Hii pia siyo hoja kwa sababu kuwa kwako mtumishi katika chama haikuondolei haki ya kuhudumu kama mtumishi wa umma.
Ndiyo maana tuna watumishi wa umma ni makada wa vyama mbalimbali lakini hatuwahukumu kwa vyama vyao tutawahukumu kwa namna watakavyotekeleza kanuni na miongozo ya utumishi wa umma
At least you can be reasonable at times....Yah, nakuunga mkono, hajavunja katiba.
Hawa watu wanaleta vipengele vya rasimu ya warioba wanawaaminisha watu kuwa katiba ya sasa ndivyo inavyosema wakati siyo!
HahahahaaKifupi wewe fahamu tu, kikatiba, kisheria na kikanuni Rais Magufuli kashemka vibaya.
Kaokota tu mtu huko Lumumba na kumpa cheo cha juu serikalini.
Sijafuatilia kiapo chake ila nijuavyo Balozi ni mtumishi wa serikali, mara nyingi tumeona watumishi wa serikali wana teuliwa kuwa wabunge na kuteuliwa kuwa mawaziri muda huo huo na kesho yake wanaapishwa na Rais kuwa mawaziri kwa kiapo kimoja.
Pia kuwa Balozi sio lazima upangiwe kituo cha uwakilishi , ile ni uwakilishi na pia ni heshima ambayo mtumishi anaweza akapatiwa na Rais kwa utumishi wake ulio tukuka.
we ndo umeweka uzio mzuri wa nini hoja ya msingi. bahat mbaya wanasheria na wajuvi weng hutawaona hapa kila kitu wanawazia kulipwa fee. na mbaya zaid wachangiaj weng hawajikiti kwenye hoja mana ufaham mdogo. tunaotaka kujifunza tunapotea njia mara. mijadala mirefu labda ihusu pipi mahaba! turud hapa.. MR BASHIRU ANAINGIA KUNDI LA WATUMISHI WA UMMA WAANDAMIZI?Hebu soma post #12 hapo juu...
Ukiisha soma, je wewe unaweza kutuambia hii ina maana gani?
".....kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa toka miongoni mwa watumishi waandamizi walio katika Utumishi Wa umma...."
1. Huyu Bashiru Ally Lyakurwa, alikuwa ni afisa mwandamizi aliye katika Utumishi Wa umma?
2. Au Je, kuna kipengere cha katiba kinachoi - counter attack IBARA hii ya katiba ili kumpa Rais nguvu/mamlaka ya kumteua huyu ndugu kushika wadhifa huo kinyume na mwongozo na maelekezo ya ibara hii ya katiba...?
NOTE: By the way, kumbuka kuwa huu ni mjadala tu wa kujengeana ufahamu. Hakuna mtu mwenye tatizo binafsi na Ndg Bashiru Ally Lyakurwa au Rais John Pombe Magufuli...
Na in fact mjadala huu unaweza usibadili chochote katika hiki kilichokwisha kutendeka na kuamuliwa na Rais Magufuli hata kama tutajadili mpaka tuvue na nguo zetu...
Lakini all in all, hii haiwazuii watu kujadiliana na kuhoji...
Kwamba ibara ya 116 ya katiba ya JMT inatamka hivi unavyosema? Na huoni aibu kuweka hii post ukiwa umejigamba?
ideally inawezekana kabisa, ila mamlaka za teuzi kama zimekaa kisiasa basi zitaona tatizo, lakini kama tuko politicaly matured inawezekana!..kwa hiyo mtu anaweza kuwa Katibu Mkuu wizara ya ulinzi, halafu akawa m-nec wa Chadema?🤣
Ibraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa na Stella Artois upate nini?Ndugu yangu utaumiza kichwa jambo la msingi ni kujikinga na corona
..huko nyuma tumewahi kuwa na makatibu wakuu kiongozi ambao sio mabalozi.Naomba kuuliza.hivi yule katibu mkuu kiongozi Martin luhanjo Naye alikua balozi?.kwakifupi ili mtu awe katibu mkuu kiongozi lazima awe balozi?
ideally inawezekana kabisa, ila mamlaka za teuzi kama zimekaa kisiasa basi zitaona tatizo, lakini kama tuko politicaly matured inawezekana!
Ndiyo maana Kitila Mkumbo alikuwa katibu mkuu wa wizara ya maji kabla ya kujivua uanachama wa ACT.
Alikuja kujivua baadae
Huapa bungeni baada ya Rais kuwaapisha na kuendelea na shughuli zao kama mawaziri, hakuna sehemu kikatiba inayosema uwape kwanza kwa kiapo fulani ndipo uwape cha pili ili uwanze kazi. Hivyo sijaona tatizo la Dk bashiri kuteuliwa kuwa balozi na katibu kiongozi kwa wakati mmoja. Labda kama kuna agenda ambayo haijulikani...hao lazima waende wakaape na bungeni.
..ninavyoelewa mimi balozi anakuwa na kituo, au anakuwa mkurugenzi makao makuu ya wizara.
..pia wako wengine ambao wamekuwa seconded kutumikia mahala fulani, lakini bado wanakuwa wanapanda ngazi za utumishi wizarani na hivyo kuwa mabalozi.
..ubalozi wa heshima sijawahi kuushuhudia hapa Tanzania.
Hoja iwe ni kushika nafasi mbili za utumishi je ni halali kisheria?..huko nyuma tumewahi kuwa na makatibu wakuu kiongozi ambao sio mabalozi.
..na ambao walikuwa mabalozi ni kwasababu walipata kuwa watumishi wa wizara ya mambo ya nje.
Uteuzi wa Kitila haukuwa na tatizo kwa sababu alimtoa ofisi moja ya utumishi ambayo ni (Lecturer kwenye chuo cha umma) na kumpeleka kwenye ofisi nyingine ya umma(ukatibu mkuu)...Je, haiwezekani kuwa uteuzi wa Kitila Mkumbo nao ulikuwa na matatizo?
Huapa bungeni baada ya Rais kuwaapisha na kuendelea na shughuli zao kama mawaziri, hakuna sehemu kikatiba inayosema uwape kwanza kwa kiapo fulani ndipo uwape cha pili ili uwanze kazi. Hivyo sijaona tatizo la Dk bashiri kuteuliwa kuwa balozi na katibu kiongozi kwa wakati mmoja. Labda kama kuna agenda ambayo haijulikani.
..basi tuletee kifungu ambacho ni sahihi, na kinachohalalisha uteuzi huu.