Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samahani kama nimekosea inaonekana wewe nikizazi cha 2K05, mema yapi ambayo wewe unayazungumzia, kwa Wananchi wa Tanzania ama kwa ndugu na jamaa wa familia yake?Pasco umenena vyema.
Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".
Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
Ritz, hili la Chadema kutamka hawamtambui rais kwa maneno ila matendo ni the other way round, nilishalizungumzia humu na nilichokipata, wenye kumbukumbu wanakijua, nikasisitiza ukweli jamani, siku zote huwa unasimama!.Kwa kweli mimi nimewashangaa sana Chadema, na viongozi wao kwa ujumla..
Chadema walitoka bungeni baada ya rais Kikwete kuanza kuhutubia bunge la jamhuri ya Tanzania.
Chadema wakatoka bungeni huku wakisema hawamtambui rais Kikwete..
Leo tena Chadema wanaunda team ndogo wakumuone rais hawasaidie wawemo kwenye rasimu ya katibu tena Mbowe, kamuita rais Kikwete, Amiri Jeshi mkuu..
Leo tena imekuaje mnataka mkamuone rais msiomtambua hakawasaidie katika mambo ya Katiba?
Rais akisema ana nafasi mpaka 2014 mtafanyaje?
Ritz, hili la Chadema kutamka hawamtambui rais kwa maneno ila matendo ni the other way round, nilishalizungumzia humu na nilichokipata, wenye kumbukumbu wanakijua, nikasisitiza ukweli jamani, siku zote huwa unasimama!.
Kwa vile hapa tunaelimishana, kutamka humtambui rais, sio kosa kisheria, siku hiyo niliwaambia urais ni taasisi (presidential institution), inayoshikiliwa na mtu mwenye jina la JK, unaweza usimtambue JK kama JK na kumuignore unavyotaka, kukebehi, kumtukana and calling him all sort of names, lakini huwezi kuikebehi taasisi ya urais. Unaweza usimtambue JK lakini huwezi kutoitambua taasisi ya urais, maana taasisi hii ndio inayoongoza mmoja ya mihimili mitatu ya dola, hivyo niliwaambia kutamka kutomtambua ni kujifurahisha tuu nafsini mwao, ila in reality, president ana exist in real man, hivyo umtambue, usimtambue yupo!.
Uwe ulimchagua au hukumchagua maan adam aliyetangazwa mshindi ni yeye (regardless alishindaje), huyu ndiye rais wa wote including hao wasiomtambua hadi waliotoa tamko hilo!.
Mkuu Mkandara, huu mjadala tulishaufunga kwa closing points za Mzee Mwanakijiji nami niliafiki tuufunge. Lakini kwa vile lengo ni kuelimishana, naomba niweke hapa majibu yangu in points form, huenda na wengine wasio nielewa wakanielewa hivyo hii itakuwa ni closing nyingine.Pasco,
Mkuu wangu mimi nashindwa sana kuelewa haswa makosa yako wapi. Nimesoma kanuni hiyo mara kibao lakini nashindwa kuona ni wakati gani haswa inatakiwa utumike kama ilivyoandikwa na nimejaribu kurudi nyuma katika vikao vya nyuma nimekuta miswada ilipingwa hata zamani kulikuwepo na hotuba ya mwakilishi wa Upinzani..
Mimi sii mwanasiasa wala sijui utaratibu wa kanuni hizi za bunge, lakini kila naposoma kanuni hii hainipi picha unayozungumzia mkuu wangu... Ebu tuisome sote kisha nipe darasa, inasema:-
- 86 (3) Mjumbe yeyote anayetaka kutoa HOJA kwamba MAJADILIANO ya kamati ya bunge zima yaahirishwe hadi wakati mwingine, anaweza kutoa hoja hiyo wakati wowote, kwa maneno yafuatayo:-
"Kwamba Waziri (au Mbunge) anayehusika atoe taarifa kwa bunge juu ya maendeleo ya kazi ya kamati hii na kuomba ruhusa kamati hii ikutane tena baadaye..."
Sasa mkuu wangu hivi kuomba kuahirisha majadiliano kunahusiana vipi na kuupinga muswada?.. na kama TL angetanguliza kanuni hii ili mjadala uahirishwe angeweza vipi kusema yale yaliyotakiwa chini yake wakati hataki taarifa ya maendeleo ya kamati blaa...blaa.... blaaa...naomba darasa mkuu.
Kwa kuelewa kwangu, kanuni hiyo ya 86 (3) itatumika wakati wa majadiliano kuanza. TL katoa hotuba yake kabla ya majadiliano iweje alitakiwa yeye kutumia kannuni hii ili iweje... waziri gani au kikao gani kilitakiwa kutoa taarifa ya maendeleo yapi?..
Na nimepitia hotuba kadhaa za Upinzani sikuona mahala mbunge akitumia kanuni hii moja kwa moja wakati wa kupinga muswada ktk vikao vya bunge zima.
