Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!

Mwanakijiji oyeeeeee...........
Pasco chaliiiiiii.................
Kudadadadadededekiiiiiii............
 
Pasco umenena vyema.

Hawa jamaa wa magwanda hawana wakitakacho zaidi ya "shortcut".

Hata Kikwete afanye nini kwao ni kosa tu, tatizo lao ni Kikwete na si Serikali. Hilo lipo wazi kabisa, lakini ukweli ni kwamba Kikwete ndiye aliyefanya mema Tanzania hii zaidi ya Rais yeyote mwingine wa kabla yake na hilo halina utata wala ubishi. Wakae wafikiri.
Samahani kama nimekosea inaonekana wewe nikizazi cha 2K05, mema yapi ambayo wewe unayazungumzia, kwa Wananchi wa Tanzania ama kwa ndugu na jamaa wa familia yake?
 
Pasco,
Mkuu wangu mimi nashindwa sana kuelewa haswa makosa yako wapi. Nimesoma kanuni hiyo mara kibao lakini nashindwa kuona ni wakati gani haswa inatakiwa utumike kama ilivyoandikwa na nimejaribu kurudi nyuma katika vikao vya nyuma nimekuta miswada ilipingwa hata zamani kulikuwepo na hotuba ya mwakilishi wa Upinzani..

Mimi sii mwanasiasa wala sijui utaratibu wa kanuni hizi za bunge, lakini kila naposoma kanuni hii hainipi picha unayozungumzia mkuu wangu... Ebu tuisome sote kisha nipe darasa, inasema:-

- 86 (3) Mjumbe yeyote anayetaka kutoa HOJA kwamba MAJADILIANO ya kamati ya bunge zima yaahirishwe hadi wakati mwingine, anaweza kutoa hoja hiyo wakati wowote, kwa maneno yafuatayo:-

"Kwamba Waziri (au Mbunge) anayehusika atoe taarifa kwa bunge juu ya maendeleo ya kazi ya kamati hii na kuomba ruhusa kamati hii ikutane tena baadaye..."

Sasa mkuu wangu hivi kuomba kuahirisha majadiliano kunahusiana vipi na kuupinga muswada?.. na kama TL angetanguliza kanuni hii ili mjadala uahirishwe angeweza vipi kusema yale yaliyotakiwa chini yake wakati hataki taarifa ya maendeleo ya kamati blaa...blaa.... blaaa...naomba darasa mkuu.

Kwa kuelewa kwangu, kanuni hiyo ya 86 (3) itatumika wakati wa majadiliano kuanza. TL katoa hotuba yake kabla ya majadiliano iweje alitakiwa yeye kutumia kannuni hii ili iweje... waziri gani au kikao gani kilitakiwa kutoa taarifa ya maendeleo yapi?..
Na nimepitia hotuba kadhaa za Upinzani sikuona mahala mbunge akitumia kanuni hii moja kwa moja wakati wa kupinga muswada ktk vikao vya bunge zima.

Sasa labda nitaarifu vizuri kama unavyotaka tuifate hiyo kanuni kinagaubaga... Ni wapi inaposema kanuni hiyo ndio inayokataa muswada kwa mara ya pili kwa sababu una mapungufu?
 
Kwa kweli mimi nimewashangaa sana Chadema, na viongozi wao kwa ujumla..

Chadema walitoka bungeni baada ya rais Kikwete kuanza kuhutubia bunge la jamhuri ya Tanzania.

Chadema wakatoka bungeni huku wakisema hawamtambui rais Kikwete..

Leo tena Chadema wanaunda team ndogo wakumuone rais hawasaidie wawemo kwenye rasimu ya katibu tena Mbowe, kamuita rais Kikwete, Amiri Jeshi mkuu..

Leo tena imekuaje mnataka mkamuone rais msiomtambua hakawasaidie katika mambo ya Katiba?

Rais akisema ana nafasi mpaka 2014 mtafanyaje?
Ritz, hili la Chadema kutamka hawamtambui rais kwa maneno ila matendo ni the other way round, nilishalizungumzia humu na nilichokipata, wenye kumbukumbu wanakijua, nikasisitiza ukweli jamani, siku zote huwa unasimama!.

Kwa vile hapa tunaelimishana, kutamka humtambui rais, sio kosa kisheria, siku hiyo niliwaambia urais ni taasisi (presidential institution), inayoshikiliwa na mtu mwenye jina la JK, unaweza usimtambue JK kama JK na kumuignore unavyotaka, kukebehi, kumtukana and calling him all sort of names, lakini huwezi kuikebehi taasisi ya urais. Unaweza usimtambue JK lakini huwezi kutoitambua taasisi ya urais, maana taasisi hii ndio inayoongoza mmoja ya mihimili mitatu ya dola, hivyo niliwaambia kutamka kutomtambua ni kujifurahisha tuu nafsini mwao, ila in reality, president ana exist in real man, hivyo umtambue, usimtambue yupo!.
Uwe ulimchagua au hukumchagua maan adam aliyetangazwa mshindi ni yeye (regardless alishindaje), huyu ndiye rais wa wote including hao wasiomtambua hadi waliotoa tamko hilo!.
 
