kifungu cha 8 raisi ndiye ataiambia hiyo tume nini cha kufanya (hadidu za rejea). Hakuna wa kuhoji!
Kifungu cha 13 kinaanzisha secretariat ya tume, katika kifungu cha 13(2) raisi anamteua katibu.
Madaraka ya hatari ni kifungu cha 20:
20(1) raisi atateua bunge la katiba (constituent assembly), wajumbe wa bunge hili tunaowajua ni mawaziri wa masuala ya sheria na katiba wa Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar na mwanasheria wa serikali ya Tanzania (mteule wa raisi) na yule wa Zanzibar-20(2). Wajumbe wengine wote watateuliwa na raisi kwa kujibu wa 20(3) -Hakuna wa kuhoji uteuzi wa mtu yeyote!
Kifungu cha 27: kura ya maoni itaendeshwa na tume ya uchaguzi ambayo mwenyekiti wake huteuliwa na raisi!

Hivi kweli watanzani wenzangu hapo mnatarajia mpate katiba ya wananchi au katiba ya raisi?

Mwita, tafuta thread ya hotuba ya TL usome comments zangu!.

Sio tuu nilitazama bunge siku hiyo, natazama bunge kila nipatapo nafasi na siku moja moja uchumi ukiruhusu, huwa natinga kabisa mjengoni. Siku hiyo nilitazama, soma hiyo kanu ya 86 ujue TL alipaswa kusema nini, utaona ni wakati gani muongozo wa spika unaruhusiwa kuombwa, na ni wakati gani, there is no room ya muongozo wa spika, utaelewa na tutakwenda pamoja!.

@Pasco, naomba niweke tena sehemu ya kifungu cha 86 ambacho ndio msingi wa hoja yako. Soma taratibu then naomba utupe tafsiri ya kipengele cha nne (in red & underlined) hapo chini.

86.-(1) Siku ambayo Muswada wa Sheria uliokwisha kujadiliwa na Kamati umepangwa kwenye Orodha ya Shughuli, Waziri,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kamati au Mbunge mwenye Muswada husika atawasilisha hoja kwamba Muswada wa Sheria ambao atautaja kwa jina Kusomwa Mara ya Pili.
(2) Hoja ya Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Pili itakuwa
kama ifuatavyo:-
“Kwamba, Muswada wa Sheria uitwao….. sasa usomwe mara ya pili”. Au kadri itakavyokuwa; “Kwamba, Muswada uitwao ……………… kama ulivyorekebishwa kwa mujibu wa jedwali la marekebisho au kama ulivyochapishwa upya sasa usomwe mara ya Pili.”
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:-
(a) mabadiliko bila kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema: “Kwamba, Muswada huu usisomwe mara ya Pili sasa na badala yake usomwe baada ya ….. kuanzia …..”, na hapo muda ambao Muswada huo unaokusudiwa kusomwa utatajwa.

(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema: “Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….”, na hapo sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya Pili zitatajwa kwa ukamilifu.
(4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii, Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.
 
Kwa jinsi mchakato mzima wa kuwasilisha mswaada jinsi ilivyokuwa ilikuwa ni lazima upite kwa kutumia wingi wa wabunge wa ccm, so hapa mimi sioni pointi ya Pasco kama ingeweza kufanya kazi, kutokana na uhalisia wa mazingira ya bunge la JMT ambalo linahodhiwa na CCM, wanachotakiwa CDM ni kuja na plan B as an alternative kwa wote ambao hawajaridhika na kilichopitishwa na ccm,
 
pasco upo sahihi sana na cdm wameona kosa lao,tatizo ni kukubali TL amekosea.Ni kweli waweza somea sheria na ukashindwa kutetea sheria. Endelea kuwapa shule ya bure.wengi washaelewa wamebaki wachache,endelea nao wataelewa tu
 
Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?
Mzee Mwanakijiji, kwa kutumia kifungu hicho na maneno hayo yaliyoandikwa kwenye hicho kifungu, Spika angeusimamisha mchakato right away na kusikiliza hoja za Chadema. Hayo TL aliyoyaweka kwenye hotuba yake, alipaswa kuyaweka kwenye pingamizi. Maadam hoja yangu ni kwanini Chadema hawakuwasilisha pingamizi, kama lingepita au la, hawakusimamisha, hii ni missed opportunity, imepita, nimesema hili lilikuwa kosa!. Mimi nimesema, alichofanya Mhe. Tundu Lissu sicho!, kuna kitu alichopaswa kufanya, hakufanya, na badala yake, hicho alichofanya ndicho kilichofanya muswada uendelee kujadiliwaKwa vile wengi humu wanaona alichofanya TL ndicho, wengi wape, ili mjadala uishe, nasisitiza Chadema wamefanya makosa, watakao yaona na wayaone, wasio yaona na tuendelee.

Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia. .
Kitendo cha Chadema kutowasilisha pingamizi was a mistake, kitendo cha kuususa jumla majadiliano ya bungeni, hivyo sheria kutunga bila imput ya vichwa makini vya Chadema, kwangu mimi its a loss, ila kama kwa wengine huo ndio ushujaa, na wanaoamini na kuusupport ushujaa huu ni wengi, wengi wape, Chadema ni mashujaa na kwenye hili wamagain, na tusubiri jinsi Chadema watakavyoitumia gain yao hii wakati sheria imeshatungwa!.

Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza. .
Mzee Mwanakijiji, kumbe utiii wa sheria unahusisha kuzitii tuu zile sheria zilizotugwa legitimately?!. Kwa hiyo inaruhusiwa kuwahamasisha wafuasi wenu wasusie ilegitimate laws!. Nimewashauri kubalini yaishe, tusonge mbele, tumeikishateuliwa tuipe ushirikiano, ila kama mnaamini bado mnayo hiyo option, mwisho wa siku the end will justify the means, na 'he who laugh last, laugh most'. Mwisho wa siku tutaona nani atalia na nani atacheka!
Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM.

Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.
Kwenye ile post yangu kuwa Chadema Haijajipanga, nilielewa wazi kuwa wale wanaodhani JK ameridhia mjadala wa katiba in good faith, are wrong!. Pia nikawaambia, kama wanadhani CCM itawapatia katiba bora ili Chadema waitumie kuingia ikulu kwa mteremko, they are wrong again!, nikawaambia Chadema, mjipange ki mipango mkakati, tena nikasema CCM wanatumia delaying tactics ili hiyo katiba mpya ije baada ya bunge la Julai 2015 na itaelezwa, itaanza kutumika baada ya uchaguzi wa 2015!.

Sasa kama mtawahamasisha wafuasi wenu wasusie kutoa maoni au wapige kura ya hapana, then katiba itakaoendelea kutumika ni hii hii ya 1977 hivyo uchaguzi wa 2015, tutaufanya kwa katiba hii hii na tume ile ile!, nitawashauri kabisa Chadema pia na wasusie uchaguzi CCM itawale kote turudi kwenye ule mfumo wa Chama kimoja na pia nitashauri ile Sheria ya 'Indifinite Preventive Detention Orders' irudishwe ili nchi yetu iwe ya amani kama enzi za Nyerere!.
 
MM wewe ni miongoni mwa wapenzi wa CDM walio tayari kuburuzwa na hoja dhaifu pasipo kuhoji na kibaya zaidi unataka kuwafunga mdomo wanahoji kwa nia njema.Mkuu Pasco kaleta hoja nzuri akitegemea atapata majibu ya uhakika ninachokiona hapa ni aina ya majibu yanayokwepa swali la msingi !.

Chadema si chama cha malaika kwahiyo kukosea si jambo la ajabu.

Tatizo la ''mzazi'' wewe unachapa bakora hata pasipo na kosa. Halafu unalazimisha kwamba mtoto amekosa, hapa lazima mzazi ndiye gaidi!
 
hapana ni kwamba ana maoni tofauti na kuwa anaamini maoni yake ni sahihi. Ni jukumu letu kuonesha kuwa maoni yake si sahihi. Mtu kuwa na maoni tofauti haina maana ni mnafiki.

NO MMM, Pasco ni Mnafiki sababu anaelewa ukweli lakini anatumia uwezo wake wa kujenga hoja kupindisha ukweli.
 
Back
Top Bottom