Sasa labda nitaarifu vizuri kama unavyotaka tuifate hiyo kanuni kinagaubaga... Ni wapi inaposema kanuni hiyo ndio inayokataa muswada kwa mara ya pili kwa sababu una mapungufu?
Kuanzia hapa sasa Mkuu Mkandara, naomba sasa ndio nikulete kwenye kanuni 86 kifungu cha 3.
(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema:
"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo sababu za kupinga Muswada Kusomwa Pili zitatajwa kwa ukamilifu.
maneno hayo ndio Mhe. Tundu Lissu alitakiwa ayaseme ili kuweka pingamizi kwa muswada huo, usisonge mbele. Hli ndilo pingamizi rasmi kwa mujibu wa kanuni.
Wamwombe Nani Msamaha!
Maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani chini ya Mh.tundu lissu yalikuwa Tight ile mbaya!
Wamechambua na Kudadavua Mswada ndani na nje jamaa hawa wapo safi!CCM iache kutumia msuli bora wakae na jamaa wa CDM
Vinginezo wanaweza umbuka mbele ya safari!Tupo na tuombe Uhai ili tuone
Lissu akitoa hoja ya kukataa muswada kwa kanuni ya 86 3( b ) iliyokataliwa:
Mkuu Mkandala, muswada ulishawasilishwa kwa mara ya kwanza, hivyo huo uliowasilishwa kwa mara ya pili ni muswada wenye jina lile lile japo contents zilibadilishwa. Mhe. Lissu was very right our government is playing with its people's mind.Pasco,
Mkuu wangu usijali ya Mwanakijiji... mimi nataka kupata darsa maanake ndio unanichanganya kabisaaaa..Muswada uliporudi ulikuwa ule ule isipokuwa umebadilishwa lugha tuiweje urudi tena kuwa mara ya kwanza wakati haukuwasilishwa kama muswada mpya?..Na nilimsikia JK akanichanganya ya kwamba muswada unapokabidhiwa kamati ya bunge ndio mara ya kwanza na unapotoka kwenda ktk Bunge zima huwa ni mara ya pili...sijui kama nimekosea..
Sasa pengine unaweza nambia kama muswada huu uliporudi ulianza tena process upya kama mara ya kwanza ama ulifika na kutaka kusomwa kama mara ya pili?..mimi nadhani ilikuwa mara ya pili kwa sababu sidhani kama ulichapishwa tena upya ktk gazeti na kadhalika..Yaani hizi siasa zenu jamani zinatuchanganya sisi na sii rahisi kwetu kujua kinachoendelea...
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.
Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.
Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.
Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.
Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.
Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.
Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.
Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.
Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.
Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.
Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.
Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).
Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.
2015 sio mbali kihivyo!.
Wasalaam
Pasco (wa jf).
Update 1.
Update 2.
Update 3.
Mkuu Mkandara, madam speaker was very right, Maneno hayo TL alitakiwa ayaseme kwenye 86 (3) b ni kuwasilisha pingamizi. Mkandara nakuhakikishia Hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa!.Duh! ama kweli ukweli sasa umejitokeza wazi kabisa... Pasco nakuomba msikilize TL alivyowasilisha akitaja kifungu cha 86 (3)b lakini Spika akasema TL aliwasikisha kanuni ya 86 (6)... wewe umeelewa hapo kimefanyika nini?
Dah, hizi siasa kusema kweli sii uwanja wangu kabisa... yaani TL alitakiwa kuweka pingamizi pale aliposimama mara ya kwanza kabla ya hotuba yake sio? hata kama ametaja kanuni sawa haijalishi itawekwa kifungu cha kanuni nyingine kabisa bila kuwa na maana ya kifungu alichosoma..huu ndio utaratibu wa bunge!...dah kaazi kweli kweli.....Ni wakati gani HOJA zinatolewa na ni wakati gani MAONI hutolewa..Mkuu Mkandara, madam speaker was very right, Maneno hayo TL alitakiwa ayaseme kwenye 86 (3) b ni kuwasilisha pingamizi. Mkandara nakuhakikishia Hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa!.
Alichofanya TL ni 86 -6 kutoa maoni ya kambi ya upinzani, hata kama katika kutoa maoni huko ameweka maneno pingamizi, hayo yanabaki ni maoni tuu. Pingamizi ni pingamizi likiwekwa lazima bunge linasimamisha kila kitu na kulisikiliza pingamizi lile.
Kwa kuwa hakukuwa na pingamizi lolote. process iliendelea kwa kumsikiliza M/kiti wa Kamati na baadae Maoni ya upinzani. Watu wanaamini maoni hayo ndio pingamizi!. No!. Maoni ni maoni tuu na hakukuwa na pingamizi and that was a mistake!.