Pasco,
Siasa mkuu wangu mimi na wewe tuwaachie wenyewe... Mbona Mahmood Abbas alikuwa hatambuliwi, wala nchi yake Palestine haitambuliwi lakini viongozi wa nchi zote duniani walikuwa wanazungumza naye kwenye maswala ya Middle East kama rais wa Palestine na kumpa heshima zote.. Hata Afarat alikuwa nani?. Hizi ndio siasa wanasema hawatambui wakati matendo yao huonyesha heshima na kumtambua..

Kwa hiyo, CDM walijaribu walichoweza kufanya kuonyesha dhulma ilofanyika kwa wananchi na mwisho wa siku waliinua mikono na hata swala hili CDM kama chama wanatakiwa kuonyesha msimamo wao hata kama Muswada huu utapita na kuwa sheria..Jamani yote haya sii kwa ajili yao ila kwa niaba ya wewe mwananchi..Na amini maneno yangu CDM walijua toka mwanzo katiba mpya haiwezi kupatikana kwa maslahi ya wananchi - Yaani haiwezekani, lakini kisiasa ni lazima waonyeshe wamesimama wapi. Marekani leo tu bunge lao limeshindwa kupitisha muswada muhimu sana ktk uchumi wao kwa sababu kila chama kinacheza ngoma ya kisiasa wakidai kulinda maslahi ya wananchi.

CCM katu hawawezi kuibadilsiha katiba ambayo inawalinda kwa sababu ya CDM isipokuwa wananchi ndio pekee wanaweza kuwekea mkazo huo.. Ni sawa na Misri leo hii wananchi wanadai katiba mpya lakini isingekuwa kazi rahisi kwa njia za kawaida kupitia vyama. CCM leo ni watawala na lugha ya JK mwenyewe imeonyesha Mtawala aliyevaa ngozi ya kondoo maanake vitisho kwa mbali sana wakati Katiba sii yake wala ya CCM isipokuwa madai yake analinda haki alokabidhiwa na wananchi..Na sisi wananchi wenyewe hatujui kama katiba ni mwongozo wetu sote, tunatazama ugonvi wa CDM na CCM hali sisi ndio wenye mali - ELIMU ya URAIA muhimu sana mkuu wangu..
 
Ritz, hili la Chadema kutamka hawamtambui rais kwa maneno ila matendo ni the other way round, nilishalizungumzia humu na nilichokipata, wenye kumbukumbu wanakijua, nikasisitiza ukweli jamani, siku zote huwa unasimama!.

Kwa vile hapa tunaelimishana, kutamka humtambui rais, sio kosa kisheria, siku hiyo niliwaambia urais ni taasisi (presidential institution), inayoshikiliwa na mtu mwenye jina la JK, unaweza usimtambue JK kama JK na kumuignore unavyotaka, kukebehi, kumtukana and calling him all sort of names, lakini huwezi kuikebehi taasisi ya urais. Unaweza usimtambue JK lakini huwezi kutoitambua taasisi ya urais, maana taasisi hii ndio inayoongoza mmoja ya mihimili mitatu ya dola, hivyo niliwaambia kutamka kutomtambua ni kujifurahisha tuu nafsini mwao, ila in reality, president ana exist in real man, hivyo umtambue, usimtambue yupo!.
Uwe ulimchagua au hukumchagua maan adam aliyetangazwa mshindi ni yeye (regardless alishindaje), huyu ndiye rais wa wote including hao wasiomtambua hadi waliotoa tamko hilo!.

Mkuu Pasco,

Umenishibisha kwa maelezo yako makini ya uchambuzi!
 
Pasco,
Mkuu wangu mimi nashindwa sana kuelewa haswa makosa yako wapi. Nimesoma kanuni hiyo mara kibao lakini nashindwa kuona ni wakati gani haswa inatakiwa utumike kama ilivyoandikwa na nimejaribu kurudi nyuma katika vikao vya nyuma nimekuta miswada ilipingwa hata zamani kulikuwepo na hotuba ya mwakilishi wa Upinzani..

Mimi sii mwanasiasa wala sijui utaratibu wa kanuni hizi za bunge, lakini kila naposoma kanuni hii hainipi picha unayozungumzia mkuu wangu... Ebu tuisome sote kisha nipe darasa, inasema:-

- 86 (3) Mjumbe yeyote anayetaka kutoa HOJA kwamba MAJADILIANO ya kamati ya bunge zima yaahirishwe hadi wakati mwingine, anaweza kutoa hoja hiyo wakati wowote, kwa maneno yafuatayo:-

"Kwamba Waziri (au Mbunge) anayehusika atoe taarifa kwa bunge juu ya maendeleo ya kazi ya kamati hii na kuomba ruhusa kamati hii ikutane tena baadaye..."

Sasa mkuu wangu hivi kuomba kuahirisha majadiliano kunahusiana vipi na kuupinga muswada?.. na kama TL angetanguliza kanuni hii ili mjadala uahirishwe angeweza vipi kusema yale yaliyotakiwa chini yake wakati hataki taarifa ya maendeleo ya kamati blaa...blaa.... blaaa...naomba darasa mkuu.

