Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?


..kwa hiyo kumtoa mtu ofisi ya chama na kumpeleka ofisi ya umma hamna makosa?
 
Lakini unasahau kwamba rais ni taasisi.
 
..kwenye taarifa ya Ikulu inaonyesha alimteua kuwa katibu mkuu, halafu akamteua kuwa balozi.
Sheria inayounda Ofisi ya katibu mkuu Kiongozi ni The Public Service Act na uteuzi wake hufanyika kwa mujibu wa kifungu cha nne cha sheria hiyo.

Sheria husika haijaweka sifa za mtu anayetakiwa kuteuliwa katika nafasi ya Katibu Mkuu.

Sheria ya mwaka 2002 iliainisha sifa za mtu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi lakini 2018 na 2019 yalifanyika mabadiliko yaliyoondoa kipengele kinachotaja sifa za mtu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
 

..Duh!!

..kwa hiyo hata kuwa machinga kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi?

..MUNGU atusaidie.
 
Unaweza kuweka kifungu cha sheria kuthibitisha makosa kama unadhani alikosea?

..kwanini hunionyeshi kifungu ambacho kinaonyesha kuwa yuko sahihi?

..hii ni mara ya kwanza ktk historia ya Tanzania kuteuliwa Katibu Mkuu Kiongozi kama alivyoteuliwa Dr.Bashiru.

..yaani hata wakati wa chama kimoja, na chama kushika hatamu, Katibu Mkuu Kiongozi hakuwahi kuteuliwa kwa mtindo huu.
 
Bashiru alikuwa mtumishi wa umma alikuwa mwalimu UDSM
University of Dar es Salaam ni Chartered entity

Kwahiyo watumishi wa UDSM wako nje ya sheria ya utumishi wa umma na hata ukiangalia definition of a public service utapata jibu sahihi
 

Man, the budden of proof lies squarely on the accuser.

Sisi tunasema yuko sahihi, ni jukumu la wewe unayemuaccuse kuwa kakosea ulete kifungu kuwa kakosea!
😁😁
 
University of Dar es Salaam ni Chartered entity

Kwahiyo watumishi wa UDSM wako nje ya sheria ya utumishi wa umma na hata ukiangalia definition of a public service utapata jibu sahihi
Nani amekudanganya karudie kufanya research
 
Mheshimiwa nadhani aliambiwa kuwa atakuwa anavunja katiba, ndiyo maana ikabidi amuapishe kwanza kuwa balozi, kisha ndiyo amuapishe awe katibu kiongozi. Amei-exploit loophole hiyo.

Kiufupi ametimiza hitaji la kikatiba.

Lakini jinsi alivyofanya hivyo, arguably its unethical.
 
..huko alishatoka.

..aliingia kwenye SIASA.

..watumishi wa umma hawaruhusiwi kujihusisha na siasa.
Universities are chartered entities kama UDSM ilivyo hivyo watumishi wake wako excluded kwenye public service by virtue of the Public Service Act
 
Kwani kama hujui kitu lazima uchangie mada, ambazo zinahutaji ufahamu mzuri wa jambo husika?!!kimya kinaficha mengi, sana!!hadi hapo umeshajionyesha ni mtu wa namna gani kwenye mambo ya sheria!!hapa sio kule simba kwa sasa hata bayern munich hatoki, !!
Shame on u!!yaani hata katiba hujui inasrmaje juu ya sifa za mtu kuwa katibu kiongozi, unaleta sifa za mjumbe wa shina ndio hizo za katibu kiongozi?!!
la muhimu kwa sasa mambo hayazingatii katiba bali ni kwani meko anasemaje?!!na hakuna wa kuhoji!!haya mambo yangekuwa KENYA, sijui!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…