Dah, hizi siasa kusema kweli sii uwanja wangu kabisa... yaani TL alitakiwa kuweka pingamizi pale aliposimama mara ya kwanza kabla ya hotuba yake sio? hata kama ametaja kanuni sawa haijalishi itawekwa kifungu cha kanuni nyingine kabisa bila kuwa na maana ya kifungu alichosoma..huu ndio utaratibu wa bunge!...dah kaazi kweli kweli.....Ni wakati gani HOJA zinatolewa na ni wakati gani MAONI hutolewa..
Sasa tuseme kuna mtu wa CCM ambaye alitaka kuuzuia muswada huo usisomwe angeweza vipi ikiwa TL ndiye ametangulia kuzungumza kwa niaba ya kambi ya Upinzani.. Kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini kosa linaitwa la CDM wakati hawa wote ni wabunge wetu sisi sote. Why only TL ndiye alitakiwa kusimamisha muswada huo..
Sasa turudi kwa wananchi kama Mama Kilango alivyosema kwamba wao ni wawakilishi wetu ingawa naye kabomoa bomoa... Kwa maslahi ya wananchi kama Spika ameona utata ktk muswada huo kulingana na hoja ya TL kwa nini asiwatumikie wananchi badala yake anamtumikia JK na chama Chake kuhakikisha upinzani hawapewi nafasi ya kusitisha muswada huo? Hivi kweli Spika akiona tatizo ktk muswada huwezi kuzuia usisomwe mara ya pili wakati wowote.. au naye aliona kikanuni kila kitu safi tu maanake navyochukulia mimi wabunge wote pale ni wawakilishi wetu inakuwaje swala hili ghafla likawa la vyama badala ya wananchi.
Dah, hizi siasa kusema kweli sii uwanja wangu kabisa... yaani TL alitakiwa kuweka pingamizi pale aliposimama mara ya kwanza kabla ya hotuba yake sio? hata kama ametaja kanuni sawa haijalishi itawekwa kifungu cha kanuni nyingine kabisa bila kuwa na maana ya kifungu alichosoma..huu ndio utaratibu wa bunge!...dah kaazi kweli kweli.....Ni wakati gani HOJA zinatolewa na ni wakati gani MAONI hutolewa..
Sasa tuseme kuna mtu wa CCM ambaye alitaka kuuzuia muswada huo usisomwe angeweza vipi ikiwa TL ndiye ametangulia kuzungumza kwa niaba ya kambi ya Upinzani.. Kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini kosa linaitwa la CDM wakati hawa wote ni wabunge wetu sisi sote. Why only TL ndiye alitakiwa kusimamisha muswada huo..
Sasa turudi kwa wananchi kama Mama Kilango alivyosema kwamba wao ni wawakilishi wetu ingawa naye kabomoa bomoa... Kwa maslahi ya wananchi kama Spika ameona utata ktk muswada huo kulingana na hoja ya TL kwa nini asiwatumikie wananchi badala yake anamtumikia JK na chama Chake kuhakikisha upinzani hawapewi nafasi ya kusitisha muswada huo? Hivi kweli Spika akiona tatizo ktk muswada huwezi kuzuia usisomwe mara ya pili wakati wowote.. au naye aliona kikanuni kila kitu safi tu maanake navyochukulia mimi wabunge wote pale ni wawakilishi wetu inakuwaje swala hili ghafla likawa la vyama badala ya wananchi.
Mkuu hata mimi najiuliza swali hili sipati jibu...Kumbe hata hicho kifungu kilinukuliwa na TL wakati wa hoja yake!
Tundu hakuwa na hoja yake. Na hapo pia unakosea.
Tundu ni mwanasheria na anajuwa maana ya kanuni za bunge na anajuwa kakosea na ingekuwa kama spika kakosea basi kuna taratibu za kibunge ambazo zingefatwa na ziko wazi kabisa, lakini kwa kuwa Tundu anajuwa kuwa kakosea ndio maana hakuweza kufata hata hizo za kanuni za kumrekebisha anapokosea.
Magwanda kwa hili halina ujanja, ni makosa makubwa sana ambayo huwezi kuyafuta kwa maneno. Kanuni ni kanuni, kesi zinatupwa mahakamani kwa sababu tu hazijafata kanuni ya aina gani ya kuandika au "Font size" tu. Sasa hapo panapotungwa sheria ni lazima ufate sheria, hata JF wana kanuni ukuzikiuka unakula ban labda "Makinda" wa JF siku hiyo awe kalewa na kakuonea. Bungeni usione tu wanaongea pale, wewe unaweza kubwabwaja tuuu kama alivyofanya Tundu lakini haikuwa na maana yoyote maneno yake, alikuwa hapingi pale alikuwa anatoa maoni yake, na maoni yake ni wanaomsikiliza ama wayakubali ama wasiyakubali lakini hayabadili kanuni za bunge.