Kwa kuelewa kwangu, kanuni hiyo ya 86 (3) itatumika wakati wa majadiliano kuanza. TL katoa hotuba yake kabla ya majadiliano iweje alitakiwa yeye kutumia kannuni hii ili iweje... waziri gani au kikao gani kilitakiwa kutoa taarifa ya maendeleo yapi?..
Na nimepitia hotuba kadhaa za Upinzani sikuona mahala mbunge akitumia kanuni hii moja kwa moja wakati wa kupinga muswada ktk vikao vya bunge zima.

Sasa labda nitaarifu vizuri kama unavyotaka tuifate hiyo kanuni kinagaubaga... Ni wapi inaposema kanuni hiyo ndio inayokataa muswada kwa mara ya pili kwa sababu una mapungufu?
Mkuu Mkandara, huu mjadala tulishaufunga kwa closing points za Mzee Mwanakijiji nami niliafiki tuufunge. Lakini kwa vile lengo ni kuelimishana, naomba niweke hapa majibu yangu in points form, huenda na wengine wasio nielewa wakanielewa hivyo hii itakuwa ni closing nyingine.

1. Uwasilishaji wa miswada bungeni is a process ambayo huanzia hatua ya kwanza mpaka hatua ya mwisho. Hatua hizo zimeainishwa katika kanuni za kudumu za bunge, tolea la mwaka 2007.
2. Katika process hiyo, kanuni zinatoa muongozo, ni wakati gani mbunge anaweza kufanya jambo gani na wanakuwekea mpaka maneno ya kutumia.
3. Pia kanuni hizo zinatoa muongozo kwa spika, ni wakati gani ataruhusu hoja, pingamizi au miongozo, na kumueleke muswada ukishafikia stage fulani on the process, kunakuwa hakuna tena kuhoji, maswali wala kupokea hoja yoyote ili kuikamilisha process nzima.
4. Muswada huu ulipoletwa kwa mara ya kwanza, ile mwezi April, uliwasilishwa na kupokelewa rasmi na bunge, ambalo lilitoa maelekezo kuwa muswada urudishwe serikali, ufanyiwe a,b,c, na d, halafu uletwe tena kwenye kamati.
5. Kamati ilipewa majukumu ya kukusanya maoni zaidi ya wananchi na kujumuisha maoni hayo.
6. Kilichofanyika, ni serikali iliuchukua huo muswada na kuufanyia marekebisho bila kuihusisha kamati ya bunge!. Ikumbukwe, muswada wa serikali, ukishawasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni, ownership ya muswada husika inachange hands toka kwa serikali kwenda kwa bunge, hivyo sasa wanaoumiliki ni bunge, serikali inapokeo maelekezo ya bunge nini kifanyike hivyo hoja ya Mhe. TL ni valid kuwa serikali imefanya mabadiliko katika ule muswada wa kwanza ambao ndio ulitakiwa kuletwa na kusomwa kwa mara ya pili, lakini kilicholetwa sasa sio ule ule muswada wa awali, bali serikali imeleta muswada mpya ambao ulipaswa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza na sio mara ya pili, na hapa ndipo jukwaa la katiba na wanaharakati walichotaka.

7.Kuanzia hapa sasa Mkuu Mkandara, naomba sasa ndio nikulete kwenye kanuni 86 kifungu cha 3.
(3) Haitakuwa halali katika hatua hii kuleta hoja ya kufanya
mabadiliko katika hoja isipokuwa tu kwamba:- ( Kanuni inatamka wazi kuweka zuio kwa spika kuruhusu hoja yoyote, hivyo alikuwa right kumzuia Mnyika, Kafulila au yoyote, unless otherwise hii inayofuatia,
(a) mabadiliko bila kutoa sababu yanaweza kutolewa
kwa kusema:
"Kwamba, Muswada huu usisomwe mara ya Pili
sasa na badala yake usomwe baada ya …..
kuanzia …..", na hapo muda ambao Muswada
huo unaokusudiwa kusomwa utatajwa.
Hapa ndipo ulipopotea Mkuu Mkandara, hapa hapano hoja kwangu kwa vile hili ni pingamizi tuu la kuomba bunge liusiupokee muswada husika siku hiyo na badala yake kuomba liupokee siku nyingine, kwa case yetu, this is immaterial.

(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza

kutolewa kwa kusema:
"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu
Kusomwa
Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo
sababu za kupinga Muswada Kusomwa Mara ya
Pili zitatajwa kwa ukamilifu.
Hapa ndipo mimi niliposimamia kwenye hoja yangu mwanzo mwisho!. Maneno hayo ndio Mhe. Tundu Lissu alitakiwa ayaseme ili kuweka pingamizi kwa muswada huo, usisonge mbele. Hli ndilo pingamizi rasmi kwa mujibu wa kanuni. Baada ya kuweka pingamizi hili, Spika lazima alisikilize na kuzikiliza sababu za pingamizi hili, na hapa ndipo Mhe. Lissu alitakiwa kutoa sababu ni kwa nini wanapinga.

Nilieleza kuwa kama ni kweli, Lissu aonyesha contrast kati ya ule muswada wa awali na huu mpya, na kuwafungua macho wabunge kuwa huu ni muswada mpya kabisa, wabunge wangeelewa na wangewaunga mkono.

