Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?

..sina kumbukumbu ya mabalozi wa aina hiyo.

..sijui wewe mwenzangu unamkumbuka balozi yeyote aliyeteuliwa halafu asiwakilishe nchi, au kuwa mkuu wa idara wizara ya mambo ya nje?

..ila wako watumishi wa wizara ya mambo ya nje ambao wako seconded maeneo mengine ambao nadhani huwa wanaendelea kupanda ngazi kama foreign service officers.
Ibrahim Msabaha siyo balozi?
 
Ibrahim Msabaha siyo balozi?

..Dr.Msabaha nakumbuka alikuwa chuo cha diplomasia, baadae akawa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje, halafu akagombea ubunge. inawezekana utumishi wake chuo cha diplomasia ndio uliopelekea akateuliwa kuwa balozi.
 
Kifupi wewe fahamu tu, kikatiba, kisheria na kikanuni Rais Magufuli kashemka vibaya.
Kaokota tu mtu huko Lumumba na kumpa cheo cha juu serikalini.

Mhe Antipas Tundu Lissu aliposema kuna WATU MAGUFULI HUWA ANAWAOKOTA MAJALALANI he was correct to the dot.
Naomba TAL2025 atupe ufafanuzi wa kisheria kulingana na uteuzi huu! Over n' Out😎
 
Tuendelee kunywa 'chachandu'
Ndimu+pilipili kichaa+tangawizi+vitunguu swaumu+maji
 
kuna kipindi manabii walimuomba mungu kisha mambo yafanyao yeye mungu na kutaka kujua hana fananaje ila hakuna hata mmoja kutaka kujua aliwajaribu kidodo kujua binadamu ni watu zaidi ya mungu.uhuru wa habari,katiba,sheria,mawazo yote haya yeye si mkubwa
 
..Dr.Msabaha nakumbuka alikuwa chuo cha diplomasia, baadae akawa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje, halafu akagombea ubunge. inawezekana utumishi wake chuo cha diplomasia ndio uliopelekea akateuliwa kuwa balozi.
Ok.

Still, Magufuli hajavunja katiba kwa kumteua Dkt. Bashiru.

Natambua kuna watu hawampendi tu Magufuli kwa sababu anuai.

Hivyo, chochote kile akifanyacho, kwao ni kibaya tu.

Vilevile natambua kuna wengine hawajapendezwa na uteuzi huo kwa sababu mteule alikuwa katibu mkuu wa chama kilichopo madarakani.

Lakini kusema kwamba uteuzi huo umevunja katiba, ni kusema uongo.
 
Naomba utuwekee ibara ya katiba ya JMT inayotoa sifa za mtu anayestahili kuteuliwa kuwa CS

Hebu soma post #12 hapo juu...

Ukiisha soma, je wewe unaweza kutuambia hii ina maana gani?

".....kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa toka miongoni mwa watumishi waandamizi walio katika Utumishi Wa umma...."

1. Huyu Bashiru Ally Lyakurwa, alikuwa ni afisa mwandamizi aliye katika Utumishi Wa umma?

2. Au Je, kuna kipengere cha katiba kinachoi - counter attack IBARA hii ya katiba ili kumpa Rais nguvu/mamlaka ya kumteua huyu ndugu kushika wadhifa huo kinyume na mwongozo na maelekezo ya ibara hii ya katiba...?

NOTE: By the way, kumbuka kuwa huu ni mjadala tu wa kujengeana ufahamu. Hakuna mtu mwenye tatizo binafsi na Ndg Bashiru Ally Lyakurwa au Rais John Pombe Magufuli...

Na in fact mjadala huu unaweza usibadili chochote katika hiki kilichokwisha kutendeka na kuamuliwa na Rais Magufuli hata kama tutajadili mpaka tuvue na nguo zetu...

Lakini all in all, hii haiwazuii watu kujadiliana na kuhoji...
 
"Katiba yetu ni mbovu haifai ila ikivunjwa,hatutasita kuitetea kwa nguvu zote" Mdau.😁
 
Ok.

Still, Magufuli hajavunja katiba kwa kumteua Dkt. Bashiru.

Natambua kuna watu hawampendi tu Magufuli kwa sababu anuai.

Hivyo, chochote kile akifanyacho, kwao ni kibaya tu.

