Hebu soma post #12 hapo juu...
Ukiisha soma, je wewe unaweza kutuambia hii ina maana gani?
".....kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa toka miongoni mwa watumishi waandamizi walio katika Utumishi Wa umma...."
1. Huyu Bashiru Ally Lyakurwa, alikuwa ni afisa mwandamizi aliye katika Utumishi Wa umma?
2. Au Je, kuna kipengere cha katiba kinachoi - counter attack IBARA hii ya katiba ili kumpa Rais nguvu/mamlaka ya kumteua huyu ndugu kushika wadhifa huo kinyume na mwongozo na maelekezo ya ibara hii ya katiba...?
NOTE: By the way, kumbuka kuwa huu ni mjadala tu wa kujengeana ufahamu. Hakuna mtu mwenye tatizo binafsi na Ndg Bashiru Ally Lyakurwa au Rais John Pombe Magufuli...
Na in fact mjadala huu unaweza usibadili chochote katika hiki kilichokwisha kutendeka na kuamuliwa na Rais Magufuli hata kama tutajadili mpaka tuvue na nguo zetu...
Lakini all in all, hii haiwazuii watu kujadiliana na kuhoji...