Mimi ni mhudhuriaji mzuri wa bunge, mule bungeni kuna wabunge makini ambao ni vichwa vya ukweli, wangedhibitishiwa huo upuuzi wa serikali, wangewaunga mkono Chadema, ingawa pia lazima nikiri, bunge hili pia limeshehenezwa wabunge kibao ambao ni vichwa maji, vichwani ni watupu kabisa lakini ni mahodari sana kupiga kele kama lilivyo debe tupu. Ili hoja za kipuuzi puuzi kupitishwa, serikali kupitia vikao vya wabunge wa vyama, party causes, hukaa na wabunge wao kuwaambia lazima waunge mkono hoja za serikali, na huwategemea sana hawa madebe matupu kuzipigia tarumbeta.

Nilimuhakikishia Mzee Mwanakijiji, kuwa suala la katiba ni suala la kitaifa, hivyo kama hoja za TL zilikuwa na mashiko kwa maslahi ya taifa, wabunge vichwa wa CCM, wangewaunga mkono wapinzani. Mbona kuna baadhi ya miswada ya serikali iliwahi kupigwa chini, ukiwemo ule wa baraza la usalama la taifa na serikali kujikuta imelazimika ku withdraw

Mkuu Mkandara, hapa ndipo niliposimamia kuwa hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa, kama TL au mbunge yeyote angewasilisha hilo pingamizi, then hiki ndicho kingefuatia

(4) Iwapo hoja itatolewa chini ya fasili ya 3(a) na (b) ya Kanuni hii,

Spika atalihoji Bunge ili kufikia uamuzi.

8. Kwa kuwa hakuwa na pingamizi lolote rasmi kuhusu muswada huu, process iliendelea kwa

(5) Mwenyekiti wa Kamati iliyopelekewa Muswada wa Sheria au

Mjumbe mwingine wa Kamati aliyeteuliwa kwa ajili hiyo, atatoa
maoni ya Kamati kuhusu Muswada husika.
Hapa ndipo mwenyekiti wa kamati ya Lissu (Sheria na Katiba) Mhe. Pindi Chana (pia ni kichwa!), aliwasilisha maoni yake
Ikumbukwe, baada ya kukosekana pingamizi rasmi, ile kanu bado inamlazimisha spika kutoruhusu hoja yoyote, pingamizi lolote wala muongozo wowote!

9. Baada ya hapo ndipo ikafuatia

(6) Ikiwa Muswada wa Sheria unaohusika ni Muswada wa Serikali,

basi Msemaji wa Kambi ya Upinzani atatoa maoni yake juu ya
Muswada husika na endapo ni Muswada Binafsi au Muswada wa
Kamati, basi msemaji wa Serikali atatoa maoni yake.

Hapa ndipo Mhe. TL aliposoma hotuba yake, nawaombeni sana tuwe waangalifu zaidi, muda wa pingamizi ulishapita sasa ni maoni, hivyo anachokisema Mhe. Lissu ni maoni tuu, hata kama katika maoni hayo, atatamka matamshi ya kupinga, maoni ni maoni (opinion) hayasitishi kitu, hayasimamishi kitu, hayazuii kitu, ndio maana mimi nililalamika kwanini hawakuupinga rasmi muswada huu?.

Hoja kubwa ya Mwanakijiji kutetea kutowasilisha pingamizi, ni eti wangepinga wangeshindwa kwenye kura za kulihoji bunge, hivyo wakaamua bora waendelee, mimi nikasisitiza that was a mistake!

Ikumbukwe lile zuio linalomtaka spika kutoruhusu hoja zozote, swali lolote wala muongozo wowote, bado lipo.

10. Kama mtakumbuka, hapo mwanzo nilisema hii ni process na inakamilishwa kwa hotuba ya kambi ya upinzani. Kanuni inasema ili muswada wa serikali upite, lazima upate maoni ya kambi ya upinzani ku complete the process. Nikauliza, kama Chadema, ambacho ni chama makini cha upinzani, kinaupinga muswada huu, kwanini hakikuwasilisha pingamizi?, watetezi wake wakajenga hoja za utetezi. Nikauliza Tena na hili ndilo swali langu la pili kwa Lissu, Kama ni kweli mnapingwa kuwasilishwa kwa muswada huo, kwa nini mmetoa maoni ambayo ndio yanahitimisha process, nilisema Lissu alipiga chenga, nikawaambia hotuba ile ndio the missing link to complete the process.

Ingawa kanuni haitamki wazi nini kingefanyika iwapo kambi ya upinzani itasita kutoa maoni yake, kwa vile hii ni process, nikasema bila maoni hayo, muswada huo usingeweza kujadiliwa kwa sababu maoni ya kambi ya upinzani ni pre-requisite kwa muswada wa serikali kusonga mbele!.

Baada ya Hotuba ya TL, wakina Nyika na Kafulila etc wanasimama kuomba muongozo wa spika!, wanaomba muongozo wa nini at this stage wakati kifungu kinamlazimisha spika kutoruhu chochote!.

Hitimisho.
Mkuu Mkandara, kwa maoni yangu, kutowasilisha pingamizi was a mistake, kusoma hotuba ya TL was another mistake na at the end of the day sheria imetungwa we've lost!
Kwenye hoja yangu ya msingi nimesema, baada ya sheria kusainiwa, no one can do anything, sio Chadema wala wanaharakati.

