Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Leo umeandika kama mwananchi mzalendo .
 
Kama maelezo haya ya CPA Catherine Ruge ni ya kweli. Basi ninawashauri wajeda wachukue nchi kesho.

Sikiliza mwenyewe

View attachment 2692415

Aiseeh maelezo ya huyo dada yanaendana na hali halisi kuanzia king musukuma, wapambe wakina kitenge na wengineo ukiwaona na nguvu kubwa iliyo nyuma ya ccm havipishani na picha iliyopo kwa sasa na watu ona wanavyokamatwa.

Ni hivi iwe kwa KUZINYA AU KUZITAPIKA wanajua wenyewe na hili la bandari tayari siki ishaingiamo

Kubabaake manina wallah ccm safari hii sioni pa kutokea na ndo maana Lisu leo kabadili tusi na nnaomba iwe kweli tuone Ccm huo uzalendo wenu.

Kila kukicha Tanzania ni kudaiwa fidia tu kumbe ni michongo hela zipigwe mikataba wanasign ccm

Nileteeni kile kibibi faiza fackin
 
Pascal ninyi ccm wote ni wanafiki Sana, na hapa ndipo mtakumbuka maneno ya Tundu Lissu.

Lissu alishauri vizuri bungeni namna nzuri na kutoka hapa na njia mbadala ya kukwepa hiki lakini pia hatimaye akaeleza hatua za kuachana na mikataba mibovu akitahadharisha madhara yatakayoikabili nchi ikiwa tutaiparamia mikataba hii kienyeji.

Mlimtukana na kumpiga risasi, mkaendelea kubeza kwa kumpa majina ya hovyo eti Mzee wa MIGA. (cc tutusa mmoja anayejiita Eltwege), sasa ona MIGA Ndio hiyo inaendelea kututafuna na mmeshaanza kulia kungali mapema. Na huenda hii ikawa mwanzo wa mdogo wa kesho nyingi zilizofunguliwa.
 
With all due respect, Sir, this is no news at all in this godforsaken country. Hii ni kama kusema "mbwa kamng'ata mtu". No news at all. Hatushangai tena mambo hayo ya ovyo kutendeka nchini mwetu. Tena tunatarajia uwezekano wa wanasheria wetu na hata viongozi "kuwasaidia" hao wadai wetu kutushinda katika mahakama za kimataifa ili wapate "pasenti" zaidi. Hii ni nchi ya "kitu kidogo". Ujanja wetu ni kukogana mitaani kishamba kwa mijengo, ndinga kali, pamba kali na bata kubwa kubwa! Huku nchi ikizidi kuzama kwenye lindi la umasikini na ujinga uliotopea.

Siku serikali ya CCM ikishinda kesi kwenye mahakama ya kimataifa andika makala hata kwenye gazeti la Uhuru. Kwa mara ya kwanza nakuhakikishia nitanunua nakala. Ile jeuri feki ya JPM kujidai hadharani hatulipi huku tukilipa na riba kubwa juu kimya kimya ilikuwa ni maumivu ya kuhuzunisha ambayo wengi ama hawakujua au hata kutaka kujua ili tu waweze kumtukuza binadamu "waliyemzimikia"!

Serikali ya CCM ina bahati sana kwamba Watanzania wengi hawasumbuki kujua hela yao inavyochezewa na kufujwa viongozi wanavyojisikia. Wao wanafikiri kuonyeshwa majengo, madaraja, barabara, ndege, flyovers, n.k. inatosha bila kuelezwa gharama iliyotumika na ubora halisi wa vitu hivyo. Hata wanaojali, hawana jeuri ya kuihoji serikali.
 
Mbona wanaendelea kuingia kwa lazima? Hiyo solution yako hauoni kuwa haipo?

Solution sahihi ni wananchi kwa umoja wao kujitoa mhanga hata ikibidi damu kumwagika ili kwanza mfumo unaoruhusu mikataba mibovu uondolewe.

Tunatakiwa kuhakikisha tunapata Katiba mpya haraka kabla ya 2025, kisha CCM kuondolewa madarakani mapema iwezekanavyo.

Kama hawataki, basi inatupasa kila mwananchi popote alipo aweke shinikizo kwa njia anayoona inafaa. Mfano, migomo, kuwazomea viongozi, kuandamana, kuchora katuni, kuelimisha umma nk.
 
Wabaya na maadui wakubwa wa nchi yetu ni sisi wenyewe - inauma mno!
 
Hapo hakuna cha mkataba mbovu, usitake kudsnganya watu.

"Unlawful expropriation" haaimaanishi "mkataba mbovu". Inamaanisha "unyakuzi kinyume cha sheria." Sema ukweli, ni nani alimnyakulia mwenzie kinyume cha sheria?


Wewe unasema umesoma sheria halafu hapo hujaelewa kilichoandikwa uau umependa tu kuudanganya uma?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Pascal mtoto wa mayala kwa maandiko kama nitakuwa pamoja nawe. Ila kwa maandiko ya mapambio ya hosana mbinguni hata ukitupwa kagera ukiwa chakula cha mamba. Mimi nitachangia petroli ya kukufikisha mtoni. Nisiwe mnafiki wa kuita mwanzi mua mkubwa wakati wafu wakigema wanalewa.
 
Mimi nimeona kwa mkataba huu kuna unyakuzi kinyume cha sheria wa bandari za Tanganyika.
 
Hiv Pascal hili la bandari linatofauti gan na hili
 
P, kuepukana na haya Kuna mambo mawili tu
1.kuitaka katiba mpya
2. au laa , tuilejelee Tanganyika yetu Kama nchi inayoitwa Tanzania inatuletee maumivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…