Pasco, hivi wangetoa hoja kwa kutumia kanuni ya 86 mjadala ungesimamishwa automatically au Spika angeuliza Bunge na Bunge kuamua? Unafikiri Wabunge wa CCM wangekubali kusimamisha mjadala baada ya kuulizwa na Spika?
Mzee Mwanakijiji, kwa kutumia kifungu hicho na maneno hayo yaliyoandikwa kwenye hicho kifungu, Spika angeusimamisha mchakato right away na kusikiliza hoja za Chadema. Hayo TL aliyoyaweka kwenye hotuba yake, alipaswa kuyaweka kwenye pingamizi. Maadam hoja yangu ni kwanini Chadema hawakuwasilisha pingamizi, kama lingepita au la, hawakusimamisha, hii ni missed opportunity, imepita, nimesema hili lilikuwa kosa!. Mimi nimesema, alichofanya Mhe. Tundu Lissu sicho!, kuna kitu alichopaswa kufanya, hakufanya, na badala yake, hicho alichofanya ndicho kilichofanya muswada uendelee kujadiliwaKwa vile wengi humu wanaona alichofanya TL ndicho, wengi wape, ili mjadala uishe, nasisitiza Chadema wamefanya makosa, watakao yaona na wayaone, wasio yaona na tuendelee.
Sidhani kama wame lose; ukiangalia zaidi utaona kuwa wao wamegain kwa sababu mstari umechorwa kati ya wale wanaoamini Rais na wana CCM wanaweza kufanya yote wayatakayo na wale ambao wanaamini the CCM government is in contempt of the people. Tofauti hii ya maoni ni ya muhimu. Rais na CCM wameweza kulazimisha sheria waitakayo wao kupita - kama walivyofanya kwenye sheria ya gharama za uchaguzi - lakini mwisho wa siku watajikuta ni wao pekee ndio wanaandika hiyo Katiba mpya na wale wanaowaamini au kuwafuata. Je kwa vile sheria imepitishwa ina maana mchakato utakuwa halali kwa kuangaliai first principle? Ukweli ni kuwa CCM hawakuhitaji hoja za CDM au za mtu mwingine yeyote juu ya mswada huu, walikuwa na mawazo yao na wameyatekeleza bila kuzuiwa kwani hakukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza kuwazuia. .
Kitendo cha Chadema kutowasilisha pingamizi was a mistake, kitendo cha kuususa jumla majadiliano ya bungeni, hivyo sheria kutunga bila imput ya vichwa makini vya Chadema, kwangu mimi its a loss, ila kama kwa wengine huo ndio ushujaa, na wanaoamini na kuusupport ushujaa huu ni wengi, wengi wape, Chadema ni mashujaa na kwenye hili wamagain, na tusubiri jinsi Chadema watakavyoitumia gain yao hii wakati sheria imeshatungwa!.
Siyo lazima. Watanzania ambao hawaamini katika uhalali wa mchakato huu kwa sababu umevunja the First Principle wanaweza kuupinga, kukataa kushiriki na kuwahamaisha wengine wasishiriki kwa hoja ambazo zitaonesha kuwa mchakto mzima umekosewa toka mwanzo na haukuwa nafasi ya kufanikiwa kwa sababu ulikuwa ni wa kulazisha kwa kutumia tyranny of thte majority. Wananchi hawawezi kulazimishwa kuitii tume ambayo hawaamini ni halali. Tume kupitishwa na kuundwa hakuipi uhalali (legitimacy) kwani uhalali wa sheria hauji kwa kupitishwa tu bali pia kwa uhalali wa hoja zake na mantiki yake. Mwanadamu hawezi kulazimishwa kutii kitu ambacho ni kinyume na dhamira yake, ukweli na mantiki yake au kile ambacho kinaonekana kwa makusudi kimetengezwa ili kumkandamiza. .
Mzee Mwanakijiji, kumbe utiii wa sheria unahusisha kuzitii tuu zile sheria zilizotugwa legitimately?!. Kwa hiyo inaruhusiwa kuwahamasisha wafuasi wenu wasusie ilegitimate laws!. Nimewashauri kubalini yaishe, tusonge mbele, tumeikishateuliwa tuipe ushirikiano, ila kama mnaamini bado mnayo hiyo option, mwisho wa siku the end will justify the means, na 'he who laugh last, laugh most'. Mwisho wa siku tutaona nani atalia na nani atacheka!
Wanaoamini kuwa sheria hii ni halali na kuwa mchakato ni halali wanayo haki ya kujitokeza kwa furaha kwenda kutoa maoni yao. Wale ambao wanaamini mchakato huu umesurp power ya wananchi na kuwa umelazimishwa wanayo haki ya kukaaa kushiriki na kuhamasishana kutoshiriki hadi hoja zao zisikilizwe vinginevyo wanalo jukumu la kuhakikisha kuwa itakapokuja kura ya maoni wataenda na kuhamasishana kupigia kura ya "hapana" hiyo referendum na kuzuia Katiba Mpya itakayopitishwa na wana CCM.
Wanaweza kukataa kusikiliza maoni juu ya mchakato na wanaweza kabisa kulazimisha watu waje kwenye tume yao lakini watakapoletwa swali hilo kwa wananchi hawana namna ya kuwazuia wale wasioshiriki mjadala kupiga kura ya hapana. Unless waseme watakaopiga kura ya maoni ni WALE TU walioshiriki kwenye kutoa maoni! Kitu ambacho hakimo kwenye mswada huu hadi waufanyie mabadiliko.
Kwenye ile post yangu kuwa Chadema Haijajipanga, nilielewa wazi kuwa wale wanaodhani JK ameridhia mjadala wa katiba in good faith, are wrong!. Pia nikawaambia, kama wanadhani CCM itawapatia katiba bora ili Chadema waitumie kuingia ikulu kwa mteremko, they are wrong again!, nikawaambia Chadema, mjipange ki mipango mkakati, tena nikasema CCM wanatumia delaying tactics ili hiyo katiba mpya ije baada ya bunge la Julai 2015 na itaelezwa, itaanza kutumika baada ya uchaguzi wa 2015!.
Sasa kama mtawahamasisha wafuasi wenu wasusie kutoa maoni au wapige kura ya hapana, then katiba itakaoendelea kutumika ni hii hii ya 1977 hivyo uchaguzi wa 2015, tutaufanya kwa katiba hii hii na tume ile ile!, nitawashauri kabisa Chadema pia na wasusie uchaguzi CCM itawale kote turudi kwenye ule mfumo wa Chama kimoja na pia nitashauri ile Sheria ya 'Indifinite Preventive Detention Orders' irudishwe ili nchi yetu iwe ya amani kama enzi za Nyerere!.