Nashukuru taarifa ya M/k wa Chadema jana kuwa sasa wanakubali yaishe, wanamtafuta JK kuongea nao ili serikali iwasikilize. Naomba niwadokolee kitakachofuata. Waungwana watamshauri JK kukutana na Chadema kuwasikiliza, rais JK japo ni mtu wa smilling face, in reality ni very arrogant!. Mimi nilizishuhudia his true colors siku ile alipohutubia Wazee wa Dar es Salaam kuzua mgomo wa wafanyakazi!. Hivyo JK, kamwe hatakubali kuwaona Chadema mpaka baada yakusaini muswada ule kuwa sheria, kuwaona kabla ni ku bow down, something he will never do!, nilimuona akibow down wakati wa kuomba kura tuu, never again on anything else, lakiwa akiwa safari za nje zile za kutembeza bakuli, but not to Chadema!.

Naomba tusiende kulijadili hili, mjadala huu umeshafungwa, ila tuendelee kuelimisha tuu, sio kubishana!.

Pasco.

[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif][FONT=Helvetica, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
[/FONT]
[/FONT]
 
Pasco,
Mkuu wangu usijali ya Mwanakijiji... mimi nataka kupata darsa maanake ndio unanichanganya kabisaaaa..Muswada uliporudi ulikuwa ule ule isipokuwa umebadilishwa lugha tuiweje urudi tena kuwa mara ya kwanza wakati haukuwasilishwa kama muswada mpya?..Na nilimsikia JK akanichanganya ya kwamba muswada unapokabidhiwa kamati ya bunge ndio mara ya kwanza na unapotoka kwenda ktk Bunge zima huwa ni mara ya pili...sijui kama nimekosea..

Sasa pengine unaweza nambia kama muswada huu uliporudi ulianza tena process upya kama mara ya kwanza ama ulifika na kutaka kusomwa kama mara ya pili?..mimi nadhani ilikuwa mara ya pili kwa sababu sidhani kama ulichapishwa tena upya ktk gazeti na kadhalika..Yaani hizi siasa zenu jamani zinatuchanganya sisi na sii rahisi kwetu kujua kinachoendelea...
 
Kuanzia hapa sasa Mkuu Mkandara, naomba sasa ndio nikulete kwenye kanuni 86 kifungu cha 3.

(b) mabadiliko yenye kutoa sababu yanaweza kutolewa kwa kusema:

"Kwamba, Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu zifuatazo …….", na hapo sababu za kupinga Muswada Kusomwa Pili zitatajwa kwa ukamilifu.

maneno hayo ndio Mhe. Tundu Lissu alitakiwa ayaseme ili kuweka pingamizi kwa muswada huo, usisonge mbele. Hli ndilo pingamizi rasmi kwa mujibu wa kanuni.

Lissu akitoa hoja ya kukataa muswada kwa kanuni ya 86 3( b ) iliyokataliwa:

Last edited by a moderator:
Pasco,
Kwa kuongezea tu nimekuta habari hii ktk moja na mada za hapa JF imeandikwa hivi:-
Wakati wa kufunga muswada wa katiba, Waziri wa sheria na katiba Celina kombani alituambia watanzania kwamba anamshangaa Tundu Lissu anafunguka leo na kutoka bungeni na wanachadema wenzake wakati hakutokea kwenye vikao vya kamati ambako angeweza kutoa maoni yake. Kombani alisema, kwa mfano katika kikao cha mwezi juni, 2011 Lissu alikuwa Tarime wakati wajumbe wengine wakikutana kuandaa mchakato huo kwa ajili ya kuwakilishwa bungeni lakini pia Waziri alisema anayo orodha ya mahudhurio kuthibitisha kwamba Lissu hakuhudhuria. Katika hitimisho lake hilo Kombani alisema, wajumbe wengine kama Halima Mdee na wabunge wengine wa upinzani walihudhuria na walitoa maoni yao ambayo yamepokelewa na kufanyiwa kazi.

Kumbuka kamati hii iliundwa baada ya kukataliwa kwa muswada uliosomwa kwa mara ya kwanza ili kuribu mchakato huo upya kabla hujasomwa kwa mara ya pili miongoni mwa wajumbe alikuwa Tundu Lissu ambaye taifa limetangaziwa kwamba hakuhudhuria vikao...

Wamwombe Nani Msamaha!
Maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani chini ya Mh.tundu lissu yalikuwa Tight ile mbaya!
Wamechambua na Kudadavua Mswada ndani na nje jamaa hawa wapo safi!CCM iache kutumia msuli bora wakae na jamaa wa CDM
Vinginezo wanaweza umbuka mbele ya safari!Tupo na tuombe Uhai ili tuone

Tatizo la CDM ni kuto tumia the right strategy at a right time!! katiba ni muafaka wa wote! get this right! hivi hata tu assume CDM inapendwa saaaana hapa nchini wanafikiri kuna siku TZ itakua nchi ya chama kimoja? yaani CDM ikisema its final? mimi nadhani mtu anaye waza hivi ni mwana masaburi jazz band!!
 
Lissu akitoa hoja ya kukataa muswada kwa kanuni ya 86 3( b ) iliyokataliwa:

Duh! ama kweli ukweli sasa umejitokeza wazi kabisa... Pasco nakuomba msikilize TL alivyowasilisha akitaja kifungu cha 86 (3)b lakini Spika akasema TL aliwasikisha kanuni ya 86 (6)... wewe umeelewa hapo kimefanyika nini?

