Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

Haya yanayotokea siyo kwa sababu katiba yetu ni mbovu, la hasha. Wala si kwa sababu tuna sheria mbovu, la hasha. Wala si kwamba tuna wanasheria wabovu, la hasha. Kazi ya mwanasheria ni kumwandalia kile ambacho mteja wake anataka, na matakwa hayo ya mteja wake mwanasheria atayatetea hadi mwisho.

Haya yanayotutokea ni kwa sababu ya mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji wa nje. Wa kulaumiwa kwa mikataba hii mibovu ni watawala wetu (wanasiasa), wanasheria hutekeleza kile ambacho watawala wanataka.

Sheria zetu zinazohusu wawekezaji wa nje ni nzuri. Sheria zetu, kwa nia njema ya kuvutia wawekezaji wa nje ziliridhia Conventions za Umoja wa Mataifa za kulinda (guarantee) mikataba hii ya uwekezaji haswa kwa nchi zinazoendelea na hivyo kuzifanya conventions hizo kuwa sheria ya nchi yetu. Na ni karibu nchi zote duniani zilifanya hivyo. Conventions hizi ni zile za Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) na ile ya International Center for Settlement of Investment Disputes (ICSID). Hivyo hata huyu DP World hakupaswa kuwa na wasi wasi wa kutafuta protection nyingine ya kwake tu kwa uwekezaji wake nchini kwetu.

Ni jambo bora kabisa kuvunja hiyo mikataba mibovu na kulipa hiyo USD 100m kuliko kuendelea kupoteza hayo madini yetu yote ya nickel yenye thamani ya mabillion ya dollars za marekani.

Hilo liwe funzo kwetu kuwa makini sana na mikataba ya uwekezaji tunayoingia. Timu za negotions tunazoziteua zinapaswa kufuatiliwa kwa karibu na security system yetu wakati zinapofanya majadiliano hayo kwani kick back ya 10m USD kwa kila member wa timu hiyo is just peanut kwa hawa foreign investors. Na timu hizi zinapaswa kusheheni wachumi wabobezi na watalaam wa mipango waliobobea, siyo wanasheria. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali ndiyo inapaswa ku draft makubaliano hayo na kumshauri rais wetu. Na si vibaya wananchi na bunge letu wakashirikishwa kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya mikataba hii hasa ile mikubwa. La sivyo tutaendelea kupigwa na vitu vizito.
 
sisiemu
 

Hivi mbona kama tumekwama kwenye tatizo la mikataba? Shida ni nini? Kwanini hatuheshimu yale tulioyasaini ndani ya hiyo mikataba?
 
Kabisa mkuu, Ccm ndi sababu na chanzo cha umasikini ndani ya hili taifa.
 
Kumbuka TU kuwa Sheria ya rasilimali asili inaenda kurekebishwa ili dp atushtaki vizuri tukivunja mkataba endapo tutaona hawaleti faida na hawatekelezi tuliyokubaliana.


Wenyewe wanajisemea wakiwa kwenye minsion zao " tutafunga mkataba wa wa kukupendelea Ila utatupatia 10% alafu wewe utajua utakachofanya wakiona una manufaa tutawashauri kuvunja mkataba ili ukashtaki MIGA nitakusaport ukishinda utanipa 15% Sawa!.
 
Tujiandae kupigwa mnada kama alivyosema Ndugai
 
Nashangaa Pasco Mayalla, wakati Tundu Lissu anawambia tunavunja mikataba, tutashitakiwa, mulimdhiaki! Bora umenena wewe P. Sasa yametukuta
Gharama ya kuendelea na mikataba hiyo ilikuwa kubwa sana kuliko gharama ya kuivunja. Wewe fikiria tulikuwa tukilipa capacity charges ya shilingi bilioni 15 kwa siku kwa makampuni hayo ya umeme. Tukitaka yawashe mitambo yake tulilazimika kuyajazia mafuta au gesi kwa gharama zetu halafu umeme yanatuuzia (yanamuuzia tanesco) kwa bei ya USD 1 kwa unit. Tanesco ilibidi atuuzie umeme huo kwa USD 0.3 kwa unit, bei ya hasara (subsidized) kwani hatungaliweza bei hiyo ya USD 1 per unit. Tukayatimua, tukalipa gharama ya kuyatimua ya USD 100 tu kupitia award ya ICSID. Sasa shirika letu la tanesco linapata faida ya shillingi trillion 15 kwa mwaka kwa kutuuzia umeme kwa bei ya 12 cents USD kwa unit. Lengo ni kuwa umeme wa JNHPP utakapoanza kuzalishwa gharama ya umeme tutakaouziwa utakuwa chini ya senti tatu USD, sawa na ile ya nchi zingine za viwanda ili tuweze kushindana nazo. Akina Maharage wakituzingua kwa hili tuna uwezo wa kuwazingua pia.
 
Sasa unamlilia nani? We si umeshakula 0.125%yako hapo?
 
Akili imeanza kukuingia tena.
 
Taasisi pekee inayoweza kuibwekea serikali na ikamtii ni CCM.

Na kwa kuwa Serikali ndiyo CCM, basi kama nchi tuna hasara ya kuwa na Chama cha Hovyo cha CCM.

Chama kikiwa cha hovyo hata Wanachama wake ni wa HOVYO. Paskali ukiwepo.

Nawe ni wa Hovyo.
.
 
Shida inaanzia kwako kama mwanahabari na mwanasheria ... unapoona jamba ovu na kujifanya upo nyutro haya ndo matokeo yake
 
Hii ilipostiwa humu Jana, na ni kweli, wawekezaji wakija, wanakuja kuvuna kutokana na loop holes za sheria zetu wenyewe, ngoja tuliwe hadi mifupa ili tuamke.. ndio maana watu wa Mungu wameanza kutoa maombi hapa :
 
CCM mbele kwa mbeleee 🎶🎶🎶🎶!!
 
Hatari sana, ndio maana hata hii mikataba mingine tunapata wasiwasi nayo, maana tunajiuliza Mtanzania akili kaipata lini kujadili na kusign mikataba na nchi ikanufaika pamoja pia ikawa salama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…