Vilevile natambua kuna wengine hawajapendezwa na uteuzi huo kwa sababu mteule alikuwa katibu mkuu wa chama kilichopo madarakani.

Lakini kusema kwamba uteuzi huo umevunja katiba, ni kusema uongo.

..na wewe lazima ukiri kwamba una mapenzi makubwa na Magufuli.

..kwa mfano, huoni tatizo lolote kwamba Dr.Bashiru alikuwa mwandamizi CCM, halafu anapelekwa kuwa mwandamizi ktk civil service.
 
Yah, nakuunga mkono, hajavunja katiba.
Hawa watu wanaleta vipengele vya rasimu ya warioba wanawaaminisha watu kuwa katiba ya sasa ndivyo inavyosema wakati siyo!
 
..na wewe lazima ukiri kwamba una mapenzi makubwa na Magufuli.

..kwa mfano, huoni tatizo lolote kwamba Dr.Bashiru alikuwa mwandamizi CCM, halafu anapelekwa kuwa mwandamizi ktk civil service.
Hii pia siyo hoja kwa sababu kuwa kwako mtumishi katika chama haikuondolei haki ya kuhudumu kama mtumishi wa umma.
Ndiyo maana tuna watumishi wa umma ni makada wa vyama mbalimbali lakini hatuwahukumu kwa vyama vyao tutawahukumu kwa namna watakavyotekeleza kanuni na miongozo ya utumishi wa umma
 
..na wewe lazima ukiri kwamba una mapenzi makubwa na Magufuli.

..kwa mfano, huoni tatizo lolote kwamba Dr.Bashiru alikuwa mwandamizi CCM, halafu anapelekwa kuwa mwandamizi ktk civil service.
Hahaaaaa.

Kwa bahati mbaya kwako, rekodi yangu humu JF inaonyesha kinyume na hilo dai lako la kwamba nina mapenzi makubwa kwa Magufuli.

Nimeshamsema sana Magufuli humu na ushahidi upo.

Unabisha?

Kwa hiyo haupo sahihi. Mimi nipo measured sana.

Akikoseaga huwa namsema. Na ambapo hajakosea, huwa nasema kuwa hajakosea.

Wewe rekodi yako humu ya Magufuli ikoje?
 
..hebu tusaidie kujua kama Dr.Bashiru aliapishwa mara mbili. kwanza kuwa balozi, halafu kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

cc Nyani Ngabu
Sijafuatilia kiapo chake ila nijuavyo Balozi ni mtumishi wa serikali, mara nyingi tumeona watumishi wa serikali wana teuliwa kuwa wabunge na kuteuliwa kuwa mawaziri muda huo huo na kesho yake wanaapishwa na Rais kuwa mawaziri kwa kiapo kimoja.

Pia kuwa Balozi sio lazima upangiwe kituo cha uwakilishi , ile ni uwakilishi na pia ni heshima ambayo mtumishi anaweza akapatiwa na Rais kwa utumishi wake ulio tukuka.
 
Hebu soma post #12 hapo juu...

Ukiisha soma, je wewe unaweza kutuambia hii ina maana gani?

".....kutakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi atakayeteuliwa toka miongoni mwa watumishi waandamizi walio katika Utumishi Wa umma...."

1. Huyu Bashiru Ally Lyakurwa, alikuwa ni afisa mwandamizi aliye katika Utumishi Wa umma?

2. Au Je, kuna kipengere cha katiba kinachoi - counter attack IBARA hii ya katiba ili kumpa Rais nguvu/mamlaka ya kumteua huyu ndugu kushika wadhifa huo kinyume na mwongozo na maelekezo ya ibara hii ya katiba...?

NOTE: By the way, kumbuka kuwa huu ni mjadala tu wa kujengeana ufahamu. Hakuna mtu mwenye tatizo binafsi na Ndg Bashiru Ally Lyakurwa au Rais John Pombe Magufuli...

Na in fact mjadala huu unaweza usibadili chochote katika hiki kilichokwisha kutendeka na kuamuliwa na Rais Magufuli hata kama tutajadili mpaka tuvue na nguo zetu...

Lakini all in all, hii haiwazuii watu kujadiliana na kuhoji...
Kwamba ibara ya 116 ya katiba ya JMT inatamka hivi unavyosema? Na huoni aibu kuweka hii post ukiwa umejigamba?
 
Back
Top Bottom