- Taso shukran sana sana...
 
Last edited by a moderator:
Pasco,
Mkuu wangu usijali ya Mwanakijiji... mimi nataka kupata darsa maanake ndio unanichanganya kabisaaaa..Muswada uliporudi ulikuwa ule ule isipokuwa umebadilishwa lugha tuiweje urudi tena kuwa mara ya kwanza wakati haukuwasilishwa kama muswada mpya?..Na nilimsikia JK akanichanganya ya kwamba muswada unapokabidhiwa kamati ya bunge ndio mara ya kwanza na unapotoka kwenda ktk Bunge zima huwa ni mara ya pili...sijui kama nimekosea..

Sasa pengine unaweza nambia kama muswada huu uliporudi ulianza tena process upya kama mara ya kwanza ama ulifika na kutaka kusomwa kama mara ya pili?..mimi nadhani ilikuwa mara ya pili kwa sababu sidhani kama ulichapishwa tena upya ktk gazeti na kadhalika..Yaani hizi siasa zenu jamani zinatuchanganya sisi na sii rahisi kwetu kujua kinachoendelea...
Mkuu Mkandala, muswada ulishawasilishwa kwa mara ya kwanza, hivyo huo uliowasilishwa kwa mara ya pili ni muswada wenye jina lile lile japo contents zilibadilishwa. Mhe. Lissu was very right our government is playing with its people's mind.

JK is right muswada unapowasilishwa kwa mara ya kwanza, haujadiliwi bali hukabidhiwa kwa kamati ili kujumuisha maoni ya wadau. Unapowasilishwa mara ya pili ndipo hujadiliwa.

Hoja ya Lissu ina mashiko kuwa baada ya muswada huo kutinga bungeni ile April na kupewa kamati yao kujumuisha maoni ya wadau, vikao vyenyewe vya kukusanya maoni ndio vile vitatu tuu, cha Karimjee nilikuwepo kikao kilivunjika, Zanzibar Muswada ulichanwa chana na Dodoma mabomu yalirindima.

Lissu is right kuwa baada ya hapo serikali ikauchukua na kuufinyanga jinsi ilivyoona inafaa na kuurudisha na mabadiliko makubwa, alichouliza Lissu serikali ilipata wapi mamlaka ya kufanya mabadiliko iliyoyafanya bila kamati yake kuridhia.

Lissu akasema hakujawahi kuwepo kikao chochote cha kamati yake kujadili mabadiko hayo, mwekiti wake anadai walikutana kujadili ila Lissu ni mtoro.

Kiukweli mabadiko yoyote ya muswada yalitakiwa yatolewe na kamati kwenda serikalini lakini kamati haikuwahi kutoa mapendekezo hayo, sasa hayo mabadiliko serikali iliyoyaleta yametoka wapi?.

Mimi naamini kama Chadema wangewasilisha pingamizi na kutoa hizo hoja za msingi, wabunge wangewaelewa na muswada ungepigwa chini!.

Kama Lissu angewasilisha pingamizi na kulithibitishia bunge kuwa hakuna kikao chochote cha kamati yake kilichofanyika na hakuna mapendekezo yoyote toka kamati yake kwenda serikalini, bunge lingejiridhisha kuwa huu sasa ni muswada mpya hivyo uliposwa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza na kukabidhiwa kwa kamati ili kujumuisha maoni ya wadau!. Hili halikufanyika!. Mimi nasisitiza it was a mistake!.
 
Wanabodi,
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.

Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Suala la kususia jumla mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni kuunda katiba mpya ni kosa kwa sababu Chadema kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ilikuwa na uwezo wa kuusimamisha na kuzuia uwasilishwaji kwa mara ya pili huo muswada kwa kutumia kanuni ya kifungu 86 hivyo kutoa fursa ya hoja ya kuzuia uwasilishwaji huo kusikilizwa, lakini Chadema haikufanya hivyo.

Hakuna ubishi kuhusu uwezo wa wabunge wa Chadema katika umakini, kitendo cha oversight ya opportunies provided by kifungu cha 86 cha kanuni za bunge kuuzuia huo muswada, sio tuu ni udhaifu mkubwa, but kosa kubwa ambalo Chadema lazima wakiri, waombe radhi na kusonga mbele.

Kanuni hiyo ya 86 inaeleza wazi hatua kwa hatua za kufuatwa ili kuuzuia muswada usisomwe kwa mara ya pili. Chadema ilipuuza na kuendelea kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani.

Kama Chadema ingezingatia kanuni hiyo, isinge wasilisha maoni ya kambi ya upinzani bali ingewasilisha pingamizi!.

Kitendo cha Mhe. Lissu kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani, yamemaanisha wameijibu hoja ya serikali hivyo kutoa go ahead majadiliano yaendelee. Uwasilishwaji wa hotuba hiyo ndio passport ya mjadala kuendelea, kama kambi ya upinzani wasingewasilisha maoni yao, muswada ungesitishwa kwanza na wao kusikilizwa. Hivyo iwasilishwaji wa hotuba ile ni kosa la pili, Chadema lazima wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Kitendo cha kususia mjadala kwa siku ya kwanza na kutoka nje, was the right move kuonyesha protest dhidi ya unyanyasaji wa Mhe. Spika, lakini kuisusa hoja jumla, was a mistake hivyo sheria imetungwa bila imput yao, hivyo hili ni kosa la tatu, Chadema wakiri kosa, waombe radhi na kusonga mbele!.

Nimebahatika kuhudhuria mdahalo wa Star TV kuhusu Tanzania tuitakayo ambapo Mhe. Tindu Lissu ilikuwa ni mdahiliwa, na nilipata fursa ya kuuliza swali kuhusu kanuni ya 86 lililokuwa na vipengele a, b na c
(a) Kanini hawakitumia kanuni ya 86 kuuzuia muswada usisomwe?.
(b) Kwanini waliwasilisha hotuba ya maoni ya kambi ya upinzani yaliyotoa passport mjadala uendelee badala ya kuwasilisha pingamizi ambayo ingeusimamisha mjadala?.
(c) Chadema wamesusa sheria imepitishwa, jee wamefaidika na nini na kususa kwao?.

Mhe. Lissu amepiga chenga kutoa majibu ya kina kwa kujibu
(a). Amenisomea hitimisho la hotuba yake. Kanuni ya 86 ilimtaka Mhe. Lissu awasilishe pingamizi na sio hotuba!.
(b) Amepiga chenga kueleza ni kwanini amewasilisha hotuba badala ya pingamizi!.
(c) Wananchi wanaelewa ni nani mtetezi wao wa ukweli.

Kwa vile sheria imepitishwa na itasainiwa na rais kwa mbwembwe, lazima Chadema na wapenzi wao na mashabiki wao waukubali ukweli mchungu kuwa they lost the bettle hivyo watake wasitake, lazima wakubali matokeo. Hawawezi kuendelea kususa, lazima wajisibmit kwenye tume ya kuratibu maoni na kutoa maoni yao hata kama tume hiyo itaundwa bila imput yao na bila ridhaa yao!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.

Wasalaam
Pasco (wa jf).

Update 1.

Update 2.

Update 3.

Pasco umefunga kazi, hakuna ambae hajakuelewa. Wamekosea na wanajuwa wamekosea na ndio maana wanatafuta pa kutokea kwa kujipendekeza kwenda kumuona Rais. Hawana njia nyingine.

Shamsi Vuai Nahodha anawangoja mitaani huko wakijidai wanaleta fujo, si ndio zao "wapiganaji", kampeni ijayo tunataka Msajili wa vyama atueleze kama CHADEMA kina uhai wa uhalali kwa kutimiza kuwa na wanachama pande zote mbili za Muungano. Hili nalo neno.
 
Duh! ama kweli ukweli sasa umejitokeza wazi kabisa... Pasco nakuomba msikilize TL alivyowasilisha akitaja kifungu cha 86 (3)b lakini Spika akasema TL aliwasikisha kanuni ya 86 (6)... wewe umeelewa hapo kimefanyika nini?
Mkuu Mkandara, madam speaker was very right, Maneno hayo TL alitakiwa ayaseme kwenye 86 (3) b ni kuwasilisha pingamizi. Mkandara nakuhakikishia Hakuna pingamizi lolote lililowasilishwa!.

Alichofanya TL ni 86 -6 kutoa maoni ya kambi ya upinzani, hata kama katika kutoa maoni huko ameweka maneno pingamizi, hayo yanabaki ni maoni tuu. Pingamizi ni pingamizi likiwekwa lazima bunge linasimamisha kila kitu na kulisikiliza pingamizi lile.

Kwa kuwa hakukuwa na pingamizi lolote. process iliendelea kwa kumsikiliza M/kiti wa Kamati na baadae Maoni ya upinzani. Watu wanaamini maoni hayo ndio pingamizi!. No!. Maoni ni maoni tuu na hakukuwa na pingamizi and that was a mistake!.
 
Dah, hizi siasa kusema kweli sii uwanja wangu kabisa... yaani TL alitakiwa kuweka pingamizi pale aliposimama mara ya kwanza kabla ya hotuba yake sio? hata kama ametaja kanuni sawa haijalishi itawekwa kifungu cha kanuni nyingine kabisa bila kuwa na maana ya kifungu alichosoma..huu ndio utaratibu wa bunge!...dah kaazi kweli kweli.....Ni wakati gani HOJA zinatolewa na ni wakati gani MAONI hutolewa..

Sasa tuseme kuna mtu wa CCM ambaye alitaka kuuzuia muswada huo usisomwe angeweza vipi ikiwa TL ndiye ametangulia kuzungumza kwa niaba ya kambi ya Upinzani.. Kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini kosa linaitwa la CDM wakati hawa wote ni wabunge wetu sisi sote. Why only TL ndiye alitakiwa kusimamisha muswada huo..

Sasa turudi kwa wananchi kama Mama Kilango alivyosema kwamba wao ni wawakilishi wetu ingawa naye kabomoa bomoa... Kwa maslahi ya wananchi kama Spika ameona utata ktk muswada huo kulingana na hoja ya TL kwa nini asiwatumikie wananchi badala yake anamtumikia JK na chama Chake kuhakikisha upinzani hawapewi nafasi ya kusitisha muswada huo? Hivi kweli Spika akiona tatizo ktk muswada huwezi kuzuia usisomwe mara ya pili wakati wowote.. au naye aliona kikanuni kila kitu safi tu maanake navyochukulia mimi wabunge wote pale ni wawakilishi wetu inakuwaje swala hili ghafla likawa la vyama badala ya wananchi.
 
Mkuu hata mimi najiuliza swali hili sipati jibu...Kumbe hata hicho kifungu kilinukuliwa na TL wakati wa hoja yake!
 
Mkuu Mkandala, bunge huendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni, ila kuna kitu kingine hakijaandikwa nacho ni busara. Mama Makinda analiendesha bunge kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, na kweli hili la kufuata kanuni, namvulia kofia kufuatia 'uzoefu wa long experience ya uzoefu wa muda mrefu'. Tatizo lake kubwa ni moja tuu, Mama hana busara!, kufuatia kukosekana kwa busara, analiendesha bunge kama robot kufuata sheria taratibu na kanuni lakini busara zero!.

Ni kwenye matukio kama haya, huwa namkumbuka sana spika Sitta, ambaye licha ya kutumia kanuni, pia alitumia busara in goot faith.

Kwa mfano angelikuwa ni enzi za Sitta, hotuba ile Lissu ilishawasilishwa ofisi ya spika kabla, alipoipitia angekuta kumbe ni maoni ya kambi ya upinzani yakijumuisha pingamizi, angeshauri mbunge kutoa hoja ya kuitengua kanuni 8. (6) na kuruhusu kanuni ya 8(3) (b) ili maelezo hayo ya Lissu yawe treated kama pingamizi rasmi ambalo lingejadiliwa. Sitta aliruhusu mijadala yenye changamoto na angelikuwepo, asingeruhusu upuuzi huu wa serikali kwenye the most important issue (Katiba). Kwa baadhi ya nchi, Spika wa Bunge ni lazima awe Mwanasheria.
 
Mkuu hata mimi najiuliza swali hili sipati jibu...Kumbe hata hicho kifungu kilinukuliwa na TL wakati wa hoja yake!

Tundu hakuwa na hoja yake. Na hapo pia unakosea.

Tundu ni mwanasheria na anajuwa maana ya kanuni za bunge na anajuwa kakosea na ingekuwa kama spika kakosea basi kuna taratibu za kibunge ambazo zingefatwa na ziko wazi kabisa, lakini kwa kuwa Tundu anajuwa kuwa kakosea ndio maana hakuweza kufata hata hizo kanuni za kumrekebisha spika anapokosea kama ingekuwa kakosea.

Magwanda kwa hili halina ujanja, ni makosa makubwa sana ambayo huwezi kuyafuta kwa maneno. Kanuni ni kanuni, kesi zinatupwa mahakamani kwa sababu tu hazijafata kanuni ya aina gani ya kuandika au "Font size" tu. Sasa hapo panapotungwa sheria ni lazima ufate sheria, hata JF wana kanuni ukuzikiuka unakula ban labda "Makinda" wa JF siku hiyo awe kalewa na kakuonea. Bungeni usione tu wanaongea pale, wewe unaweza kubwabwaja tuuu kama alivyofanya Tundu lakini haikuwa na maana yoyote maneno yake, alikuwa hapingi pale alikuwa anatoa maoni yake, na maoni yake ni wanaomsikiliza ama wayakubali ama wasiyakubali lakini hayabadili kanuni za bunge.
 
Tundu hakuwa na hoja yake. Na hapo pia unakosea.

Tundu ni mwanasheria na anajuwa maana ya kanuni za bunge na anajuwa kakosea na ingekuwa kama spika kakosea basi kuna taratibu za kibunge ambazo zingefatwa na ziko wazi kabisa, lakini kwa kuwa Tundu anajuwa kuwa kakosea ndio maana hakuweza kufata hata hizo za kanuni za kumrekebisha anapokosea.

Magwanda kwa hili halina ujanja, ni makosa makubwa sana ambayo huwezi kuyafuta kwa maneno. Kanuni ni kanuni, kesi zinatupwa mahakamani kwa sababu tu hazijafata kanuni ya aina gani ya kuandika au "Font size" tu. Sasa hapo panapotungwa sheria ni lazima ufate sheria, hata JF wana kanuni ukuzikiuka unakula ban labda "Makinda" wa JF siku hiyo awe kalewa na kakuonea. Bungeni usione tu wanaongea pale, wewe unaweza kubwabwaja tuuu kama alivyofanya Tundu lakini haikuwa na maana yoyote maneno yake, alikuwa hapingi pale alikuwa anatoa maoni yake, na maoni yake ni wanaomsikiliza ama wayakubali ama wasiyakubali lakini hayabadili kanuni za bunge.

Ningependekeza sasa tujielekeze kwenye muswada wenyewe na kuachambua. Bunge la CCM limeupitisha, je, wananchi tunakubali yote yaliyomo ndani ya muswada huu kama yalivyopitwa na bunge hilo la ccm? Nini kifanyike? na wapi pa kurebisha? haya ndio mambo ya msingi kwa maoni yangu.
 
Back
Top Bottom